Kumekucha!
Kundi la Wanamgambo wa Al-Shabaab wa nchini Somalia, Leo tarehe 4/4/2015 asubuhi na mapema, wametoa TAMKO lao kuhusiana na mfululizo wa matukio ya kushambulia nchini Kenya na sababu za wao kufanya hivyo, huku wakieleza dhamira yao ya kuendelea kufanya matukio zaidi iwapo madai yao hayatatimizwa na Serikali ya nchi hiyo.
Madai Makuu ya msingi ya Al-Shabaab waliyoainisha kwenye Tamko hilo, wamesema Serikali ya Kenya imekuwa ikiwaua Waislamu kwenye Ukanda wa Afrika Mashariki, huku wakitolea mfano wa historia ya Mauaji ya kutisha ya Waislamu yaliyotokea katika miji ya Wagalla na Garissa ambapo wamedai zaidi ya Maelfu ya Waislamu waliuawa na kuacha makovu yasiyofutika kwa ndugu na jamaa wa wahanga hao.
Pia, wameshutumu Majeshi ya Kenya kwamba yamekuwa yakiwafanyia vitendo vibaya raia wa Kiislamu wa Somalia vikiwemo ubakaji, mauaji na udhalilishaji wa wanawake wa Kiislamu kwa 'baraka' za serikali ya Kenya.
Zaidi katika tamko hilo, Wanamgambo hao wamedai kwamba iwapo Serikali ya Kenya haitaacha kuwatendea unyama Waislamu, basi wataendelea na mashambulizi yasokwisha!
Hii sasa ni kali
ReplyDelete