Wiki iliyopita, Rais Kikwete akiwa Marekani, wakati akihutubia kwenye taasisi ya Wood Wilson International Center for Scholars alielezea mafanikio na changamoto alizokumbana nazo wakati wa uongozi wake wa miaka 10 unaomalizika Oktoba, mwaka huu na kusema:
“Wakati unaingia Ikulu unakuwa na shauku kubwa sana pamoja na furaha ya ushindi, lakini hakika urais ni kadhia kubwa. Ukipata fursa ya kuwa rais kwa awamu mbili kama mimi nadhani zinatosha kabisa. Nimefanya mengi kwa nchi yangu atakayekuja ataendeleza nilipoishia.”
Kauli hiyo ya Rais Kikwete imekuja wakati makada wa CCM wakipigana vikumbo kuwania urais.
January Makamba:
"Nilitangaza nia hiyo huku nikiwa nafahamu kwa asilimia 100 uzito wa jambo hilo... kufahamu changamoto hizo ndiyo moja ya vitu vilivyonisukuma kuchukua uamuzi huo,” alisema.
Sumaye:
“Kama mtu ameamua kuwania nafasi hiyo ina maana anafahamu anachokitaka. Tunajua ziko changamoto na namna ya kukabiliana nazo kwa hiyo hakuna sababu ya kuwa na wasiwasi.”
Dk Kigwangalla alisema:
“Kauli kama hiyo haiwezi kumvunja mtu moyo, ari itabaki palepale tu kwa aliyetangaza nia. Aliyetangaza nia anataka kutoa utumishi wake kwa nchi yake kama mimi.”
Udaku Specially Blog
Maoni yako
KAURI YA RAIS KIKWETE HAINA MAANA YEYOTE ZAIDI YA KUJISIFIA MAJUKUMU AMBAYO YALIMSHINDA. KAMA ALIONA UGUMU WA KUWA IKULU KWA NINI ASIJIUZURU KABLA? WATU KAMA HAWA HAWAFAI KUONGOZA NCHI..NYERERE ALISEMAGA IKULU SIO SEHEMU YA KUKIMBILIA,,
ReplyDeleteAMEKAA KIWIZI WIZI TU!
ReplyDeleteTAMAA YA UTAJIRI AMEISHAUPATA SASA ANAWAACHIENI NCHI YENU FULL OF MADENI WALALAHOI MLIPE WAO BATA KWA MRIJA KWA KWENDA MBELE
ReplyDelete