Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe amefunguka na kusema kuwa alipofukuzwa wanachama katika chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) alitamani kujiunga na Chama Cha NCCR-Mageuzi kwani ndicho chama ambacho kilikuwa kinaendana na itikadi yake anayoifuata na kuiamini ambayo ni itikadi ya Ujamaa. Zitto Kabwe amefunguka haya leo alipokuwa akichat Live kupitia ukurasa wa facebook wa EATV katika kipengele cha KIKAANGONI ambacho kimeanza upya katika msimu wa pili na kitakuwa kikifanyika kila Jumatano kuanzia saa nane mchana mpaka kumi Alasiri.
Zitto Kabwe alisema kuwa alishindwa kujiunga na Chama hicho cha NCCR-Mageuzi kutokana na kuwepo kwa matatizo hivyo aliona siyo vyema kujiunga nacho, ndiyo maana alifikiri kuwa na chama cha siasa ambacho kitakuwa na misingi na itikadi ambayo yeye anaiamini na kuisimamia.
Nilipofukuzwa CHADEMA nilitamani kujiunga na Chama cha NCCR Mageuzi
1
May 06, 2015
Tags
Makubwa haya, ACT sialiianzisha yeye? au alipoona NCCR wako UKAWA akaacha, haeleweki nae huyu
ReplyDelete