Pamoja na mvua hizi kulaumiwa na kulaaniwa kila kona kwa kuleta madhara pamoja na kupoteza maisha ya watu, mvua hizi sio balaa kwa kila mtu bali kwa wengine ni neema na simestahili pongezi!.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Said Meck Sadick, amezipongeza mvua zinazoendelea kunyesha katika jiji la dar es salaam, kwa mvua hizo kuisaidia serikali katika utekelezaji wa hukumu ya mahakama kuu, kuwaamuru wakazi wa mabondeni kuhama kwa lazima, ambapo waligoma kata kata kuhama, na serikali ilimkuwa bado inajishauri namna ya kuwahamisha watu kwa nguvu bila kuleta madhara, haswa kwa kuzingatia huu ni mwaka wa uchaguzi!, mvua hizi zinazoendelea kunyesha zimeisaidia serikali kuwahamisha wananchi hao, hivyo Meck Sadik amezishukuru sana!.
Mkuu huyo wa Mkoa, ametoa shukrani hizo, katika mahojiano ya moja kwa moja katika kipindi cha Kumepambazika, kinachorushwa na Redio One Stereo asubuhi hii.
Amesema ametokea taarifa za kupoteza maisha kwa watu wengine wawili, mmoja amesombwa alipotaka kuvuka mto Ng'ombe maji yakamzidi nguvu na kumsomba, na mwingine ni mtoto mdogo wa miaka miwili, alikuwa akicheza nje ya nyumba yao mafuriko yakapita mbele ya nyumba na kumsomba!.
Kuhusu wakazi wa mabondeni, Mkuu wa Mkoa alisema baada ya mafuriko ya 2011, waliwahamisha na kuwapatia viwanja Mbweni, baadhi yao walihama na wengine waligoma na kwenda mahakamani ambapo serikali ilizuiliwa kuwahamisha kwa nguvu.
Hoja za wakazi hao kupingwa kuhamishwa ni kwa sababu wametumia gharama kubwa kwa ujenzi na kuwekewa huduma muhimu za maji na umeme, hivyo hawawezi kuhama bila kufidiwa!. Lakini sasa mahakama imeishatoa uamuzi lazima wahame, na serikali ilijipanga kutumia nguvu kuwahamisha, tena this time bila kuwapatia maeneo mbadala, lakini kabla ya utekelezaji wa zoezi hilo, Mungu akaleta mvua saidizi ambazo zimekuwa msaada mkubwa kwa kuwahamisha, hivyo kuipunguzia serikali kazi ya kuwahamisha kwa nguvu.
Mkuu wa Mkoa amesema baada ya usaidizi huu wa mvua kwenye kuwahamisha watu hao, sasa serikali imebakiwa na kazi ndogo tuu, kuhakikisha watu hao hawarudi katika maeneo hayo, na kuwasisitiza wale wote walohama na kubakiza baadhi ya vifaa vyao, mvua zikisimama wataruhusiwa kivichukua kabla ya kupitisha tingatinga na kulisawazisha eneo lote kubaki tambarare kama walivyofanya kwa eneo la Kipawa!.
Pia Meck Sadiki aliviomba vyombo vya habari kutoa ushirikiano katika zoezi hili kuhakikisha wakazi wa mabondeni wanahama kwa ridhaa yao kutekeleza amri ya mahakama na wale wote watakao kaidi, watahamishwa kwa nguvu.
Pasco.
Meck Sadick aipongeza Mvua na Kuishukuru Kwa Kuwahamisha Wakazi wa Mabondeni!
0
May 11, 2015
Tags