Tanzania tuliivamia DRC kuwatoa M23 mbona kigugumizi kuwang'oa Alshaabab?

Nimekuwa nikishawishi serikali yetu mara kadhaa kuwa kuna haja ya Tanzania kuivamia Somalia kijeshi kwa kushirikiana na majeshi mengine ya Afrika yaliyoko Somalia ili kuwang'oa Alshaabab.

Kuna haja ya sisi watanzania kufanya hivyo kwani kwa sasa ni dhahiri ndugu zetu wa Kenya wanakaribia kuzidiwa nguvu na hawa alshaabab.

Ikumbukwe wakati alshaabab wanaanza harakati zao walikuwa wanateka meli tu ambazo zilikuwa zinapita pwani ya Kenya na Somalia na kuteka watalii kisha kutoa rai ya kubadilishana mateka na fedha.

Kwa sasa wamejipanua na kutaka kuanzisha jamuhuri yao hivyo kuwa tishio zaidi huku wakijipambanua kwa mgongo wa uislamu!

Na endapo wakiachwa watawale kama wanavyofanya sasa baada ya muda pwani nzima ya Afrika mashariki haitokuwa salama tena.

Kuna vitisho kadhaa ambavyo hufanya alshaabab endapo unaenda kwenye ardhi yao kuwapiga kama vile kutoa maneno ya vitisho, kufanya mashambulizi ya kushtukiza kwa raia na kutesa wanajeshi wanaowakamata/kuwateka.

Mfano, Marekani ilipoivamia Somalia kuwapiga alshaabab, kwa bahati mbaya alshaabab wakamkamata askari mmoja wa Marekani, wakamuua kikatili kisha kuanza kumburuza akiwa amefungwa nyuma ya gari mitaani Mogadishu. Baada ya kuona tukio lile raia wa Marekani wakapiga makelele serikali yao iwaondoe askari walioko Somalia. Kweli askari wengi wakarudishwa Amerika. Kitisho kile kikawa kimefanikiwa.

Wametoa vitisho pia mara kadhaa kwa serikali ya Kenya na Uganda kwa kuwavamia na kuua raia wao mara kadhaa kama ile ya westgate, Garissa, nk.

Tusiogope vitisho tuna jeshi imara ambalo halina shaka na tumelipa sifa kila uchao.

Twendeni Somalia!!

Shukrani A. Ngonyani,

Dar Es Salaam,

April 9, 2015.

00255784 37 97 99

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Katika watu wenye akili ndogo hapa duniani na wewe ni mmojawapo, ni nadhani una malengo yako binafsi, wewe unataka tuvamie somalia kwa sababu gani? kwa faida gani? je tumejiandaa na uvamizi wa kuvizia wa al shabab kwa kiasi gani? Hakika lengo lako ni baya na tunachoshukuru Mungu viongozi wetu wanajua kwamba kupeleka majeshi Somalia ni jambo la hatari na lisilo na tija kwa taifa letu. Hatuwezi kuzuia vita vyote duniani, tunaweza tu kujilinda pale tutakapochokozwa, Admin/Mmiliki wa udaku specially nafikiri imefika wakati watu wanaotuma andiko lililokaa kiuchochezi zisichapishe hapa ubaoni.

    ReplyDelete
  2. LABDA WATUCHOKOZE NDIO TUWATANDIKE

    ReplyDelete
  3. Kama mlivyojitia kiherehere na propaganda za kujipendekeza kwenye vita vya kagera,emb wapelekeni MBWA wenu Somalia tulianzishe,cha kwanza itakuwa ni lile genge la wahuni(bunge) kusambaratika.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Una akili za kuokota matambara,Pumbavu wee anonyymous 11.05.

      Delete
  4. Wewe anonymous 11.05AM wacha kutishia watu nyau na kujisifia ujinga na wala usidhanie kuvamia soft target ndio ubingwa. Nyie ni wahuni tu au sawa na panya road tu hamna uwezo wa kushinda vita yyte. Sana sana mtawaua wasio na hatia na huo sio ushindi kwa sababu mtaendelea kuishi porini na mapangoni miaka yote mkijificha. Kama vidume kweli mbona hamji kibabe mchana kweupe tuwaone jeuri yenu? Nyie ni wanyama wa porini mtasumbua ndio but mtaishia pabaya mmoja mmoja.

    ReplyDelete
  5. YAANI WEWE ADMINI HUYO ALOANDIKA ARTICLE HII HAJIELEWI,..MAREKANI MWENYEWE MPAKA LEO HATAKI KUISIKIA SOMALIA ITAKUWA SISI...MAREKANI KAKIMBIA SOMALIA WEWE UTAWEZA...WE MWENYEWE ULIEANDIKA UJINGA HUU UKIAMBWA SHIKA BUNDUKI TWENDE VITANI UTAANZA KUJILIZA..

    ReplyDelete
  6. Kule somalia kuna jeshi la kenya,amison ambao wapo warundi,waganda wanyyarwanda..kuna jeshi la ethiopia na drons za wamarekani halafu kuna wazungu wengi tu wakitoa ushauri na bado alshabab wana eneo kubwa zaidi ya hayo majeshi yote...hao watu sela yao ni ama kufa au kushinda..lau mngejua majeneza yanayorudi kwa nchi nilizozitaja hapo juu usingethubutu kutamani jeshi kwenda somali.

    ReplyDelete
  7. ashindwe na alegee atuache tuishi kwa amani

    ReplyDelete
  8. wewe ni mpumbavu

    ReplyDelete
  9. mi nisha copy no yake naona kama hapa hataona vile nataka mwambia yani uyu ngonyani kweli anawaza kama herufi tano za jina lake baada ya ngo jinga kabisa!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad