Mwigulu Nchemba apewa ‘Upako’ wa Urais

Askofu Mkuu wa Kanisa la General Mission Center Limited (GMCL) la jijini hapa, Nabii David Mpanji juzi alimkabidhi mafuta ya upako, Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba kwa ajili ya kung’arisha nyota yake katika harakati zake za kuwania urais.

Nabii Mpanji alisema mafuta hayo yanaashiria ufalme na utawala na kusisitiza kwamba kitendo hicho ni kudhihirisha kuwa Nchemba, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha, anafaa kuliongoza Taifa.

Tukio hilo lilifanyika kwenye ibada maalumu iliyoambatana na harambee ya kuchangia vifaa vya redio ya kanisa hilo iliyoendeshwa na Nchemba na Sh53 milioni zilipatikana.

Alimtaka Nchemba kutamka nia yake ya kugombea urais mbele za watu, huku akisisitiza kuwa Taifa linahitaji mtu anayeweza kusimamia wananchi wenye kipato cha chini na kumtaja mbunge huyo wa Iramba Magharibi kuwa amethubutu kufanya hivyo.

“Mimi nasema wazee wasikuumize kichwa, hata Biblia inasema fahari ya wazee ni mvi zao lakini fahari ya vijana ni nguvu zao. Tunahitaji Watanzania wazalendo na jasiri ambao wanaweza kusema bila kuogopa kama wewe (Nchemba),” alisema.

Akizungumza katika ibada hiyo, Nchemba aliwashukuru Watanzania wenye imani naye na kubainisha kuwa muda ukifika atasema nia yake.

“Imebaki kitambo kidogo nitasema kwani mimi ni kiongozi wa chama, hivyo natakiwa kufuata taratibu na kanuni cha chama, nawaomba mvute subira kidogo nitasema tu,” alisema.

Nchemba alisema upako huo ni dalili tosha za Watanzania kutambua mchango wake katika kuwatumikia na yeye hatawaangusha... “Tutavuka mto tukifika mtoni.”

Mwigulu ambaye aliongozana na waimbaji maarufu wa nyimbo za Injili akiwamo Boniface Mwaitege na Moses Makondeko, alisema katika suala hilo (la urais) anamtegemea sana Mungu.

Aliwataka wananchi kuwa na uchungu na nchi yao kwa kutanguliza uzalendo kwani ni vigumu kupata kiongozi mzalendo katika Watanzania wasio kuwa na uzalendo.

Akisoma risala mchungaji wa kanisa hilo, Aquina Mhanze alisema mahitaji ya kanisa hilo ni Sh200 milioni kwa ajili ya kukamilisha vifaa vya redio na ofisi na kwamba kwa sasa kuna Sh15 milioni.

Alisema kuwa kati ya fedha hizo, Sh150 milioni ni kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya redio na Sh50 milioni kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya redio.

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. KUSEMA UKWELI HUYU JAMAA ANATUFAA MAANA HAOGOPI MWIGURU ANAFAA KUFUTA UFISADI ATASIMAMIA KILA KONA YEYE MWENYEWE SABABU ANAJUA JINSI YA KUBADILISHA MFUMO ULIOPO SASA WA MAKUSANYO YA KODI NA WALE WASIOLIPA, NA WALE WA MICHONGO KUSAMEHEWA KODI, MATUMIZI YA MADALAKA KWA WANANCHI NA SEKTA BINAFSI, KUSHUKA KWA SHILINGI YA TZ, KILIMO, MFUMUKO WA BEI, KUSIMAMIA KIKAMILIFU MFUMO WA WAWEKEZAJI, ELIMU, MAZINGIRA, MIUNDO MBINU, NA ASKARI

    ReplyDelete
  2. Hii ni aina nyingine ya ushirikina! Mungu ameshaandaa mtu! sisi tunatakiwa tumshukuru tu kwa huyo aliyetupangia! kinyume chake ni ushirikina!

    ReplyDelete
  3. Wajinga ndiyo waliwao jus'imagine urself misa1mazishi wametapeliwa kiaina million 53 tsh duh!!ķweli bilblia ilisema wataibuka manabii wengi wa uongo na hivi ndivyo ilivyo sasa kila kona kuna kanisa fake ĺa kujinufaisha kibinafsi kwa kutumia neno MUNGU utendaji ukweli ufanisi akili(kielimu)nia na moyo wako ndiyo utakufanya wewe ufanikishe lengo/malengo yako na siyo eti vinginevyo huyo mwingine alijidai kuisimamisha mvua mbona haijasimama na inaendelea kunyesha tu mtindo mmoja sasa tumchukulie vipi?

    ReplyDelete
  4. INAELEKEA HILI SWALA LA URAISI WENGI LINAWANYIMA USINGIZI, KHA SIO BURE YOTE HIYO SI ZANI KAMA WANA MAWAZO MAZURI NA HII NCHI, ZAIDI YA UFISADI NA WIZI NA RUSHWA NA MIKATABA YA UONGO ILI WAJILIMBIKIZIE NA BILA KUSAHAU HELA ZA WALIPA KODI NAZO NDANI, MAANAKE KILA KUKICHA MTU NA LAKE, SI MCHEZO KILA MTU ATAKA KUISHI MAISHA YA JUU,

    ReplyDelete
  5. IQ za wabongo ni shiiiidam, hata JK walisema nii Mungu katuchagulia...............

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad