Anayolalamikia Reginald Mengi Kama ni Kweli, Tunaelekea Kwenye Udikteta Usiomithilika

Serikali inaweza kuingia katika mgogoro usio wa lazima na vyombo vya habari wakati huu nchi inapokaribia kufanya uchaguzi Mkuu, iwapo miswada ya Huduma ya Vyombo vya habari na wa Sheria ya Haki ya kupata Habari itapitishwa bila kufanyiwa marekebisho.

Mwenyekiti wa Wamiliki wa vyombo vya Habari nchini – MOAT Dr Reginald Mengi ametoa tahadhari hiyo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano wa Mashauriano ya Amani na Utulivu nchini, na kusisitiza kuwa kupitishwa kwa miswada hiyo kutasababisha ukiukwaji mkubwa wa Uhuru wa Habari, uvunjifu wa amani, na ni kifo kwa vyombo vya habari binafsi nchini.

Akitolea mfano, Dr Mengi ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP amesema kifungu nambari 14 cha muswada wa sheria ya Huduma za Vyombo vya habari kinatoa amri kwa vituo binafsi vya Utangazaji kujiunga na chombo cha habari cha umma kwa ajili ya Taarifa ya habari ya kila siku saa mbili usiku, kinyume na ilivyo sasa, na ni dalili za kurudi tulikotoka.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. YAANI HUYU BABA, BORA AMALIZE MUDA WAKE NI HATARI TU, SASA ATAKA IANZISHA KWA KUWA MUDA WAKE UNAISHA, YOOTE NA KATOTO KAKE KANASUMBUA, ILI ATA AKITOKA BABA MAMBO YAWE MSWANO KWA WIZI , UFISADI, HIII NCHI KUENDELEA NI KAZI, YAANI NI SHIDAAA

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad