Waziri Steven Wasira Awafukuza Kazi Wakurugenzi Watendaji Watatu Kwa Kuisababishia Serekali Hasara ya Sh Billioni 2.5

WAZIRI wa kilimo, Chakula na Ushirika Steven Wasira amewafukuza kazi wakurugenzi watendaji watatu wa Mamlaka ya Kuendeleza Bonde la Mto Rufiji (Yaani Rufiji River Basin Development Authority – RUBADA) kutokana na matumizi mabaya ya ofisi ya Umma ambayo yameitia  hasara ya Bilioni 2.5 Serikali .

Akitoa agizo hilo leo mbele ya Waandishi wa Habari, Waziri Wasira amewataja Watendaji hao kuwa ni Bwana Aloyce L. Masanja – Kaimu Mkurugenzi Mkuu; Bibi Tabu Ndatulu – Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji; na Bwana Filozi John Mayayi – Mkurugenzi wa Fedha na Utawala.

Wassira amesema  baada ya Ofisi yake kupata malalamiko kutoka kwa wananchi wa  vijiji vya Rufiji pamoja na wawekezaji juu ya Urasimu wa shirika hilo, aliunda  timu ya Uchunguzi kutoka wizara ya Kilimo na Hazina kwenda kuchunguza malalamiko hayo.

“Baada ya kuunda tume  kutoka hapa Wizarani ikishirkiana   na Hazina, walienda  kwenye shirika hilo  kufanya  ukaguzi.Tume ilibaini kwamba mfumo wa pale ulikuwa ni mbovu, wakurugenzi  hawa  walijifanya  wahasibu, wakawa  wanakuanya  pesa  wenyewe  na  kutembea  nazo.Walifanya  maksudi tu ili kujiwekea mianya ya kuiba  Fedha” Amesema  Wassira

Taarifa ya Mheshimiwa Wasira imeanisha kuwa kati ya shilingi 2.748 billion zilizokuwa zimekusanywa kwa ajili uwekezaji, ni shlingi 714.606 milioni tu ndizo zimetumika kihalali wakati kiasi kilichobaki kimetumika bila kuzingatia sheria na kanununi za fedha za umma.

Waziri Wassira amesema kuwa mbali ya kuiba pesa hizo, kamati ilibaini kwamba watendaji hao wametumia zaidi ya Milioni 314 kwenye matumizi yaliyo  kinyume  cha  utaratibu
ikiwemo pesa zilizotengwa kwa ajili  maendelea ya miradi ya Shirika hilo ambazo  zimetumika  ndivyo  sivyo.

Vilevile Waziri Wassira amesema hata pesa ambazo wamewakata wafanyakazi kwa ajili ya kupelekwa kwenye mifuko ya Hifadhi ya Jamii zimekuwa zikiliwa na watendaji , tena kwa makusudi pasipo kupelekwa huko.

Aidha,Waziri Wasira amesema baada ya kupata Ripoti ya Tume hiyo ameiagiza Bodi ya shirika la Ludaba kuwafukuza kazi mara moja watendaji hao watatu na nafasi zako kujazwa mara moja huku  taratibu na sheria za kuwafikisha mahakamani zikifanyika.

Toa Maoni yako Hapa Chini
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Duh hongera MH.Wasira, huyo Masanja kaulize bonde la Kilombero ndo wanamjua vizuri Masanja.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad