Nchini Burundi, aliyekua mkuu wa majeshi Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza Jumatano Mei 13 kuwa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza amepinduliwa madarakani.
Meja Generali Niyombareh alisema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza.
Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari alisema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa.
Wakati Mapinduzi hayo yakitangazwa, Rais Nkurunziza alikuwa nchini Tanzania kujumuika na viongozi wa kanda ya Afrika Mashariki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu.
Baada ya tangazo la kupindulikwa kwake, Rais huyo alipanda ndege kurejea nchini kwake licha ya tangazo la kufungwa kwa mipaka yote na viwanja vya ndege.
Kwa mujibu wa taarifa ya BBC asubuhi hii ya mei 14, Ndege ya Rais huyo haikuweza kutua nchini Burundi na badala yake ilirudi tena Tanzania ambapo mpaka sasa Rais Nkurunzinza yupo jijini Dar es Salaam- Tanzania
Rais kikwete alipohutubia waandishi wa habari Dar es Salaam akiandamana na Rais Nkurunzinza
Maafisa wa jeshi la Burundi wakisheherekea Barabarani Bujumbura
Raia wakisheherekea ''Mapinduzi''
Umoja ni nguvu. Hongoreni burundi, hawa maraisi wa africa bara hili wamekalia tamaa na ubinafsi ndio uliowajaaa, mrimpigia kura na mmetoa, ata kama alikuwa hataki kutoka, alitaka leta udiktata wake sasa mmemuweza
ReplyDeleteTAMAA NYINGI MBELE GIZA TOTOROOO!SASA UMEKUWA MKIMBIZI BONGO NAWASHANGAA NYINYI VIONGOZI HASA AFRIKA KWA KUNG'ANG'ANIA KUKAA MADARAKANI ILI WAWEZE KUJILIMBIKIA MALI WANAZOZIKIMBIZA KATIKA MABENKI YA ULAYA(WAZUNGU WANAFURAHIA SANA HUU UPAMBAVU KWANI MNAWATAJIRISHA WAO)KWA NINI MSIFUATE MFANO WA MWL.NYERERE WA KUJIUZULU MWENYWEWE BILA YA MLIO WA MTUTU?NA NYIE WENGINE MLIOPO MADARAKANI MJIFUNZE KUTOKANA NA HILI LILILIMTOKEA HUYU MWENZENU NA KUMBUKENI KUWA"WATU WAKITAKA HAKI ZAO WAPE USIPOWAPA KUNA SIKU WATAJICHUKULIA WENYEWEWE KWA NAMNA YEYOTE ILE WAIONAYO INAFAA KUPATA HAKI YAO IWE KWA MTUTU AU KWA AMANI BARE THIS IN YOUR GREEDY&FILTHY MINDS WEAKED POLITICIANS
ReplyDeleteNdio akome kuwafanya wenzake wakimbizi
ReplyDeleteSafi sana na watanzania tungeweza kuking'oa CCM madarakani kwa njia hii mambo yangikuwa shwari.
ReplyDeleteWabongo kamwe hawawezi, sababu wanatokana na UDONGO WA MWISHO yaani UDONGO ULIO BAKI...fundi mwashi akimaliza kujenga kuna udongo au mchanga huwa unabakia, hivyo hulazimika kuutumia katika kazi yoyote isiyo rasmi ili mradi usipotee bure. Wabongo wanajua KULA KULALA, UTASHI sifuri, UZALENDO sifuri, UPEO sifuri, HAKI ZAO hawajui , wana-enjoy BIA ZA BEI NAFUU na kupanda DALADALA bure. Hawatumikii wananchi ingawa wajiita wa wananchi. Upeo wao wa kuona umefunikwa na mikopo ya mashangingi, nyumba, posho za vikao nk wanajiona wako peponi
ReplyDeleteINSHALLAH kuna siku hao mafisadi wanaojiita CCM(CHUKUA CHAKO MAPEMA)Nao pia tamati yao itawadia watafunga virago vyao na kutokomea kabisa kutoka katika upeo wa Watanzania wanaoipenda na kuithamini nchi yao nzuri TANZANIA Amen
ReplyDeleteCCM TANGU LINI IKATOKA MADARAKANI HIVI NYIE AKIRI MUNAZO KWELI
ReplyDeleteUshauri wa bure kwa mheshimiwa rais wa zamani Nkurunziza, usirudi tena burundi watakufanya hakuna maana tabu na vifo vinakuhusu, kumbuka Samueli Doe alifanywa nini.
ReplyDeleteNA WEWE MWENYE AKILI(NA SIYO "AKIRI"KAMA ULIVYOANDIKA)NA HIYO CCM YAKO HAMJUI KUWA KILA LENYE MWANZO HALIKOSI MWISHO?
ReplyDelete