Kiwango Stars Stars Chakera Watanzania..Wadau Wataka Kocha Afukuzwe..Sasa Wamkumbuka Maximo

Taifa Stars Imefungwa Michezo yote mitatu kwenye michuano ya Mataifa ya Kusini mwa Afrika (Cosafa) ,Matokeo hayo yamewaumiza Watanzania wengi nchini, ambapo mara baada ya kumalizika mechi hiyo kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, watu wengi wamelaumu kiwango kibovu kilichoonyeshwa na Stars.

“Siku zote kila mtu anavuna alichopanda, Taifa Stars wamevuna walichopanda, timu inachaguliwa kwa upendeleo, wachezaji waliofanya vizuri na wenye uwezo hawachaguliwi ukiuliza au ukiongea wanasema kocha anajua tumwachie, hebu tujiulize huyu kocha ana uchungu kweli na kipigo anachopata kuliko sisi Watanzania?” alihoji Charles Mayilla kupitia mtandao wa facebook.

Kipigo hicho kinakuja wiki chache mara baada ya wapenzi wengi wa soka nchini kulalamikia uteuzi wa kikosi wa Kocha Mkuu, Mart Nooij, ambaye ameendelea kuwaita baadhi ya wachezaji wanaokaa benchi kwenye timu zao huku akiwaacha wale waliofanya vizuri.

Baadhi ya wachezaji aliosafiri nao na wamekuwa wakiwekwa benchi kwenye mechi nyingi za timu zao msimu uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) ni kipa Deogratius Munishi ‘Dida’ (Yanga), Mwadini Ally (Azam), Hassan Dilunga (Yanga) na John Booco (Azam), aliyesumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara.

Makocha wanena

Akizungumza na MTANZANIA kocha mkongwe visiwani Zanzibar, Hemed Morocco, anayeinoa timu ya taifa ya huko ‘Zanzibar Heroes’, alisema hakuna njia ya mkato ya mafanikio kwa Stars, amedai lazima iachane na wachezaji wazee na kutengeneza kikosi bora cha vijana.

“Kila siku matokeo yetu yamekuwa ni kufungwa, mimi naona bado tunakurupuka, tunakumbatia timu ile ile ya wazee, Tanzania ina wachezaji wengi vijana waliobarikiwa vipaji, tukitaka kufika mbali tutengeneze kikosi bora cha vijana wenye umri wa miaka 17 ambacho baada ya miaka minne kitatupa mafanikio,” alisema.

Naye kocha mzoefu nchini, Kennedy Mwaisabula, alisema matokeo ya Stars dhidi ya Swaziland yametokana na kupwaya eneo la ushambuliaji waliopoteza nafasi kadhaa za wazi, huku akipata shaka kwenye safari ya timu hiyo kufuzu Mataifa ya Afrika (AFCON) 2017 na Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN).

“Uteuzi wa kikosi ndio unaiangusha timu, si vibaya kocha kuita kikosi chenye sura zile zile, lakini lazima tuangalie ya kuwa kikosi anachoendelea kukiita kina mafanikio, kama hakina mafanikio kocha lazima abadili kikosi na kujaribu wachezaji wengine, tunaona hapo amewaacha wachezaji bora kwenye ligi kama mshambuliaji Mandawa (Rashid), Malimi Busungu yule wa Mgambo, full back Kessy (Hassan),” alisema.

Alisema ipo haja kwa kocha wa Stars, Nooij kupata usaidizi mzuri wa ushauri kwa makocha wazawa ambao wanawajua vizuri wachezaji wa hapa, huku pia akieleza lazima Mholanzi huyo awe na mahusiano mazuri na makocha wa timu za Ligi Kuu.

“Kuna makocha wakongwe kabisa nchini kama mzee Kibadeni (Abdallah) na Mshindo Msolla, lazima watumiwe kwenye ushauri kwani wameipatia nchi mafanikio, kingine kocha inaonekana hana mahusiano mazuri na makocha wa ligi, kwani hata uteuzi wake amekuwa akiita wachezaji wagonjwa, hivyo lazima aimarishe mahusiano kwani wachezaji wanatoka kwenye klabu,” alisema.

Taifa Stars enzi za Maximo ilikuwa Team ya Kuogopwa sana yaaani mpaka sasa wadai tunataka kocha afukuzwe tu hata wapewe watanzania labda mambo yatabadilika...

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad