Alikiba asema vurugu zilizotokea Afrika Kusini zimesababisha video ya ‘Chekecha’ ichelewe, awaomba msamaha mashabiki

Staa wa muziki Alikiba amesema kuwa video shooting ya wimbo wake ‘Chekecha’ ambayo imepangwa kufanyika Afrika Kusini, imechelewa kutokana na vurugu dhidi ya raia wa kigeni (Xenophobia) zilizoibuka hivi karibuni nchini humo.

Tayari tulikuwa tumeplan kila kitu unajua kunakuwa kuna zile dancing, choreographer wangu alikuwa ameshacreate kila kitu amewatumia dancers wa South Africa, lakini kilichotufelisha ni hii Xenophobia iliyokuwa imetokea,” alisema Alikiba kupitia Ubaoni ya E-Fm. “Vile vile unajua vifaa kule wanakuwa wanaazima kwahiyo imekuwa ni sheria ambayo imepitishwa hairuhusiwi kufanya hivyo mpaka patulie.”

Hata hivyo Alikiba amesema mipango yote inaenda vizuri na siku si nyingi atasafiri kuelekea Afrika Kusini kwaajili ya kulipa deni la video alilonalo kwa mashabiki wake.

Kwahiyo tumefanya tena opportunity nyingine tumepata tayari namshukuru Mungu tumeshapanga kila kitu.

Kwa kuonesha kuwa anawajali na kuwaheshimu mashabiki, King Kiba hakusita kuwaomba msamaha kwa kuchelewa kufanya video ya ‘Chekecha’, wimbo ambao una karibia kufikisha miezi mitatu toka ulipoachiwa mwishoni mwa February.

Mimi nataka kuchukua nafasi hii kukuomba samahani, mafans wangu wote na wapenzi wa muziki, najitahidi sana lakini sisi tunapanga yetu na Mungu anapanga yake.”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad