Zitto aandika mazito kuhusu CAG katika ukurasa wake wa facebook, soma hapa alichokisema

"Kumbukumbu zangu ( Machi 20, 2015)
"Mjadala mkali ulikuwa kuhusu mtiririko wa fedha kwenda kwa CAG. Sheria ya ukaguzi wa umma kifungu cha 41 na 44 kinataka PAC ikishapitisha Bajeti ya CAG kwa mashauriano na Waziri wa Fedha, Bajeti ile itolewe yote mara moja kwenda mfuko wa Ukaguzi kutoka mfuko Mkuu wa Hazina. Kutokana na upatikanaji wa Mapato ya Serikali PAC ilikubaliana na Serikali kutoa fedha mara 2 kwa mwaka. Nayo ikawa ngumu tukakubaliana mara 4 kwa mwaka. Nayo haikukutekelezwa, fedha zikawa zinatoka kwa wiki mbili mbili. Hali hii imeathiri sana utendaji wa ofisi ya CAG kiasi cha CAG kushindwa hata kununua tairi Mpya za gari yake ya kazi.
Baada ya mjadala mkali na umuhimu wa kutekeleza Sheria, PAC ilikubaliana na Waziri wa Fedha kutoa fedha za Bajeti ya CAG kwa miezi Sita Sita kwa kutoa 50% mwanzo wa mwaka wa Bajeti na 50% nyingine kila mwezi Januari.

Baada ya hapo tukajadiliana kuhusu Bajeti. Waziri wa Fedha aliomba Bajeti ibakie ile ile ya mwaka Jana wakati CAG kaomba nyongeza ya 21%. Waziri alijulisha kamati kuwa Bajeti ya mwaka 2015/16 kila wizara na idara Bajeti imekatwa kwa 19%, hivyo haitakuwa sawa kwa CAG kuongezewa. Waziri aliijulisha kamati kuwa katika Bajeti inayokuja Serikali inataka kujitegemea kwa 100%, bila misaada ya wafadhili. Ndio maana kuna punguzo la Bajeti.

PAC ilijenga hoja kwamba CAG anaanza ukaguzi wa mapato ( revenue audit ) na ukaguzi wa mikataba ya Gesi, Mafuta na Madini hivyo kwa mawanda mapya lazima Bajeti iongezeke. Baada ya mjadala tukakubaliana Bajeti ya CAG kupanda kwa 8% kutoka tshs 86 bilioni mpaka tshs 94 bilioni".
Leo ninasoma vitabu vya Bajeti ya Serikali nakuta Ofisi ya CAG imepunguziwa Bajeti chini ya kiwango cha Bajeti ya Mwaka jana. Kinyume na Sheria. Kinyume standadi za kidunia kuhusu Uhuru wa Ofisi ya Ukaguzi ya Taifa. Kisa? Kuibuliwa kwa hoja za ukaguzi? Impunity? Hili lisikubalike aslani. Mwananchi Communications Ltd The Citizen JamiiForums simamieni hili. Ofisi ya CAG ndio jicho la Watanzania. Hata kama yanayoripotiwa hayafanyiwi kazi, tujue tu. Ipo siku Wananchi wataamka na kufanyia kazi. Cloudsfm Radio EATV EFM"
Zitto Kabwe.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad