Kufuatia uvumi kuwa Edward Lowassa waziri mkuu aliyeng'oka kwa kashfa za ufisadi kutaka kuhamia UKAWA, Dr. Willbrod Slaa katibu mkuu wa CHADEMA amesema kuwa hayupo tayari kula sahani moja na mafisadi.
Akijibu tuhuma hizo Dr. Slaa amesema wazi kuwa Chadema na UKAWA hawapo tayari kupokea mafisadi kwani itakuwa ni kinyume kabisa na dhamira ya UKAWA ya kuwatumikia watanzania wanaotegemea mabadiliko makubwa.
"Watanzania wapo tayari kwa mabadiliko na wameonyesha nia ya dhati kutuunga mkono, hatupo tayari kuchafuka na mafisadi" amesema Dr. Slaa
Kutokana na hali halisi ilivyo mdani ya CCM, chama hicho kinatarajiwa kukumbwa na mgogoro mkubwa kutokana na msuguano mkali wa makundi mawili makubwa yanayowania urais huku kundi hasimu na Lowassa likiungwa mkono na rais Kikwete.
Lowassa tayari ametoa hotuba huku akiainisha vipaumbele vyake ambavyo vinaenda kinyume kabisa na ilani ya CCM mwaka 2015-2020 jambo linalohashiria kuwa ndani ya chama hicho hali si shwari.
Mawazo yako tuu!
ReplyDeleteNa wewe unajiita Dr.ulivyokuwa ukishupalia uongezewe mshahara (au wenyewe mnasema hela za mboga) na kusahau kuwa kuna watanzania wenzako ambao hawana hata uwezo wa kupata mlo mmoja kwa siku Je?ukipewa huo urais au hata uwaziri naona itakuwa kasheshe siyo ufisadi bali itakuwa ufisudi mr.Dr
ReplyDeletewatanzania kukosa hata mlo mmoja kwa siku ni ubovu wa serikali ya sasa wala hata dr.slaa anaathirika na hali hii, siyo eti mtu kudai aongezewe mshahara ndo mbovu kumbe mnataka achote pesa kama wale wajanja wa chama cha mapesa
ReplyDelete