Kauli nisiyopenda Kuisikia "Wenye akili wako Chuo cha UDSM, Huko Kwingine Utachelewa Sana Kuajiriwa Ukimaliza Chuo"

Nikiwa mwaka wa kwanza Chuo Kikuu Cha Tumaini- Iringa(sasa wanakiita University Of Iringa); nilikutana na "brother" mmoja aliyekuwa ndio kwanza ametua nchini baada ya kumaliza digrii yake katika chuo kikuu cha Makerere cha nchini Uganda. Akaniambia kauli ya ajabu sana, akasema, "Kwa nini umeenda kusoma chuo hicho?(akimaanisha Tumaini). Wenye akili wako UDSM, huko Tumaini umeingia choo cha kike, utachelewa sana kuajiriwa". Nikamwangalia weeee, (nikamuhurumia na kumdharau ndani kwa ndani) halafu nikamjibu; "Brother, wenye akili ni wale wenye hela za maana; wanaweza kuwa wamesoma huko UDSM ama chuo chochote na wanaweza kuwa hawakusoma kabisa!. Kujidhania una akili za kufaulia mitihani halafu usiwe na hela za maana(au atleast za kutosha) huo ni ujuha." Akiwa bado anashangaa-shangaa nilichomwambia, nikamuongezea;

"Kwanza wanaohangaika na CV za mavyuo ni wale wanaotaka kuwavutia wenye akili(waajiri) ili wawaelekeze cha kufanya(yaani wawaajiri). Mtu mwenye maono ya kujiajiri hahangaiki na CV za mavyuo bali anaangalia maarifa ya kumsaidia na kimsingi anaweza hata asiende shule bali akayapata maarifa hata mtaani tu". Akaniuliza, "Unamaanisha nini?" Nikamwambia, "Umesoma chuo Kikubwa lakini bado una akili za kikoloni zinazowaza kuwa hakuna maisha ya maana mpaka uajiriwe. Kusoma ni jambo zuri na kuajiriwa sio jambo baya lakini usikariri kuwa hakuna maisha pasipo kuajiriwa; na usifikiri kila anaefika chuo kikuu anawaza kuajiriwa tu. Siku hizi mafanikio kimaisha hayamo katika CV ya chuo ulichosoma na kamwe hutatajirika (au atleast kuwa na pesa za maana) kwa kutegemea mshahara pekee". Ikiwa imepita miaka sita sasa, sijajua hali ya kiuchumi na kimaisha ya yule brother; lakini ikiwa hajabadilisha ile "mentality" nina uhakika atakuwa "ni mbangaizaji tu" kiuchumi na kimaisha kwa ujumla licha ya kuwa anamiliki cheti cha digrii kutoka Makerere!

By Albert Nyaluke Sanga
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. well said... iko wazi wengi tuko nao mitaani wakisubiri siku rais atakapowapigia simu kuwa kuna kazi sehemu fulani.. ndio kuajiliwan ni vema, ila kujiajili ni vema zaidi, kama utaweza kufanya hivyo.

    ReplyDelete
  2. bonge moja ya point..nitafute nikutoe lunch hahaha tubadilishane maidea...
    ukwel ni kwamba %95 ya wanavyuo wengi wanawaza kumaliza then waanze kuzunguka na maCV..ndorobooooo kabisaa..ndo maana utasikia nafasi za kazi post 40 0r 20, alafu utakuta waliotuma CV ni zaidi ya 2000...ndoroboo kabisa...
    Tufikirie nje ya box..na tuache mawazo ya kimo cha zakayo..
    THE HIGHER THE RISK THE HIGHER THE RETURN

    ReplyDelete
  3. semeni sana lakini ukweli unabaki UDSM ndiyo chuo bora Tanzania.Badala ya kulalama kuwa wana UDSM wanaringa lazima mfanye juhudi kubwa tena ya makusudi ili kuhakikisha kuwa mnapata pass marks za kuwawezesha kujiunga na Udsm! labda nikuulize hivi uoni fahari kumaliza Udsm alafu ukajiajiri? Yaani umemaliza chuo kinachotambulika alafu unafanya mambo yako binafsi! Kwa vyovyote vile mwanafunzi aliyemaliza Udsm alafu akaamua kujiajiri atakuwa bora kuliko wewe uliyemaliza Tumaini ukajiajiri! haya ni mawazo yangu tu, mnisamehe kama nimewakwaza!!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad