Ray C Akana Tetesi Kuwa Ameanza Kujisogeza Tena Kwa Lord Eyez Aliyemfundisha Kutumia Unga, Asema Haya

Ngoma mpya itakayotoka hivi karibuni ambayo Lord Eyez amemshirikisha Ray C haimaanishi kuwa mastaa hao waliowahi kuwa wapenzi wamerudisha ukaribu wao.

Kwa mujibu wa Ray C, wimbo huo ulirekodiwa miaka 7 iliyopita.

Ray C amepost picha hii kwenye Instagram na kuitolea maelezo hapo chini

Mambo iende kwa wote wanipendao!Naomba tu kuwajulisha kuwa Nimeskia Lord Eyes anakaribia kuutoa wimbo uitwao Matatizo ambao alinishirikisha!Najua wengi wanaweza tafsiri vingine lakini Niwambie tu kwamba Huu wimbo tuliurekodi miaka SABA ILiopita nchini Kenya kipindi tuko pamoja na si kipindi cha hivi karibuni!Nimeona niongee tu maana naona magazeti yashaanza Udaku,” ameandika Ray C kwenye Instagram.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad