Watoto 147 wakutwa misikitini Kilimanjaro Wakifundishwa Dini ya Kiislam Kinyume na Sheria

WATOTO 140 wenye umri kati ya miaka 10 na 21 wamekamatwa wilayani Hai mkoani Kilimanjaro wakilelewa katika misikiti mitatu tofauti. Taarifa zilizopatikana wilayani hapa zinasema watoto hao wamekuwa wakifundishwa mafunzo ya dini ya kiislam kinyume cha sheria.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, watoto hao waligundulika baada ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Hai kupata taarifa na kuwafuatilia kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, kati ya Machi 25 na 27 mwaka huu.

Taarifa hizo zimeyataja maeneo waliyokutwa watoto hao kuwa ni Misikiti ya Masjid Bilal, Masjid Othiman na Msikiti wa Kwa Kiriwe.Taarifa hizo zimesema katika Msikiti wa Masjid Bilal uliopo Mtaa wa Kibaoni wilayani hapa, walikutwa watoto wa kiume 70 wanaotoka katika mikoa mbalimbali nchini.

Watoto wengine 50 wa kiume walikutwa katika Msikiti wa Masjid Othiman uliopo Mtaa wa Uzunguni ambao nao inasemekana wamekusanywa kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Taarifa hizo zinasema watoto wengine 27 walikutwa katika Msikiti wa Kwa Kiriwe ambako pia walikuwa wakifundishwa mafunzo ya dini ya kiislam na walimu Watanzania. Mkuu wa Wilaya ya Hai, Anthoy Mtaka, alikiri kuwapo watoto hao wilayani kwake.

“Tukio hilo lipo na wanaohusika ni watu wanaotumia mwamvuli wa dini fulani kufanya mambo yasiyofaa katika jamii. “Kwa hiyo naziomba mamlaka husika likiwamo Baraza Kuu la Waisalam Tanzania (BAKWATA) kutambua miskiti na shughuli zinazoendelea katika nyumba hizo za ibada.

“Hili lazima walifanyie kazi kwa sababu hao vijana inasemekana wanafundishwa mazoezi makali ya kareti na judo katika nyumba hizo za ibada,” alisema Mtaka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Geofrey Kamwela, alisema atazungumzia tukio hilo leo. Kupatikana kwa watoto hao ni mwendelezo wa matukio ya watoto wanaolelewa kinyume cha sheria mkoani Kilimanjaro baada ya matukio mawili ya aina hiyo kuripotiwa hivi karibuni. La kwanza lilihusisha watoto 18 na la pili lilihusisha watoto 11 waliokutwa katika maeneo ya Lyamungo wilayani Hai.

Chanzo: Mtanzania
Tags

Post a Comment

19 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mapadre sio wajinga kuikataa mahakama ya kadhi. sasa mnaona?

    ReplyDelete
  2. Siku hizi Tanzania kufundishwa mafunzo ya dini ya kiislam ni kinyume cha sheria? Hiyo sheria imeanza lini?

    ReplyDelete
  3. Huu ni ukuda si udaku tena, kwani tatizo la watoto kusoma uislamu shida ni nini au wao kucheza judo na karate ni kosa katika ibara gani na sheria ipi imevunjwa ? Mbona fikra za kishenzi mnazipa uzito usiostahili?

    ReplyDelete
  4. Ata uku ukonga mazzni wapo watoto wanasoma mazingira ayo ayo. Waandishi njoon mpaka mombasa. Ukifika mombasa chukua bodaboda Ata tax wambie wakupeleke mskiti wa makobe. Wameji funika akuna mtu kuingia ndani zaidi ya ayo watoto.

    ReplyDelete
  5. Mwandishi jaribu kuandika vitu na maelezo Kuna sheria gani ya Tanzania inayosimamia mafunzo ya dini ilituelewe wamefanya kosa gani

    ReplyDelete
  6. serikali inatakiwa kuwa macho kwani watu wanatumia vivuri vya dini kutanya mambo yao
    wawajibishe kisheria wanaoishi na watoto hao pamoja na wazazi wa watoto hao kulingana
    na sheria ya nchi,watanzani tuwa macho.Majeshi yote msilale

    ReplyDelete
  7. Wanafundishwa dini ya kiislam misikitini kinyume cha sheria, hivi mlitaka wakafundishwe dini ya kiislam wapi kama si misikitini? Pia wanafundishwa judo na karate, nalo kosa pia, ile dhana ya kutaka tujifundishe judo na karate kwa self defence haipo tena? Nadhani kuna jambo la siri mnalo juu ya mafunzo ya dini ya kiislam, kama si hivyo basi chunguzeni kwa undani sio kila madrasa imekuwa haramu nchi hii. Kumbukeni mahubiri yenu ya "serikali haina dini" yawe fair sio kubana upande mmoja tu.

    ReplyDelete
  8. Kama hiyo ni kinyume na sheria basi ili iwe kimbele na sheria itabidi wafundishiwe makanisani!

    ReplyDelete
  9. Hao watoto wanalelewa kuja kuwa ISIS na EL-SHABAB, Wa Tanzania tuwe makini sana

    ReplyDelete
  10. Nyie serikali kuweni makini sana waislam tukifanya mambo yetu kwenu nyie ni makosa mnatuingilia katika zone zetu but itawacost one day

    ReplyDelete
  11. Mazoezi ya nini sasa, mtaendelea kutuchinja lakini hamtakua na amani, kama wanataka mazoezi si jkt ipo, waende

    ReplyDelete
  12. Jamani kuna dini hazifikiri

    ReplyDelete
  13. Elimu itolewe jamani, dini huenezwa kwa sera, sio upanga, tuwaombee hao wrnxetu

    ReplyDelete
  14. Mi naona hawa wenzetu wameshapoteza mwelekeo maana harakati zote hizi ni kuhakikisha mkristo haishi kwa amani ktk hii dunia.tuliwakoseaga nini jamani ndugu zetu?

    ReplyDelete
  15. Nyie ni wapumbavu tu na mna chuki na uislam mbona kuna sehem kibao watu wanafundishwa karate na boxing hamjasema kitu iwe waislam ndio kosa.

    ReplyDelete
  16. Muandishi wa habari hii ya watoto na waliyo nyuma yake wanafuata falsafa ya "Ukitaka kumuua mbwa anza kwa kumpa jina baya....." kwani wanachofanya ni kuanza kutengeneza "negativity" juu ya uislam kwa ujumla wake!

    ReplyDelete
  17. Tatizo sio kufundisha dini, kama ni halali
    kwanini wanafundishiwa mafichoni?

    ReplyDelete
  18. Wanaandaliwa kuwa Alshabab na ISIS hao, kwa nini watoke mikoa mbalimbali? kwani hiyo mikao mingine haina madrasa? judo na karate vinahusiana vipi na mambo ya dini kama sio mnaandaa kizazi kiovu ambacho mnakijaza chuki alafu mnajiita watu wa dini! Hamna dini yoyote nyie mna shetani maana hayo mnayofundisha/fundishwa si mambo ya Mungu. Kumfundisha mtu chuki kwa watu wa dini nyingine, kumfundisha judo na karate hayo si mafundisho ya MUNGU, Mungu anapenda watu wote na pia hukumu ni juu yake hakuna mtu mwenye haki ya kumhukumu mwingine, kwa sababu hata hivyo wewe unayehukumu una dhambi kuliko hata unayemhukumu.

    ReplyDelete
  19. Wakafie mbele,, hawa sio waislam tunaowajua

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad