Barua Nzito Wema Kuna Kitu cha Kujifunza kwa‭ ‬Zari‭!

KWAKO mtoto mzuri, Beutiful Onyinye, Wema Sepetu !'Madam'. Vipi uko poa? Ukitaka kujua afya yangu, mimi ni mzima namshukuru Mungu, hofu na mashaka ni kwako wewe uliye mbali na upeo wa maisha yangu.

Kitambo kidogo hatujaonana, nimeona si mbaya kama nitakukumbuka kwa barua maana najua kutokana na majukumu yako na yangu kuwa mengi, wakati mwingine tunaweza tukafikisha hata miezi sita hatujaonana.

Dhumuni la barua hii ni kutaka kukushauri kwamba unaweza kujifunza kitu kutoka kwa mpenzi wa sasa wa aliyekuwa mpenzi wako, Nasibu Abdul !'Diamond, Zarinah Hassan !'Zari!

Naomba usinielewe vibaya. Sina nia ya kukupambanisha wala kutaka kukukejeli kwa namna yoyote. Kuna kitu kidogo tu cha kujifunza kutoka kwa binti huyo wa Kiganda.
Achana na maneno yanayosemwa mtaani, kila mmoja ana upungufu wake lakini binadamu tunashauriwa kuiga yale mazuri kutoka kwa wenzetu.

Iko hivi Wema, wewe na yeye mna nafasi moja nzuri katika jamii. Nyinyi ni maarufu. Mnapendwa na watu kupita maelezo. Mna ushawishi mkubwa sana katika jamii hivyo mnaweza kufanya jambo na likapata mafanikio makubwa sana.

Umaarufu wenu ni biashara. Kwa nini uendelee kubaki chini wakati umezungukwa na fursa kibao? Umaarufu wako ni biashara kama utaamua kuwa !٪serious!& na kila hatua unayoipiga.
Nikwambie ukweli bila unafiki, unapaswa kuiga jambo moja tu la msingi kutoka kwa Zari, kuwekeza na kuheshimu fedha.

Mwenzako anaijua fedha. Anajua namna ya kuitafuta na namna ya kuiwekeza katika maeneo ambayo yatazidi kuzizalisha. Akili yake inawaza pesa na si starehe zisizokuwa na msingi.
Mfano mdogo tu ni !٪idea!& kama ya All White Party aliyofanya Zari kule Uganda. Alifanikiwa, anaendelea kufanya na wiki iliyopita aliifanya pale Mlimani City jijini Dar na kupata mafanikio makubwa.

Kwangu mimi kile ni kitu kikubwa sana ambacho kinaingiza fedha nyingi kwa wakati mmoja. Si vibaya kama utaiga vitu vya namna hiyo. Nisikufiche, nafasi ya umaarufu uliyonayo Kibongobongo, unaweza kufanya zaidi ya shoo ile kama utaamua na kupata watu wazuri wa kufanya nao kazi.

Na unapofanya mambo makubwa kama hayo, lazima pia udhibiti matumizi yako. Starehe zipo lakini wakati mwingine unapaswa kuheshimu fedha. Yale mambo ya kwenda kuzimwaga ukumbini eti kuwa kama kina pedeshee !٪nanilii!&, si mazuri.

Jeuri ya fedha ifanye kwa kufungua miradi mikubwa ambayo hata utakapozeeka utainjoi matunda yake. Kuigiza kuna mwisho, huwezi kuwa mwigizaji milele, kuna wakati utatakiwa kuwa msimamizi wa miradi yako tu binafsi na mkono uende kinywani kiulani tu.

Usikubali kushikiwa akili na wapambe, unayoshauriwa na wapambe yachuje maana si yote yanakuwa na manufaa. Tumia kipaji na jina lako vizuri, una nyota ya kupendwa basi kupendwa huko kuwe na faida.
Natambua una idea zako ambazo tayari umeanzisha kama kipindi chako cha In My Shoes, usiishie hapo fanya makubwa zaidi.
Kwa leo acha niishie hapo. Ni matumaini umenielewa.
Wasalaam

BY: Eric Evarist/ GPL

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ukweli ni kwamba Wema kama Wema inabidi kwanza aweke zile biashara zisizo na mpango kama za Team Wema, hazina mpango wowote kwani ndo zinazomuangusha na kuonekana hana mpango wowote wala maharifa. kwenye hili kundi Team Wema wengi wao sio wabunifu bali na hawana zile akili kabisa, yaani ni waswahili,matusi yamewajaa mdomoni... Bila hivyo wema atabaki kuparamia watu wenye pesa ili wamtoe

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha ubwege wewe, deal na maisha yako, achana na mambo ya huyo Kicheche na wapumbuvu wenzake. Jiulize je ungekuwa ni wewe uko katika the same situation kama ya kwake angeweza kukushauri kama unavyojifanya kumshauri sasa????? Watanzania mko so funny kufuatilia maisha ya watu wengine wakati ya kwenu wenyewe yanawashinda.

      Delete
  2. Nakubaliana na wewe 100%

    ReplyDelete
  3. Ungeweza kumshaur yy kama yy sio lazma kumcompare na zari, wema nae ana mambo yako pil una uhakika na hizo mali za zari kam ni jasho lake au alifunguliwa na mzaz mwenzake? Nachokiona kwa wema ambacho sipend ni kugawa hela sehem za starehe bas

    ReplyDelete
  4. Wewe unavyomshauri hivyo je ingekuwa ni wewe angekushauri kwa namna unavyomshauri???????? Acha ubwege wewe nenda kashike jembe ulime. Endelea na maisha yako. Maisha yake hayakuhusu.

    ReplyDelete
  5. wewe mtoa ushauri. umeshawai kuuliza wema akakwambia hana investment.? na sio lazima awe kama zari, kila mtu atakua vile anavyotaka awe mwenyewe. cze wote hatujui anawaza nini juu ya future yake. so stop concluding!

    ReplyDelete
  6. Wewe Domo acha kujifanya unajua kushauri mshauri mzee wako ulie nae acha ale pesa zako baadae ndo utapata akili sasa hivi ubongo wako una vumbi ningekuona wa maana kama unge mshauri kipindi uko nae naushauri sio lazima uweke kwa magazeti iliuonekane kwa watu ungekua na nia nzuri ungefanya private acha kujionyesha kwa watu kwani umedhani hakuna watu wakumshauri wema wapo wenye akili watamwita faragha wamshauri sio wewe unae tafuta sifa kwa watu na bibi kizee wako Hebu Muache wema wangu haumlishin wala kumvisha part part ndo mavi mamavikwenda zako huooooooooo na kizeee chako mshauri bibib yako huyo ulie nae

    ReplyDelete
  7. Mmmmmh!!! Umekuwa ugomvi tena ila endeleeni tu mi napita naenda shamba kulima.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad