Sakata la Gwajima: Serikali Inapoamua Kukumaliza Baada ya Kuchanganya Dini na Siasa

Ishu ya Gwajima ni kama ndio imeanza upya baada ya kutakiwa kuleta nyaraka kumi muhimu, zikiwemo returns za hesabu zake za kanisa, bodi ya wadhamini, hati ya usajili wa kanisa, namba ya utambulisho, jumla ya makanisa yake, mali anazimiliki nk 

Kwa juu juu ni rahisi kuona hili ni jambo jepesi lakini kiuhalisia huu unaweza kuwa mwanzo wa mwisho wa enzi za gwajima. Kila nyaraka atakayoleta itachambuliwa kwa vigezo vyote na kwakweli nyingi ya nyaraka hizo (kama zitakuwepo) zitakuwa na mushkeli

Na mushkeli utakaotokea kwenye kila nyaraka utaangaliwa kwa jicho la kisheria na adhabu zake, hii ni msiba kwa yoyote yule ambaye anafanyiwa ukaguzi na serikali, yataibuka mengi mengi ambayo hayajulikani, kuanzia mamlaka ya mapato, vyeti na usajili, uhamiaji, taratibu za kuendesha kanisa nk nk

Pamoja na kashfa zake nyingi lakini hii ishu ni ya kisiasa zaidi, na hii inatokana kuweka wazi msimamo wake bila woga wa kuwaunga mkono watu wawili muhimu kwenye uchaguzi mkuu ujao Lowassa na Dr Slaa, hawa wawili hawa ni homa mbaya kwa ccm kwasasa, yeyote atakayefanikiwa kuchukua madaraka ni kiama kwa ccm, japo El yupo ccm

Gwajima anaponzwa na kujiamini kulikopitiliza na kuchanganya na siasa za makundi, hawatamuacha hadi wahakikishe wamemmaliza kabisa

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad