Askofu wa Kanisa la Ufufua na Uzima Josephat Gwajima amelitikisa tena Jiji la Dar es Salaam leo mara bada kuwasili makao makuu ya Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam ili kuendela na mahojiano kuhusu tuhuma za kumkashfu Askofu Pengo.
Gwajima amewasili leo Kwenye Makao Makuu ya Jeshi la polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Majira ya saa mbili kamili asubuhi huku akisindikizwa na viongozi mbali mbali wa Kanisa la Ufufuo na Uzama pamoja na Mwanasheria wake .
Eneo lote la kituo hicho cha polisi lilikuwa chini ya ulinzi mkali wa maofisa mbalimbali wa Usalama wa Taifa wakisaidiwa na Jeshi la Polisi.
Baada ya kuwasili kituoni hapo, umati mkubwa wa Waumini wake ulizunguka maeneo yote ya Kituo hicho huku wengine wakiwa maeneo ya stendi ya Treni ya Reli ya kati.
Kama kawaida, Waumini hao walikuwa wakiimba nyimbo mbalimbali ambazo wanadai zilikuwa mahususi kumpa nguvu Askofu huyo ajipu kesi hiyo kwa ufasaha.
Baada ya Mahojiano ya takribani masaa Matano, hatimaye Askofu Gwajima alitoka ndani ya kituo hicho,lakini katika hali isiyo ya kawaida,Askofu huyo aligoma kuongea na vyombo vya habari.
Baada ya Gwajima kugoma kuongea,mwandishi wetu alimfuata Mwanasheria wake aliyekuwa ameambatana naye,Paul Mallya ambaye alisema kuwa mteja wake alikuwa amechoka, hivyo asingeweza kuongea.
Mallya alimweleza mwandishi kuwa mambo aliyohojiwa Gwajima leo ni kuhusu mali zake na sio matamshi ya kumtukana Askofu Pengo.
“Askofu kahojiwa maswali mengi tena sio ya kuhusu kumtukana Askofu Pengo.Wametaka hati ya Helikopta yake anayomiliki,hati za kanisa lake na hati za viwanja vyake ambavyo ameambiwa avipeleke wiki ijayo,” alisema Mwanasheria Mallya.
Mallya aliongeza kuwa kutokana na Afya ya mteja wake kuwa mbaya , mahojiano yake yameahirishwa hadi wiki ijayo.
Huyu ni msanii na mwizi mkubwa kwa sadaka za waumini wake
ReplyDeleteANAJUTA SASA KUMTUKANA PENGO
ReplyDeleteKatajirika na pesa za mwaga mwaga
ReplyDeleteSIKU ZOTE BARE THIS IN UR MIND"USILE NA KIPOFU UKAMSHIKA MKONO
ReplyDelete