The big 3: Lowassa, Chenge na Rostam kuhakikisha wanashika Ikulu?

Mbio za kutinga Ikulu mwaka huu zina mvuto aina yake huku zikionekana kutekwa zaidi na kundi la mafisadi ambao baada ya uchaguzi mkuu uliopita Andrew Chenge, Rostam Azizi na Edward Lowasa walitangazwa kwamba ni mafisadi papa na hivyo kuwataka wajiengue chama kabla hawajachukuliwa hatua za kufukuzwa kwa kukichafua chama.

Aliyetii ni Rostam Azizi kwa kujivua ubunge wa Igunga na nyadhifa nyingine chamani akiita ni siasa za maji taka, wengine Lowasa na Chenge wakavuta subira iliyowapa ahueni kutoenguliwa na bila maelezo ya kuridhishwa kwamba zile siku tisini hazikuwekwa bayana lini zinaanza.

Hatimaye Lowasa aliporejea toka kuombewa huko Nigeria aliita press comference na tishio alilosema wakati huo ni kuwa atakayeendelea kumchafua atamchukulia hatu za kisheria mahakamani, hata hivyo bungeni amekuwa mkimya wala kutoonyesha msimamo wake juu ya kashfa nzito nzito zotokeazo serikalini.

Lowasa Kujipitishapitisha kwenye mikusanyiko na mtukio aonwe na wapita kura
Kilichoendelea ni kujipitishapitisha kwenye matukio na mikusanyuiko ambayo vyombo vya habari huwepo na pia uchangiaji usiokoma katika nyumba za ibada jambo ambalo awali hakuwa analifanya.

Lowasa kukiri marafiki wanamchangia pesa za kampeni
Maswali ya wengi anapata wapi pesa hizo anazotoa misaada na kufanya kampeni, jibu alilotoa hadharani ni kuwa anachangiwa na marafiki wake, hata hivyo hakubainisha marafiki wake ni nani wala kutaja majina yao.

Chenge kuteka Rasimu ya katiba ya Warioba/Rostam kuuza hisa zake VODA
Kilichoendelea ni matukio mawili yasiyo kawaida ambapo CCM iligeuka ghafla na kuikataa Rasimu ya Warioba ambaye ni kada wa Chama cha Mapinduzi pamoja na timu yake ambayo iliwekwa na kutawazwa na serikali ya CCM yenyewe kuendesha mchakacho wa katiba, kisha Andrew Chenge akajitwisha mzigo kuileta rasimu ya katiba aliyoiandaa na kufuta vifungu vyote vilivyokuwamo kwenye Rasimu ya Warioba kuhusu kuwabana mafisadi.

Miezi michache iliyopita Rostam Azizi ameuza baadhi ya hisa zake za Voda Com kitendo kinachoweza kuzua maswali mengi wakati tukielekea uchaguzi mkuu, kama si kuongeza mtaji wa pesa za kampeni za Lowasa au ni kibiashara tu?

Kwa kuunganisha dot kufanya msitari hakuna shaka mashaka kwamba hawa mapacha watatu kuna ushirikiano wa hali na mali na ndio maana tumeona Lowasa kuwa na nguvu sana ya pesa katika safari ya kwenda MAGOGONI. Pia marafikiwa wanaomchangia pesa Lowasa hawa marafiki wenzake vigumu kuchomoka maana ni kundi moja la mafisadi papa watu walioanikwa bayana na chama chao.

Chama kutowasafisha tuhuma za ufisadi wa kukichafua chama
Tuhuma za kuwa mafisadi papa hawa watatu chamani na kwamba wanakichafua chama bado hazijasafishwa kwa watanzania wakati suala hilo limezimika kiaina bila kujua nini kitaendelea, papo hapo fisadi mojawapo ndani ya hao watatu kuwa katika mbio za kupeperusha bendera ya CCM kugombea kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kauli ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wakati akifungua kikao mojawapo cha kichama safari hii Dodoma, licha ya hotuba yake kukubaliwa na wasomi kuwa ameonyesha ukomavu kisiasa, jambo jingine alilosema kimafumbo kuwa Bwana mmoja anajiona yuko juu ya wote na hivyo tuwe makini kuchagua atakayeuzika chamani.

Hii ni dalili wazi kuwa CCM sasa hivi ipo mikononi mwa mafisadi, na ndio maana uwezo wao kifedha unawafanya kuwanunua au kuwagawa wajumbe na hivyo kuwashika wale ambao wanaona ndio watakaofanikisha timu ya mafisadi kuingia Ikulu.

HITIMISHO
Timu ya mafisadi inatumia nguvu nyingi ya pesa, pesa hizo wakishakuwa madarakani watahitaji kufidiwa, je nani atakayeumia kama si mpiga kura. Mtindo anaotumia Lowasa na timu yake kuingia Ikulu haitofautiani na ule uliyotumiwa na Kikwete, matokeo tumeyaona taifa kubebeshwa zigo la madeni, pesa za umma kushindaniwa na watumishi kutia mifukoni mwao, ufisadi kukirithi, uvunjaji haki za binadamu kushamiri, unyanyasaji vyama vya upinzani kushika kasi, vyombo vya dola kuingia katika kashfa ya kunyanyasa wananchi, nk.

Source:By Candid Scope- JF

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kama wao mafisadi papa nawewe ni fisadi nyangumi,wote wezi tuu

    ReplyDelete
  2. Huna lolote wewe mnazi tu umetumwa na wajinga wenzio. CCM wote ni mafisadi. Lowasa angalau anamaamuzi.

    ReplyDelete
  3. Huna lolote wewe mnazi tu umetumwa na wajinga wenzio. CCM wote ni mafisadi. Lowasa angalau anamaamuzi.

    ReplyDelete
  4. Yan ww mara lowassa mzur mara mchafu. Ss muache aingie madarakan afu uone atamfanya nn liz one,mtt wa kikwete na january mtoto wa makamba na akina nape nauye

    ReplyDelete
  5. dhaa ulipata vp kazi?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad