Picha zilizowekwa Instagram za wasichana wakiwa wamekaa pembeni ya ndege ya polisi iliyokuwa itumike kuwabeba maofisa wa Recce kwenda kukabiliana na shambulio la Garissa zimezua utata nchini Kenya.
Picha hizo ziliwekwa kwenye akaunti ya Instagram ya Ndanu Munene Mbithi, anayesemekana kuwa binti wa polisi wa anga wa Kenya, Kamanda Rogers Mbithi.
Picha hizo zinamuonesha Ndanu akiwa na msichana mwingine kwenye matukio tofauti, moja ikiwa ni wiki 10 zilizopita na nyingine wiki 62 zilizopita.
Picha mbili zimeandikiwa maelezo, “Mombasa ni raha tu.” Na nyingine ya msichana akiwa ndani ya ndege hiyo iliyoweka 27 zilizopita imeandikiwa, “Hi Mombasa. #birthdayweekend.”
Akaunti hiyo ya Instagram iliyounganishwa na Twitter na Facebook kwa jina la Ndanu Mbithi imefutwa jana tangia picha hizo ziwekwe hadharani.
Wakenya wenye hasira jana walihoji kuhusiana na matumizi mabaya ya ndege za polisi na kwanini akaunti hizo zilifutwa.
Weekend iliyopita ilibainika kuwa ndege hiyo ya Cessna iliyokuwa iwapeleke makomando wa kikosi cha Recce hadi kwenye chuo kikuu cha Garissa hakupatikana kwakuwa ilikuwa imeenda Mombasa kwa safari binafsi bila ruhusa wa IGP.
IG Joseph Boinet amethibitisha kupokea ripoti inayothibitisha kuwa ndege hiyo haikuwepo kwakuwa ilikuwa Mombasa kupeleka watu. Ndege hiyo iliondoka Nairobi April 2 saa 1.30 asubuhi ikiwa ni masaa mawili baada ya shambulio la kigaidi kwenye chuo kikuu Garissa.
Ndege hiyo ilidaiwa kukodishwa na maafisa wa juu wa polisi kwa mfanyabiashara wa Nairobi kwa maelekezo kutoka kwa Mbithi kwenda kumchukua mke wa mtoto wake.
Picha za Instagram za watoto wa afisa wa polisi wa Kenya wakila bata na ndege ya jeshi hilo zazua utata!
0
April 15, 2015
Tags