Kocha Hans Van Der Pluijm Aacha Ripoti yenye Siri Nzito Yanga Kuhusu Usajili

UKISIKIA fagio la chuma ndilo hili ambalo limepitishwa katika kikosi cha Yanga na kocha mkuu wake, Hans Van Der Pluijm ambaye ameacha ripoti yenye siri nzito.
Kocha huyo Mholanzi ambaye anatarajia kuondoka nchini keshokutwa kuelekea Ghana kuungana na familia yake kwa ajili ya mapumziko, amesema kwamba amekamilisha kila kitu ikiwa ni pamoja na orodha ya wachezaji ambao hawahitaji kwenye kikosi chake msimu ujao.
“Nimetoa ripoti yangu lakini siwezi kukwambia nini nimesema kwa kuwa sina ruhusa ya kufanya hivyo hadi uongozi utakapoipitia na kisha tukashauriana,” alisema kocha huyo.
Hata hivyo, habari kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema kuwa moja ya mapendezo ya kocha huyo ni kubakisha wachezaji wawili tu wa kimataifa kati ya waliopo na kufanya usajili mpya wa wachezaji wa kimataifa.
Tayari wachezaji Haruna Niyonzima, Mbuyu Twite mikataba yao lakini taarifa mbalimbali zinadai kuwa Niyonzima tayari amesaini mkataba mpya huku Twite naye akiwa katika hatua za mwisho
Pia Mliberia, Kpah Sherman yeye anatarajia kuondoka kwenda nchini Uswisi hivyo kubaki Amiss Tambwe na Coutinho ambao bado wana mikataba na timu hiyo.
Aidha, chanzo chetu kutoka Yanga kimeeleza kuwa kwa wachezaji wa ndani panga la Pluijm limewakuta wanane (8) huku wengine watatu akishauri watolewe kwa mkopo kutokana na kuwa bado wana mikataba.
Chanzo:Bingwa
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kweli yanga safari hii ilijengeka kuanzia viongozi mpaka wachezaji,walikuwa na umoja,nidhamu na kuelewana kwa hali ya juu.Wajitahidi kutengeneza kikosi kingine chenye kuelewana,kubwa ni kutooneana aibu kukemea maovu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad