KIKAO cha viongozi wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kimeshindwa kuendelea baada ya baadhi ya wajumbe kushindwa kuafikiana kuhusu hoja iliyowasilishwa na Chama cha NCCR-Mageuzi, ya kutaka kujitoa kwenye umoja huo, imefahamika.
Viongozi hao walikutana jijini Dar es Salaam jana katika Ofisi Kuu ya Chama cha Wananchi (CUF), ambapo pamoja na mambo mengine walikuwa wakijadili hatima ya kuachiana majimbo kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.
Katika kikao hicho ambacho kilitarajiwa kuanza saa 4 asubuhi kama ilivyokuwa imepangwa na badala yake kilianza saa 6 mchana, ajenda kuu zilikuwa ni kujadili namna ya kuachiana majimbo ambayo bado mwafaka haujapatikana pamoja na utaratibu wa kumpata mgombea urais kupitia Ukawa.
Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya kikao hicho kilichokuwa chini ya Mwenyekiti mwenza wa Ukawa, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, kilishindwa kutoa mwelekeo wa majimbo 18 yenye mvutano huku kila chama kikitaka kugombea kivyake.
Hata hivyo hoja hiyo iliibua mvutano mkali baina ya wajumbe wa kikao hicho ambapo kwa upande wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ujumbe wake uliongozwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe, Katibu Mkuu Dk. Willibrod Slaa na Mwanasheria Mkuu wa chama hicho Tundu Lissu.
Kwa upande wa CUF, ujumbe wake uliongozwa na Profesa Lipumba, Naibu Katibu Mkuu Bara, Magdalena Sakaya na Naibu Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi, Shaweji Mketo.
NCCR-Mageuzi kiliongozwa na Mwenyekiti wake James Mbatia ambaye baada ya kuwasilishwa hoja ya chama chake alishindwa kuendelea na kikao na kulazimika kutoka nje ya ukumbi wa mikutano.
“Mwanzo tulianza kujadili suala la uandikishaji wapigakura kwa mfumo wa BVR na changamoto zake zilizojitokeza pamoja na hatima ya uwezekanao wa kuwapo kwa Uchaguzi Mkuu Oktoba, mwaka huu.
“Pia tulijadili kwa kina mwendelezo wa ugawaji wa majimbo yaliyobaki, lakini hata hivyo tuliacha ajenda hiyo kutokana na kuibuka kwa hoja nzito kwa kila upande,” kilisema chanzo chetu ambacho hakikutaka kuandikwa jina lake.
Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho zinapasha kuwa ilipotimu saa 7 mchana, aliingia Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, Mbatia, ambaye alishiriki katika hatua za awali za majadiliano hayo, lakini ilipofika saa 9:20 aliondoka kabla kuwasilishwa hoja ya chama chake kutaka kujitoa Ukawa.
Hata hivyo wajumbe walishindwa kuendelea na kikao hicho kutokana na NCCR-Mageuzi kutokuwa na mjumbe ambaye angeweza kueleza kwa undani sababu za kutaka kuchukua uamuzi wa kujitoa.
“Hoja iliyokuwa katika ajenda ni ya NCCR-Mageuzi waliyowasilisha ya kutaka kujitoa Ukawa na dai lao kuu ni kutotendewa haki kwa baadhi ya mambo, hasa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliopita.
“Na hili jambo si geni kwani mnapokuwa kwenye jumuiya yoyote inawezekana ikatokea hali ya kutoelewana kwa baadhi ya wajumbe kwa kuona kuna sehemu kuna mmoja anaona hajatendewa haki.
“Na jambo ambalo lilitakiwa ni kuzungumza na kulimaliza ili watu wasonge mbele, na NCCR-Mageuzi walileta kama malalamiko… siwezi kulizungumzia vizuri kwa sababu halijazungumziwa kwa undani kwenye kikao,” kilisema chanzo chetu.
Mtoa habari wetu alisema kikao hicho kilitarajiwa kumalizika jana usiku, lakini kutokana na hoja ya NCCR-Mageuzi, ilimlazimu Mwenyekiti wa kikao hicho Profesa Lipumba kukiahirisha saa 11 jioni hadi leo ambapo kitaendelea.
Ukawa inaundwa na vyama vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD kinachoongozwa na Dk. Emmanuel Makaidi.
Hivi sasa joto la kuwatangaza wagombea urais ndani ya vyama vinavyounda Ukawa pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM) linazidi kupanda huku kila upande ukimvizia mwenzake katika kutangaza mgombea nafasi hiyo.
Hatua hiyo imekuja baada ya viongozi wa Ukawa katika mkutano wao na wanahabari kueleza kuwa mgombea wao atatangazwa Machi mwaka huu, lakini hadi sasa imepita miezi miwili bila kumtangaza.
Wakati hayo yakiendelea ndani ya Ukawa, CCM nayo hadi sasa imeshindwa kueleza ni lini atapatikana mgombea wake pamoja na kutangazwa kwa hatima ya makada sita wa chama hicho ambao wanadaiwa kuanza kampeni kabla ya wakati.
Credit: Mtanzania
duhh!! tamaa mbele... thus way hata cku moja hatufanikiwi ama kufikia malengo..na sio tu kwenye siasa mpka kwenye sanaa ni hivyo hivyo tunakosa umoja wa dhati umbao utasimama km watu flani kutetea hoja flani...TAMAAA
ReplyDeleteTatizo Mbatia atawamaliza nyie mnadai Zitto anawasaliti lakini huyo Mbatia hatari mno Tundu Lisu kimya mnacheza na political science, Chadema jitoe Mzee Slaa busara iko wapi na wewe unaburuzwa kweli mbona mnatutia aibu. Mtayakosa majimbo kibao kwa stail hii na ACT itakuwa chama kikuu, shauri yenu msiposikiliza ushauri.
ReplyDeleteMLIPO TOKA NI MBALI SANA NINAOMBA MKUBALIANE HAYO MAJIMBO 18 SI MENGI KAMA MENGINE MMEYAWEZA BASI BUSARA ITUMIKE
ReplyDeleteyah ndugu zangu watanzania imefikia mahali tuwe tunajuuliza maswali ya msingi na tuyapatie majibu ya msingi hivi Vyama vya upinzani vinatakiwa viwe ndio vinara wa kuenzi na kuendeleza demokrasia na hata waanzilishi wake walikuja na hoja hiyo baada ya kuona kuwa mfumo wa chama kimoja uliwanyima fursa ya kutoa mawazo na hata nafasi ya kuonyesha uwezo wao wa kuongoza!.sasa siku za karibuni kuna mambo yaliyotokea ambayo mimi binafsi nawaomba watanzania wenzangu tuwe washabiki wa timu za mpira lakini tusikubali kuwa washabiki wa siasa nikimaanisha kuwa siasa ndio uhai wa taifa letu na italeta tija kama tuataamua kufanya tfakuri za kina kwa kila hatua na kutoa maaumuzi sahihi. Ni hvi walianza NCCR-Mageuzi pale David kafulila alipojaribu kuonyesha nia na dhamira ya dhati ya kuomba nafasi ya juu ya uongozi alitimuliwa uanachama likja suala la Hamad Rashid wa CUF naye alipotaka kutumia demokrasia inayodaiwa ipo ndani ya vyama vya upinzani kuomba uongozi wa juu naye alitimuliwa uanachama! likaja suala Zitto kabwe wa Chadema naye ametimuliwa uanachama kwa kuwa na uroho wa kutaka madaraka sasa hapa kwenye la Zitto nawaomba wanachama wa chadema wafananishe madai ya kabwe na marehemu chacha wangwe kama yanafanana wafanyie kazi kama hayafanani basi Zitto ni msaliti. Ndugu zangu kazi ya vyama vya upinzani haiwezi kuishia kwenye kuzodoana na kuitana mafisadi na chama tawala mimi ninafikiri ni vizuri hvi vyama vikaja na njia mbadala wa kuyakabili matatizo yetu kwasababu nina imani kabisa kuwa matatizo tuliyo nayo yanatatulika. Kwa mfano hapo siku za nyuma chadema walianzisha M4C na wakachangisha mamilion ya pesa ila wakayatumia kuzunguka na helicopter na magari nchi nzima wakiimba wimbo wa mafisadi lakini hebu tufikiri je isingekuwa busara kuanzisah jambo kama hilo wakajenga mashule hospital na vyuo na je mwitikio usingekuwa mkubwa? ndugu zangu tufike mahali tuamue kufikiria wenyewe badala ya watu kutusaidia kufikiri!
Deleteyah ndugu zangu watanzania imefikia mahali tuwe tunajuuliza maswali ya msingi na tuyapatie majibu ya msingi hivi Vyama vya upinzani vinatakiwa viwe ndio vinara wa kuenzi na kuendeleza demokrasia na hata waanzilishi wake walikuja na hoja hiyo baada ya kuona kuwa mfumo wa chama kimoja uliwanyima fursa ya kutoa mawazo na hata nafasi ya kuonyesha uwezo wao wa kuongoza!.sasa siku za karibuni kuna mambo yaliyotokea ambayo mimi binafsi nawaomba watanzania wenzangu tuwe washabiki wa timu za mpira lakini tusikubali kuwa washabiki wa siasa nikimaanisha kuwa siasa ndio uhai wa taifa letu na italeta tija kama tuataamua kufanya tfakuri za kina kwa kila hatua na kutoa maaumuzi sahihi. Ni hvi walianza NCCR-Mageuzi pale David kafulila alipojaribu kuonyesha nia na dhamira ya dhati ya kuomba nafasi ya juu ya uongozi alitimuliwa uanachama likja suala la Hamad Rashid wa CUF naye alipotaka kutumia demokrasia inayodaiwa ipo ndani ya vyama vya upinzani kuomba uongozi wa juu naye alitimuliwa uanachama! likaja suala Zitto kabwe wa Chadema naye ametimuliwa uanachama kwa kuwa na uroho wa kutaka madaraka sasa hapa kwenye la Zitto nawaomba wanachama wa chadema wafananishe madai ya kabwe na marehemu chacha wangwe kama yanafanana wafanyie kazi kama hayafanani basi Zitto ni msaliti. Ndugu zangu kazi ya vyama vya upinzani haiwezi kuishia kwenye kuzodoana na kuitana mafisadi na chama tawala mimi ninafikiri ni vizuri hvi vyama vikaja na njia mbadala wa kuyakabili matatizo yetu kwasababu nina imani kabisa kuwa matatizo tuliyo nayo yanatatulika. Kwa mfano hapo siku za nyuma chadema walianzisha M4C na wakachangisha mamilion ya pesa ila wakayatumia kuzunguka na helicopter na magari nchi nzima wakiimba wimbo wa mafisadi lakini hebu tufikiri je isingekuwa busara kuanzisah jambo kama hilo wakajenga mashule hospital na vyuo na je mwitikio usingekuwa mkubwa? ndugu zangu tufike mahali tuamue kufikiria wenyewe badala ya watu kutusaidia kufikiri!
ReplyDelete