Mkuu wa jeshi la Burundi amedai kuwa rais Pierre Nkurunziza amepinduliwa kufuatia kuwepo kwa fujo zilizotokana na mpango wake wa kugombea muhula wa tatu.
Meja Jenerali Godefroid Niyombareh amesema kamati ya uokozi imetengenezwa japo kiwango chake cha kuungwa mkono hakijulikani, BBC imeripoti.
Maelfu ya watu waliokuwa wakiandamana kwenye mji mkuu wa Burundi, Bujumbura wameripotiwa kuwa wanasherehekea kwa sasa.
Rais Nkurunziza kwa sasa yupo hapa nchini Tanzania.
Akaunti ya Twitter ya ikulu imesema mapinduzi hayo ya kijeshi yameshindwa.
Nkurunziza amekuwa akikutana na viongozi wengine wa Afrika Mashariki kujadili mgogoro huo. Msaidizi wake amekanusha kufanyika kwa mapinduzi hayo
Mkuu wa jeshi wa Burundi atangaza kumpindua rais Pierre Nkurunziza
1
May 13, 2015
Tags
HEEE HAWA VIONGOZI WA AFRICA WANA MATATIZO GANI? NA HAYA MADARAKA YA URAISI, HAWANA LOLOTE, WAMEPAONA NDIO SEHEMU YA STAREHE YA MAISHA CHEO CHA URISI, KWA KUWA KUIBA KWA SANA NA KUHUSUDIWA, WATU HAWAMTAKAI SI ATMKE MPAKA WAJE WAUWAWE BURE
ReplyDelete