Waziri Sitta akiwa anatambua kabisa kwamba nchi ipo katika hali ya dharura, kutokana na mgomo wa mabasi, hajachukua hata hatua moja ya kushughulikia hali hii. Tulitegemea katika hali hii ya dharura, waziri mwenye dhamana ya uchukuzi angechukua hatua ya kubadilisha ratiba ya train ili angalau train zitoe huduma ya usafiri kwa wananchi katika kipindi hiki kigumu. Lakini cha kushangaza, train zimeendelea na ratiba zake za kawaida, huku ile ya Tazara hadi kigogo ikiamua kufanya safari moja badala ya mbili jana jioni.
Mgomo huu wa daladala na mabasi ya mikoani umesababishwa na uzembe wa Sitta. Sitta alijua kabisa kwamba mgomo ule wa kwanza uliahirishwa mnamo saa saba mchana baada ya ahadi za kisiasa za waziri mwenzake wa kazi na ajira, lakini yeye akijua kabisa kwamba ndiye mwenye dhamana ya usafiri nchi alikaa kimya. Hata pale madereva walipotangaza kufanya mgomo mwingine Sitta hakuchukua hatua zozote.
Mimi napata shida sana kumuelewa Sitta, ni kama vile anamhujumu Kikwete. Maana amepewa dhamana ya kuandaa katiba, akaivuruga tu kulingana na alivyojisikia yeye, alipokuwa wizara ya afrika mashariki alikuwa anatoa matamko ya hovyo hovyo tu ilimradi avuruge mambo. Ndiye huyu aliyediriki kusema Tanzania itaweza kuanzisha umoja na Burundi pamoja na Congo kwa kuwa Kenya, Uganda na Rwanda walikuwa wanafanya mambo bila kushirikisha Tanzania.
Lakini ameingia wizara ya uchukuzi, pia anafanya mambo hovyohovyo tu hata kama anajua anao uwezo wa kuyashughulikia. Najiuliza hivi mzee Sitta alishindwaje kutumia hata japo robo tu ya ubongo wake kufikiria kwamba mgogoro huu wa madereva ungeweza kuwa mkubwa kama usingeshughulikiwa? Jana anakuja eti na hoja ya kwamba ukosefu wa kamati ya kudumu ya maridhiano ndiyo sababu ya huu mgomo. Kwani tangu walipoanza malalamiko kule mwanzo kwanini hakuunda hiyo kamati. Sitta ni waziri Kimeo sana, inashangaza kuona kwamba anautaka na Urais. Mtu huwezi kushughulikia matatizo ya dharura ya nchi utawezaje kuwa Rais?
Waziri Mkuu Pinda na Samweli Sitta wanamhujumu Rais Kikwete
0
May 05, 2015