Serikali imeahidi kumchukulia Shilole kufuatia kusambaa kwa picha zake chafu zilizopigwa wakati akitumbuiza nchini Ubelgiji.
Akizungumza bungeni Dodoma leo, Naibu Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Juma Mkamia, wakati akijibu hoja za wabunge baada ya kusoma makadirio na matumizi wa wizara hiyo, alisema tayari serikali imeliagiza baraza la sanaa taifa BASATA kufanya naye mahojiano.
“Tumemtaka ajieleze kupitia BASATA, akishajieleza serikali itachukua hatua na niombe mheshimiwa spika kupitia bunge lako tufuku, kuliomba radhi kwa upande wa serikali kwa kitendo kilichofanywa na mwanamuziki yule. Sio maadili yetu na nimesema akishajieleza serikali itachukua hatua yake,” alisema Juma Mkamia.
Huyu dada anahitaji adhabu kali sana
ReplyDeleteKuna mambo mangapi ya Haki za wasanii yanakuwa overlooked tunaishia kuhangaika na mtu nguo kuvulika bahat mbaya...CCM must go
ReplyDeleteVitu vya Nsingi mnavifumbia macho kama vile hamuoni, vitu ambavyo havina msingi na tena alikiri nguo kuwa imevuka bahati mbaya wakati wa show...Sasa wakutafutwa na kupewa adhabu ni yule alioona picha ni mbaya halafu akaisambaza... Kwa sababu ukiangalia picha iliyosambaa ni hyo moja tu hakuna zingine.... Acheni Fitna wabongo tupendane na tujifunza kufichiana aibu...
ReplyDeletenashangaa wasanii wanaibiwa kazi zao hawaoni.
ReplyDelete