Imetusikitisha sana kumbe nyuma ya kashfa alikuwa akidaiwa Askofu Gwajima juu ya Kardali Pengo ilikuwa ni ufunguo tu wa serikali kuingilia Imani na Utendaji wa Viongozi wa kidini (Askofu Gwajima) Iweje kashfa iliyokuwa inamuhusisha Kardinali Pengo na Askofu Gwajima ipelekee kuhojiwa na Kudaiwa alete nyaraka zinazohusiana na mapato na matumizi ya Kanisa la ufufuo na uzima, Kwani makanisa huwendeshwa na ruzuku kutoka serikalini !?, Je!
Kuna kanisa au dhehebu lolote la kidini wawe waislam au wakristo wameisha wahi kuhojiwa kuhusu mapato na matumizi ya madhehebu(makanisa/misikiti) yao?
Wanapohoji nyaraka za helicopter kwani! Iliingia nchini kwa uficho!?.... Kwanini wasiene kuuliza TRA kama helicopter hiyo haikulipiwa ushuru ?
Kumbe tumegundua serikali na wanasiasa walioko madarakani wanaajenda ya siri juu ya Askofu Gwajima. Nchi yetu ina mambo mengi ya kushughulikiwa na serikali ili kutatua matatizo ya wananchi kama vile vifo vya albino, migogoro ya wakulima na wafugaji, matumizi mabaya ya fedha(ESCROW) na mikataba mibovu isiyo na manufaa kwa mtanzania mmoja mmoja .
Mambo kama haya kama ya Sakata la Escrow na Epa yangekuwa yanafuatiliwa kwa karibu kama anavyofuatiliwa Askofu Gwajima ingeleta tija kwa uongozi uliopo madarakani na Imani kwa wananchi juu ya serikali yao.
Duh!! Yani mdau hapo umeongea ukweli mimi si mkristo lakini nawaunga mkono sana wakristo kwa hilo kutokana na kunyanyaswa kwa gwajima mali za gwajima haziwahusu waongelee vp watawadifend maalbino kwanza.
ReplyDeleteNa wale mafisadi serikalini wangekua wanasumbuliwa kama hivi basi ufisadi ungeisha
ReplyDeleteviongozi wetu wapo tayari kuingia gharama yoyote kwa ajili ya kukomoa watu kuliko kufanya mambo ya maendeleo ya wananchi......
ReplyDeleteHakuna inyanyasaji wowote Hawa maaskofi ndio tatizo LA taifa hawana elimu yyte Kubwa dini wanakula pesa za walokore na serikali kibaya zaidi wengi wao wanaimbia serikali nini lakufanya mwandishi wewe ni mmoja wa watetezi wa wakristo sorry
Deletekazidi kutukana watu huyo mwacheni ashughulikiwe alimtukana CAG akanyamaziwa akarudia kwa pengo kesho atamtukana mpaka rais, afungwe tuu
ReplyDeleteTatizo la nchi. Zisizoendelea na zinazojiata masikini, kutokana na ujinga wa mawazo na kufikiri na ideolog mind, bran wash, yaani tumetawalinda na kila kitu kwenye ubongo wetu, usioweza kupambanua, tu raisi kuamini hata, hata ujing ujinga tu, sasa huyu gwajima hata wakitafuta utajili wake, utawasaidia nini? kwa kuwa utajili wake huko wazi, ni hela za michango anayopata toka kwa waumini wake, tuna acha kudeal na viongozi wabovu, wanaloliangamiza Taifa kwa ufisadi, wizi, ubadhirifu wa mali za umma, na uongozi mmbovu, kila kukicha utasikia mabilioni yameibiwa lakini hataa, awawajibishwi, na lii nchi linazidi kupolomoka kwa umasikini uliokithili, hamna Elimu nzuri, huduma za hafya mbovu, kila secter ni ubovu ubovu tuuu, lakini wala awashuguliki na hayo, wanashugulika na mtu, ambae wanajua mapato yake yametokana na nini? hajaiba hela za kodi, hao waumini wake ndio waliomtajilishaa, kama ni ujinga ni wao. Wanawashindisha watoto wao na njaa, wanamtajilisha kiongozi wao, ni yao na shauri yao, Sasa tunalishaaa hili li nchi la Tanzania lenye utwala wa kidikteta, baada ya kudeal na watu wasiopenda maendeleo ya hii, nchi , wao wanashughulika na mtu anaetumia jina la mungu kujipatia kipato, wala hajaiba, si muwaulize waumini wake kama wameibiwa watasema
ReplyDeleteMdau 2;20 kulaumu na kukejeli taifa zima hakufanyi mawazo yako yawe na hekima Bali ni uzaifu wa kutoelimika na kujaribu kulazimisha taifa Zima likubaliane na wewe serikali ina makosa men gi tu na Kubwa zaidi ni hawa maaskofu feki ambao wanashurutisha serikali ifuate Matakwa Yao ngajima anastahili kushughulikiwa huwezi kumtukama kadinal pengo harafu uwachiwe kisa waumini awajasema kama wanaibiwa sasa hiyo ndio real brain washed
ReplyDeleteGwajima ni mwizi kwa kupitia jina la mungu.Halafu taperi kama wengine. Nakubari awasilishe hizi document Polis.
ReplyDelete