Rais Kikwete Amesaini Rasmi Sheria Yenye Utata ya Makosa Mitandaoni, Kuanzia Sasa Itaanza Kutumika..

Rais Jakaya Kikwete tayari ameshasaini sheria yenye utata ya makosa ya mtandao na muda wowote kuanzia sasa itaanza kutumika rasmi

Hivi ni baadhi ya vipengele vilivyozua utata katika sheria hiyo

1. Kifungu 7 (2b): Mpokeaji wa ujumbe (receiver) anaweza kushtakiwa kwa kosa la kupokea ujumbe ambao sheria imeufanya kuwa wa jinai. (Mfano: Mtu akikuforwadia ujumbe, ukiupokea na wewe umefanya kosa la jinai).

2. Kifungu 8: Itakuwa ni kosa la jinai kama mtu ataweka wazi nyaraka za siri za serikali hata kama ni nyaraka ya kusaidia nchi kwa ujumla (Mfano: Matumizi mabaya ya mali ya umma).

3. Kifungu 14: Picha yoyote yenye mwelekeo unaoweza kuonekana kama ‘mchafu kingono’ inaweza kupelekea mtu kufungwa hadi miaka 10 au kulipa milioni 30; Sasa kama mtu kaposti picha yake ambayo sio ya ponografia lakini ‘ikatafsiriwa’ hivyo. Sheria haijatafsiri ponografia!

4. Kifungu 23: Je, ulijua kuwa ‘kusababisha maudhi ya hisia’ kwa mtu mwingine ni unyanyasaji na unaweza kufungwa kifungo kisichopungua mwaka mmoja?

5. Rejea adhabu ya ibara mbalimbali: Sheria hii kila kosa linaweza fanya mtu afungwe kifungo hadi cha maisha na kulipa pesa hadi zisizohesabika kwani hakijawekwa kikomo cha juu cha adhabu bali kikomo cha chini tu kwa Kiingereza “not less than”

6. Sheria haijaeleza vizuri suala la kutumia jina lisilo lako kwenye mtandao na hivyo mtu anaweza kushitakiwa kama kuna mtu mwingine mwenye jina kama hilo katika maisha halisi.

7. Serikali kupitia waziri husika ndio ina mamlaka ya kusema jambo lililowekwa kwenye mtandao ni la kweli, uongo au la kupotosha. Kumbuka hata ESCROW, EPA walisema ni uwongo; ni wangapi katika mtandao wangeshtakiwa kiuonevu kwa hili?

8. Kifungu 22: Ukiweka ujumbe katika mtandao na ukaufuta au kuuboresha, kama ukishtakiwa kwa kuweka ujumbe huo unaweza kuhukumiwa pia kwa adhabu ya kuuboresha au kuufuta. Ni mara ngapi unafuta ‘status’ zako za WhatsApp? Unaweza shtakiwa kwa kuchelewesha ushahidi kisa tu ulifuta na hamna mtu anayeweza kujua ulifuta kwa kusudi au la.

9. Mkuu wa kituo cha Polisi chochote kile nchini anaweza kuagiza wewe umpatie simu/laptop yako au taarifa zako zote (kwenye email, chats) au hata vifaa vyako au ofisi yako kwa ajili ya upelelezi bila oda ya Mahakama.

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. HAYA BWANA MUNGU AMJAALIE AMALIZE SALAMA SAFARI YAKE YA URAISI.

    ReplyDelete
  2. Hiii nchi na viongozi corrupt sijui kama itaendlea, kwani corruption ya uongozi ndio chanjo kikubwa cha umasiki, sas watu wasijue nini? kinachendlea katika nchi yao, hasa hapo mambo ya sirikali, siri gani zaidi ya wizi na ufisadi, si kkuwaziba mdomo raia wenye nchi, ili watu wachache waendlee kujitajilisha kwa hela za wizi wa kodi za nchii, Looo!!! this only in Africa, au Tanzania nchi zilizoendlea, zimeendelea kutokana na uwazi na ukweli hasa swala la mambo ya serikali, n hilo la viongozi hata wafanye ufusika et watu wawanyamzie tu hmm litakuwa Taifa gani? hili la kidcteta?

    ReplyDelete
  3. To hell with that and fu***k you Mr President.. Yaani ameshindwa kuongoza nchi, ameshindwa kutokomeza ufisadi nchini,, leo hii unatuletea upuuzi kama huu? Tutatukana mpaka mwisho.. ASS HOLES!!

    ReplyDelete
  4. Hawa watu au mtu kama huyo alieajiliwa na umma au umati wa watanzania. Yuko hapo kwa rahaa zake kesha sahau shida za wengi wa nchi hii anakula bataa tu anawasiwasi gani, wakati ule wa uchaguzi kuomba vote wanazunguka weee mpaka wanaumwa na kudondokaa kwenye majukwa wakishapewa kazi ulaji haaaa imekula kwao wizi ,ufisadi, kula bataaa kwa sana , hawawajari tena waliowapa hizo kazi, na bado wanatafuta hila Za kuwafunga midomo wawachune vizuri mbuzi wao, walio zoea kuburuzwa, hayaaa mnyonge mnyongeni khaki yake mpeni

    ReplyDelete
  5. tumebakia kulalamika kwa midomo na kalamu mitandaoni inabidi tutoke maandamano hata ya amani kupinga sheria hii

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad