Waislamu Watoa Tamko, Kusomwa kila Msikiti Ijumaa kuhusu Tamko la Maaskofu, Kunyimwa Dhamana Kwa Mashehe na Issue ya Madrassa

SIKU chache kupita baada ya Mkutano wa 19 wa Bunge kumalizika,na serikali kuutupia mbali mswaada wa sheria ambao unaruhusu kuwepo makakama ya Kadhi nchini kutajadiliwa kwenye mkutano huo.

Nayo Jumuiya na Taasisi za Kiislam nchini wameibuka na kutoa tamko zito kwa kuwataka waislam wote nchini kutoshiriki kwenye kura ya maoni ya kupitisha katiba pendekezwa Bunge Maalum la Katiba,kwa madai kwamba serikali haina nia nzuri na waislam nchini kwa kitendo chake cha kukataa kuwepo mahakama ya Kadhi nchini.

Vilevile Taasisi hiyo imewataka pia waislam wote kujitokeza kujiandikisha kwenye Daftari la wapiga kura na kujiandaa kufanya uamuzi mgumu ambao wanasema hajawai fanywa na waislam nchini tangu taifa kupata Uhuru.

Akisoma Tamko hilo lenye kura sita jana jioni kwenye msikiti wa Kichangani uliopo Magomeni Jijini Dar es Salaam ,Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi ya Kiislam nchini Sheikh Mussa Kundesha kwa niaba ya asasi za kiislam 11 zinazounda umoja huo na kushuhudiwa na Mamia ya waumini wa dini hiyo pamoja waandishi wa Habari ambapo Sheikh Kundesha alisema-

Waislam wote nchini wamechoka na uonevu wanaodai kufanyiwa na Serikali iliyoko madarakani kwa kitendo cha kuondo Mswaada wa Mahakama ya kadhi Bungeni ambapo alisema ni kuendelea kuchochea vita ya kidini nchini.

“Kuna kila sababu ya kuamini kuwa Serikali ya CCM imeshindwa kulishughulikia suala la mahakama ya Kadhi katika uhalisia wake kama ilivyoahidi kupitia ilani yake kwenye uchaguzi ibara ya 108 (b) mwaka 2005 na sasa inafanya hadaa za kisiasa kuwadanganya waislam ili waonekane inalishughulikia suala la mahakama ya Kadhi kama walivyoahidi”

“Kwa ubabe huu wanaotufanyia waislam sasa tunawaomba waumini wote wa kiislam nchini kutoipigia kura katiba pendekezwa kwasababu sio katiba nzuri kwa waislam harafu tunawataka kila mmoja aliyetimiza miaka 18 ajiandikishe kwenye Daftari wa wapiga kura kujiandaa kufanya uamuzi mgumu ambapo utalitikisa nchi”alisema Sheikh Kundesha.

Alisema kuwa kitendo cha Serikali kuwatambua Makadhi wa Bakwata pamoja wanachosema ni ‘Mahakama hewa ya Kadhi’ chini ya Bakwata ni kinyume na Katiba ya nchini ibara 19(1) na (20) kwa kuwalazimisha waislam wawe chini ya Bakwata ambapo wanasema hawatakubaliana nalo.

KUHUSU TAMKO LA MAASKOFU.
Pia katika Tamko la Taasisi hiyo kiislam ambapo litasomwa kila msikiti Ijumaa wiki hii nchi nzima pia wamezungumzia Matamko mawili yaliyotolewa Jukwaa la kikiristo nchini ambapo Taasisi hiyo ya Kiislam wameonyesha masikitiko yao kwa kusema ni dhahili hapa nchini kuna serikali dhaifu kwa kuwaacha maaskofu kutoa matamko ambayo wanadai ni ya kichochezi.

“Ushahidi kwamba ni chuki tu husda ni pale ambapo hata waislam tuliopendekeza mahakama ya Kadi iwekwe kwenye Katiba pendekezwa,lakini tunashangaa hawa maaskofu wamekuwa wakiipinga Mahakama hii wakati hii dini tofauti na y a kwao na sisi waislam tumewavumilia lakini tunahoji hawa maaskofu wanataka nini”

KUHUSU KESI ZA MASHEIKH NA KUNYIMWA DHAMANA.
Pia Taasisi ya Kiislam wameonyesha kuchukizwa kwa kitendo cha Masheikh mbalimbali akiwemo shehe Ponda ambao wapo mahabusu na kunyimwa Dhamana na Serikali ila wanashangaa kitendo cha Serikali kuwamwachia Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Askofu Josephat Gwajima wanadai kitendo hicho kinaonesha Serikali kuwapendelea wakristo.

“Masheikh mbalimbali wako mahabusu wakinyimwa Dhamana bila sababu za msingi kwa kesi za uchochezi au kwa kisingizio cha Ugaidi wakati huo huo tumeshuhudia Maaskofu wakitoa kauli za uchochezi pasina kuchukuliwa hatua yeyote ikiwemo sakata la Askofu Gwajima”

KAMPENI WANAO DAI KUUA MADRASA.
Pia Taasisi hiyo wamezungumia kitendo cha Serikali kuwakamata wa Mashehe mbalimbali wanaowafundisha watoto majumbani kwa madai ya serikali kutofuata taratibu za mafunzo likiwemo matukioa tofauti yaliyotokea mkoani arusha-

Kwa kusema ni wazi serikali imejitosa kuua madrasa nchini.

“Lakini Takriban mwezi mmoja sasa,njama hizi za kuua madrasa zetu zimeibuka kwa kasi kubwa na nguvu kwa kuendesha kamatakamata ya waalimu wa madrasa zao katika hali duni majumbani mwao wakifundisha Quran na mafunzo mengine ya Uislam kama tulivyoshudia huko mkoan Moshi na Arusha”

“Tunataka Serikali itusaidie kufundisha Elimu ya dini ya Kiislam kwa mujibu wa sheria ndiyo ipi,sheria hiyo ilipitishwa lini na Bunge lipi?kwa mujibu wa Katiba ya nchi ibara 20 (1) kazi ya kutangaza dini ni suala binafsi,iweje sasa Serikali inakuja na madai haya ya kufundisha dini kinyume na Sheria kwa walimu wetu wa madrasa”

Chanzo: FullHabari Blog

Post a Comment

29 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Upuuzi mtupu. Walikosa kazi hao. Kwa mtu aliye na ufaham wa mambo hawezi hata kido kusaport huu ujinga. Watanzania wa leo wana upeo mkubwa wa kuchanganua mambo. Kwanza hamkutakiwa kuweka hapa mada km hizi.

    ReplyDelete
  2. Hawa ccm hawatishiki hata nchi nzima tusipopiga kura wao wataibuka washindi tu,kwahilo hawana hata wasiwasi.Waulizeni cuf zanzibar wanajua ccm ninani

    ReplyDelete
  3. Huyu Gwajima nilazima aende jela kama mashehe walio jela, hapa hakuna kuoneana huruma.

    ReplyDelete
  4. Waambiwe ukweli tu

    ReplyDelete
  5. Inna lillahi waina illahi rajiun

    ReplyDelete
  6. hawa wapuuzi wanataka TZ mwishoni iwe serikali ya kiislamu, wataota sana na ole wao walete fujo ka za Kenya kitaeleweka mwaka huu maana tumewalea sana hawa wajinga.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mjinga mama yako aliekuzaa

      Delete
    2. Unatamani vita??? Seriously? Hatujifunzi mataifa mengine yalivyosambaratika. Huwezi jua thamani ya amani mpk ikutoke you psych!

      Delete
    3. Waislamu wanachotaka ni mahakama ya kadhi kwakuwa ni sehemu sahihi ya kuamulia kesi za kidini tena kwa wale watakaopenda kesi zao kupelekwa huko hilo suala la serikali ya kiislamu umelitoa wapi? Watu kama nyie ndo huwa mnaleta uchochezi mbaya

      Delete
    4. ole wao, wanashabikia mahakama za kidini kwani wakristo wana mahakama za kidini??? tuache ujinga wa kutamani kuwa na utengano, na waking'ang\ania tu WAPIGWE TU, EEEEH WAPIGWE MAANA NCHI HII HAINA DINI NA ME NAAGIZA WAPIGWE TU TENA SANA....

      Delete
  7. haya ndiyo matokeo ya serikali kuyafanyia mzaha masuala ya kidini ........ mgawanyiko huu wa kidini unatokana na uzembe wa viongozi wetu

    ReplyDelete
  8. Amani idumu kama tulivyozoea,na Kama kawa kama dawa kwa wakristo ni kukesha kwa kuomba na kufunga,na
    Mungu wetu atasimama tu,kwa sababu hakuna mtu mwenye nia mbaya na nchi.

    ReplyDelete
  9. Wewe mjinga hapo juu 5:22 rudi shule kama hujui ndio nakwambia basi kwa taarifa yako uhuru wa tz umeletwa na waislam akina kinjeketile. Mwinyi mkuu. Milambo wa tabora kwa hiyo si vibaya serikali ikiwa ya kiislam huyo nyerere amekaribishwa tu ni mrundi kama wewe na wewe una chuki tu na uislam fala wewe

    ReplyDelete
  10. Sikia fujo za kenya hivyohivyo usiombe wewe zikukute endeleeni kutesa waislam tu duniani.

    ReplyDelete
  11. @Anonymous 7:16 AM.. Ni kweli kabisa! mgawanyiko huu unasababishwa na serikali. Hasa mimi namlaumu Kikwete kwa kushindwa kabisa kusimamia haya majukumu na kuliweka Taifa kwenye hali mbaya kisiasa, na pia hawa watu wa dini wangeacha mambo ya kulaumiana badala yake waungani kuikabili serikali.

    ReplyDelete
  12. Si muanzishe mahakama yenu wenyewe kwa nini mnataka iingizwe kwenye katiba? Alafu kitu kingine wanachonishangaza nacho waislamu, hapo Kenya wameuawa wanafunzi wengi lakini hawajatoa tamko lolote, ingekuwa ni waislamu ndio wameuawa ungeona jinsi wangejifanya wana upendo. Waislamu ni wanafiki sana wanajidai wanamcha Mungu lakini ni hawafanyi jinsi Mungu ameagiza wanafanya ya kwako na kumsingizia Mungu eti kasema tujitoe muhanga. Mungu alisema usiue katika amri kumi na kila kitabu cha dini kina hizo amri kwa nini wanaiondoa hiyo amri? wakiona mtu anazini ndio wanaona kosa, akiua hawajali wala hawakemei wanafurahia. Kila amri ya Mungu lazima mwanadamu aitii hupaswi kuchagua utii ipi na usitii ipi.

    ReplyDelete
  13. Si muanzishe mahakama yenu wenyewe kwa nini mnataka iingizwe kwenye katiba? Alafu kitu kingine wanachonishangaza nacho waislamu, hapo Kenya wameuawa wanafunzi wengi lakini hawajatoa tamko lolote, ingekuwa ni waislamu ndio wameuawa ungeona jinsi wangejifanya wana upendo. Waislamu ni wanafiki sana wanajidai wanamcha Mungu lakini ni hawafanyi jinsi Mungu ameagiza wanafanya ya kwako na kumsingizia Mungu eti kasema tujitoe muhanga. Mungu alisema usiue katika amri kumi na kila kitabu cha dini kina hizo amri kwa nini wanaiondoa hiyo amri? wakiona mtu anazini ndio wanaona kosa, akiua hawajali wala hawakemei wanafurahia. Kila amri ya Mungu lazima mwanadamu aitii hupaswi kuchagua utii ipi na usitii ipi.

    ReplyDelete
  14. Ni kweli kabisa waislam tuna subra sana lakini uonevu umezidi naungana na mawazo yako shekhe asilimia 100 swali kwani Tanzania ni yawakristo peke yao na kwa nini waingilie mahakam ya kadhi haielweki au hii nchi inaongozwa na mfuko wa kristo na gwajima ndio nani ?

    ReplyDelete
  15. Enyi mnaotaka mahakama ya kadhi hamieni nchi za kiarabu mkafanye udini wenu huko.Kwani kipi mnachokitaka kisichohukumiwa mahakama za nchi hii.au Mnataka kuwaonea baadhi ya waumini wenu?

    ReplyDelete
  16. mnamuonea kikwete kweli kwa sababu mpole hapendi fujo lkn kila kibaya kakifanya kikwete kwa kuwa anawabana waislam anawapa wakristo kipaumbele acha yamkute day i will come waislamu tumechoka na mfumom kristo.........

    ReplyDelete
  17. mnamuonea kikwete kweli kwa sababu mpole hapendi fujo lkn kila kibaya kakifanya kikwete kwa kuwa anawabana waislam anawapa wakristo kipaumbele acha yamkute day i will come waislamu tumechoka na mfumom kristo.........

    ReplyDelete
  18. Tatizo waislam mungu wao alishakufa, sisi Mungu wetu yu hai na anaishi milele ndo maana tumetulia yeye mwenyewe anajitetea hakuna haja ya kumtetea. Ndo maana hawajiamin na ndo maana maendeleo yao finyu sana. Ni ndugu zetu but nachukia sana mambo yao.Yan hawana Mungu kabisa ndani yao

    ReplyDelete
  19. tatizo lenu ndugu zetu wakristo hamuelewi mahakama za kadhi zinafanya kazi gani hata wenzenu huku kenya walibwata hivyo mwisho wakaja kuelewa mahakama za kadhi zinatatu matatizo ya kijamii ya kiislamu kama ndoa,talaka na mirathi..na kwa atakae amua matatizo haya yatatuliwe katika mahakama ya kadhi..sasa sijui mnaropoka eti tunataka mahakama zetu.elewa kwanza ndio uanze kubwata..halafu nawasikia wengine mnasema fujo za kenya ni za kidini uvumi huo mumeutoa wapi muache kuongea mambo musioyajua aliewaambia mauaji ya kenya ni kutokana na fujo za kidini ni nani

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umeona ee. Yaan wanarukia kishabiki tu bila kuwa na elimu wasioijua. Hovyo

      Delete
  20. Kuna msenge mmoja huko juu anauliza kwani wakristo wana mahakama hiyo si dini vp iwe na mahakama? Hebu twambie mtume gani kaja na ukristo au mtume gani kaja na biblia tuacheni msituzingue nyie mnamjua jesus kuliko tunavyomjua sisi waislam? Nyie si wazushi tu subirini moto.

    ReplyDelete
  21. Kuna msenge mmoja huko juu anauliza kwani wakristo wana mahakama hiyo si dini vp iwe na mahakama? Hebu twambie mtume gani kaja na ukristo au mtume gani kaja na biblia tuacheni msituzingue nyie mnamjua jesus kuliko tunavyomjua sisi waislam? Nyie si wazushi tu subirini moto.

    ReplyDelete
  22. Mahakama za kadh zinamnyima haki mwanamke Kwaiyo hazifai

    ReplyDelete
    Replies
    1. Funny..kha! Eti zinamyima haki mwanamke. Unaelewa kilichopo katika sharia? Nyie ndo hamkandamizwi? Waume zenu ndo good cheaters kwenye ndoa zenu..hiyo ni haki? Mpk kifo kitutenganishe my foot!

      Delete
    2. Yes,mimii ni muislam lakini sitaki mahakama za kadh.
      na wako hata wabunge wengi waislam wamepinga hiyo.

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad