Diamond Platnumz amewasihi wasanii wa Tanzania kuacha kulalamika kutawaliwa na muziki wa Nigeria bali wanatakiwa kutoa ngoma kali kuwapa ushindani.
Diamond alitoa kauli hiyo kwenye 255 ya XXL kupitia kituo cha redio cha Clouds FM.
“Unajua huwezi kuwalaumu tu Wanigeria, wao walitumia taaluma yao na technique zao ili kuteka soko, sasa ukionekana unamind utaonekana pia hauna akili ya kibiashara,” alisema.
“Cha muhimu nikuhahakikisha unatoa nyimbo kali ambayo itasikika yako na kuifunika hizo za Nigeria.
“Tunatakiwa wasanii wa bongo kutoa ngoma kali ili mashabiki wapende maana huwezi kumzuia Dj asipige nyimbo za Nigeria maana mashabiki wanaomba inabidi na sisi tufanye hivyo ili uombwe muziki wetu zaidi. Mfano zamani zilikuwa zinafanya vizuri nyimbo za Kongo lakini baada ya kuanza kutoa ngoma kali sasa hivi huzisikii tena kama zamani.
"Inabidi pia sasa hivi tufanye hivyo tusilalamikie ma Dj tu, naamini sasa hivi muziki wa Tanzania umeshakua. Kinachotakiwa ni kuzuia soko la nje lisiteke muziki wa Bongo kwa kutoa kazi nzuri zaidi,” alisisitiza.
Tusiwachukue Wanaijeria, Tutoe Ngoma kali Tutaenda nao Sawa – Diamond
0
April 21, 2015
Tags