ALI KIBA Atangaza Vita na Mwanamuziki Diamond Platnumz

Brighton Masalu
VITA! Saa chache tu baada ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar akitokea nchini Marekani kwa shughuli za kimuziki, staa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ametangaza kile kinachotafsirika kuwa ni vita dhidi ya hasimu wake kwenye anga la muziki huo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Ijumaa Wikienda lina ‘full’ stori.
 cdeaw3
TUJIUNGE ENEO LA TUKIO

Ali Kiba alitema cheche Alhamisi ya wiki iliyopita ndani ya Hoteli ya Sea Cliff, Masaki jijini Dar, kulikokuwa na uzinduzi wa kampeni ya kupinga vita ujangili, iliyoratibiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii, huku akiwa ni mmoja wa mabalozi sanjari na mlimbwende wa zamani, Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi ‘K-Lyin’.

USO KWA USO NA PAPARAZI

Baada ya shamrashamra za ‘event’ hiyo, haraka sana kama mshale wa Mmakonde, mwandishi wetu alimfuata Ali Kiba, lengo kuu likiwa ni kusikia chochote juu ya ushindi wa Tuzo za Kili ambapo alizoa tano binafsi na moja ya kushirikishwa.

Kiba alisema anaamini alistahili kushinda tuzo zote kwani vigezo na sifa anazo na amejiandaa kikamilifu kupambana na yeyote anayedhani kuwa ni mfalme wa muziki huo.

JINA LA DIAMOND LAMCHEFUA!

Katika mahojiano hayo, mwandishi wetu alimkumbusha Ali Kiba uwepo wa Diamond ambapo kwa haraka sana alimkata kauli mwandishi kwa kusonya na kuweka wazi kuwa miongoni mwa mambo ambayo humpa kichefuchefu, ni pamoja na kusikia jina la Diamond likitajwa mahali popote penye uwepo wake!

“Kaka, sitaki kabisa kulisikia jina hilo, linanipa kichefuchefu, unajua kwa kipindi ambacho nilikaa kimya, nilikuwa nausoma mchezo lakini hakuna aliyeweza kuchukua kiti changu na kuamua kurejea ulingoni kwa kishindo na kuanzia sasa hivi ni mapambano mwendo mdundo,” alisema  Kiba na kuongeza:

“Simaanishi kuwa hakuna msanii mzuri kama mimi, naomba nisieleweke vibaya, wapo lakini siyo huyo dogo (Diamond), muziki ni zaidi ya mbwembwe, niko kikazi na sasa nimedhamiria kweli, kama anaamini yuko fiti, kazi zitaweka wazi ukweli na si drama za kitoto.”

 VIPI KUHUSU YEYE NA WEMA?

Mwandishi wetu alitaka kujua kulikoni msanii huyo alimuweka Wema Sepetu kwenye ukurasa wake wa Instagram akimmwagia shukrani lukuki na si mtu mwingine?

“Wema amekuwa ni shabiki wangu wa siku nyingi mno, alianza kunipenda kupitia wimbo wangu wa Hands Across the World (kwenye Project ya One-Eight) na kuanzia hapo amekuwa akinipa sapoti kubwa sana, siwezi kukaa naye mbali eti kisa huyo jamaa (Diamond).

“Naamini kwa asilimia nyingi sana hata huu ushindi wangu wa tuzo, umechangiwa na sapoti yake pamoja na wadau wangu wengine,” alisema Kiba.

 AFUNGUKA KUHUSU VIDEO YA MWANA!

Pia, mwandishi wetu alimtaka staa huyo kufafanua madai ya kutoitendea haki video ya Wimbo wa Mwana, ambapo alisema, watu wengi walitarajia aifanye kulingana na mawazo yao ndiyo maana akaamua afanye vile anavyoaamini ingekuwa bora.

“Kila mtu alikuwa ameshatengeneza picha ya jinsi video ya wimbo itakavyokuwa, halafu sifanyi kazi kwa kushindana na mtu, ndiyo maana ilionekana tofauti na mawazo ya wengi, namalizia kwa kusema salamu zimfikie jamaa (Diamond) kuwa mapambano ndiyo kwanza yameanza,” alisema Kiba.

 DIAMOND ANASEMAJE?

Hadi tunakwenda mitamboni, jitihada za kumpata Diamond aweze kuzungumzia vita hiyo iliyofufuka upya hazikuzaa matunda kufuatia simu ya staa huyo aliyekuwa nchini Afrika Kusini kikazi, kuita bila majibu.

 TUJIKUMBUSHE

Kwa muda mrefu sasa, Kiba na Diamond wamekuwa wakiripotiwa kuwa na bifu la chini kwa chini linalotokana kugombania ufalme wa muziki Bongo.
Tags

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ha ha ha ha ha jipe moyo kaka dushelele, mijimbo yako yoote haina mvuto hata robo.

    ReplyDelete
  2. pumbavu fanya yako usingalie ya mwenzako

    ReplyDelete
  3. wambea wakubwa nyie mna kazi ya kuwagombanisha ndugu zetu ili muuwe sanaa ya muziki Tanzania acheni unafki ni bora mngekuwa mkiwashauri kumaliza tatizo tusonge mbele kuliko hayo mnayoandika.

    ReplyDelete
  4. akatangaze vita na malaya wake DAI hana shida ya kutangaza vita

    ReplyDelete
  5. Kiba ni mtu wa busara sana awezi kuongea huo ujinga acheni uchonganishi

    ReplyDelete
  6. Magazeti uchwara ndo yanawachonganisha hawa madogo ili wapate kuuza magazeti yao,waacheni madogo wapige kazi,huo udaku wala c kuupandisha mziki wa bongo fleva,mziki wa dansi mliuua kwa mambo kama haya msondo na sikinde matokeo yake mziki wa dansi chali,soka limetushinda basi waacheni vijana wa sekta ya bongo fleva wapeperushe bendera ya taifa,sio kila siku kuwatengenezea mabeef uchwara,hatujengi ng'o

    ReplyDelete
  7. Kabebwa kwa kupewa tuzo 5 za bure, sasa anaonyesha kifua.. Ki muziki mwaka huu hakuna alichokifanya

    ReplyDelete
  8. Kusema ukweli watanzania tunatia aibu sana, waandishi wa habari/blogs/watangazaji na wengine walio kwenye media wanafanya kila njia kutulisha mambo ya kipuuzi na yasiyokuwa na maana yoyote wakati mwingine, na sisi kama jamii tunayapokea na kuyakumbatia na kuyashabikia hata kufikia kuhatarisha maisha yetu. Hebu tujiulize bifu kama kweli lipo kati ya Ali Kiba na Dimond linafaida gani kwao wenyewe na kwetu mashabiki?

    Marekani kulikuwa na makundi yanayowekeana bifu mashariki na magharibi mwisho wake ikawa ni vifo vya wanamuziki mahiri Tupac na BIG, lakini bado yakaendelea kuwepo mabifu madogo madogo ambayo mengi yamemalizwa baada ya watu kutokuona faida yake na kadri siku zinavyokwenda yanaenda yakipungua zaidi. leo hii tunaishi katika dunia ambayo tunajifunza na kujirekebisha kutokana na makosa, tumeona kwa wenzetu hatuna cha kujifunza? Hapa kwetu kuliwahi kuwa na bifu kati ya Dudu Baya na Mr.Nice halikuwapeleka popote zaidi ya kuwapoteza na mpaka leo hawapo kwenye ushindani wa kimuziki.

    Bifu haisaidii chochote, huwezi kujipandisha kwa kumshusha mwenzio, na kama wote tukiona kwamba bifu la kiba na Dimond kama kweli lipo na ni kubwa kiasi hicho halina maana na tukalikemea na kulipuuza kwa pamoja litakwisha, ni rahisi kiasi hicho, lakini tukiachia media ikatulisha upuuzi tukauamini na kuwaaminisha Ali Kiba na Dimond kama jamii tutakuwa tumefeli sana.

    Hizi team Kiba na team Dimond ziache ushabiki usiokuwa na tija bali zifanye jitihada za kuwashauri, kuwasaidia ktk utunzi, kuwasapoti katika kununua album na biashara watakazoanzisha/walizonazo na mengine mengi ya kuwainua wanamuziki na kuwafanya wakue kimuziki, kibusara na kiuchumi.

    Kila mmoja anauwezo wa kushine bila kumzuia mwingine, jiulize Marekani au Nigeria kuna wanamuziki wangapi wenye mafanikio kimaisha na kiuchumi na hawana mabifu ya kijinga?

    Viongozi wa vyama vya burudani ( ikiwepo BASATA) na wizara inajua juu ya bifu hili la kijinga lakini hakuna kinachofanyika, mwishowe kwa sababu ya ulimbukeni wetu watu wanampigia kura DAVIDO kwa sababu tu ya chuki ya kuambukizwa ambayo wengi hata hawajua imeanzia wapi. AIBU.

    Hivi kweli leo hii Dimond akikosa tuzo za MTV ikaenda kwa Davido wewe Mtanzania inakusaidia nini? unafikiri Wanigeria watakuona shujaa? watakusifia kwa kitendo cha kishujaa?

    Hivi kweli hawa waliopo kwenye uongozi kwenye sekta ya burudani hawaoni sababu ya kukaa na hawa vijana wadogo wawili na kujaribu kujua tatizo ni nn na kulimaliza?

    hebu jaribu ku-imagine siku hakuna bifu kati ya Dimond na Ali Kiba halafu kizuri zaidi wamefanya Colabo hawa waliojiajiri kwenye hizi team KIBA na Team DIMOND wataaibika kiasi gani? mauzo ya hiyo colobo yatakuwa makubwa kiasi gani? sifa za busara zao zitavuma kwa umbali gani? pesa watakazopata ni nyingi kiasi gani? nchi itapata sifa kiasi gani kuwa na wanamuziki wazuri wanaoshirikiana? TUJIULIZE.

    ReplyDelete
  9. Kusema ukweli watanzania tunatia aibu sana, waandishi wa habari/blogs/watangazaji na wengine walio kwenye media wanafanya kila njia kutulisha mambo ya kipuuzi na yasiyokuwa na maana yoyote wakati mwingine, na sisi kama jamii tunayapokea na kuyakumbatia na kuyashabikia hata kufikia kuhatarisha maisha yetu. Hebu tujiulize bifu kama kweli lipo kati ya Ali Kiba na Dimond linafaida gani kwao wenyewe na kwetu mashabiki?

    Marekani kulikuwa na makundi yanayowekeana bifu mashariki na magharibi mwisho wake ikawa ni vifo vya wanamuziki mahiri Tupac na BIG, lakini bado yakaendelea kuwepo mabifu madogo madogo ambayo mengi yamemalizwa baada ya watu kutokuona faida yake na kadri siku zinavyokwenda yanaenda yakipungua zaidi. leo hii tunaishi katika dunia ambayo tunajifunza na kujirekebisha kutokana na makosa, tumeona kwa wenzetu hatuna cha kujifunza? Hapa kwetu kuliwahi kuwa na bifu kati ya Dudu Baya na Mr.Nice halikuwapeleka popote zaidi ya kuwapoteza na mpaka leo hawapo kwenye ushindani wa kimuziki.

    Bifu haisaidii chochote, huwezi kujipandisha kwa kumshusha mwenzio, na kama wote tukiona kwamba bifu la kiba na Dimond kama kweli lipo na ni kubwa kiasi hicho halina maana na tukalikemea na kulipuuza kwa pamoja litakwisha, ni rahisi kiasi hicho, lakini tukiachia media ikatulisha upuuzi tukauamini na kuwaaminisha Ali Kiba na Dimond kama jamii tutakuwa tumefeli sana.

    Hizi team Kiba na team Dimond ziache ushabiki usiokuwa na tija bali zifanye jitihada za kuwashauri, kuwasaidia ktk utunzi, kuwasapoti katika kununua album na biashara watakazoanzisha/walizonazo na mengine mengi ya kuwainua wanamuziki na kuwafanya wakue kimuziki, kibusara na kiuchumi.

    Kila mmoja anauwezo wa kushine bila kumzuia mwingine, jiulize Marekani au Nigeria kuna wanamuziki wangapi wenye mafanikio kimaisha na kiuchumi na hawana mabifu ya kijinga?

    Viongozi wa vyama vya burudani ( ikiwepo BASATA) na wizara inajua juu ya bifu hili la kijinga lakini hakuna kinachofanyika, mwishowe kwa sababu ya ulimbukeni wetu watu wanampigia kura DAVIDO kwa sababu tu ya chuki ya kuambukizwa ambayo wengi hata hawajua imeanzia wapi. AIBU.

    Hivi kweli leo hii Dimond akikosa tuzo za MTV ikaenda kwa Davido wewe Mtanzania inakusaidia nini? unafikiri Wanigeria watakuona shujaa? watakusifia kwa kitendo cha kishujaa?

    Hivi kweli hawa waliopo kwenye uongozi kwenye sekta ya burudani hawaoni sababu ya kukaa na hawa vijana wadogo wawili na kujaribu kujua tatizo ni nn na kulimaliza?

    hebu jaribu ku-imagine siku hakuna bifu kati ya Dimond na Ali Kiba halafu kizuri zaidi wamefanya Colabo hawa waliojiajiri kwenye hizi team KIBA na Team DIMOND wataaibika kiasi gani? mauzo ya hiyo colobo yatakuwa makubwa kiasi gani? sifa za busara zao zitavuma kwa umbali gani? pesa watakazopata ni nyingi kiasi gani? nchi itapata sifa kiasi gani kuwa na wanamuziki wazuri wanaoshirikiana? TUJIULIZE.

    ReplyDelete
  10. Kusema ukweli watanzania tunatia aibu sana, waandishi wa habari/blogs/watangazaji na wengine walio kwenye media wanafanya kila njia kutulisha mambo ya kipuuzi na yasiyokuwa na maana yoyote wakati mwingine, na sisi kama jamii tunayapokea na kuyakumbatia na kuyashabikia hata kufikia kuhatarisha maisha yetu. Hebu tujiulize bifu kama kweli lipo kati ya Ali Kiba na Dimond linafaida gani kwao wenyewe na kwetu mashabiki?

    Marekani kulikuwa na makundi yanayowekeana bifu mashariki na magharibi mwisho wake ikawa ni vifo vya wanamuziki mahiri Tupac na BIG, lakini bado yakaendelea kuwepo mabifu madogo madogo ambayo mengi yamemalizwa baada ya watu kutokuona faida yake na kadri siku zinavyokwenda yanaenda yakipungua zaidi. leo hii tunaishi katika dunia ambayo tunajifunza na kujirekebisha kutokana na makosa, tumeona kwa wenzetu hatuna cha kujifunza? Hapa kwetu kuliwahi kuwa na bifu kati ya Dudu Baya na Mr.Nice halikuwapeleka popote zaidi ya kuwapoteza na mpaka leo hawapo kwenye ushindani wa kimuziki.

    Bifu haisaidii chochote, huwezi kujipandisha kwa kumshusha mwenzio, na kama wote tukiona kwamba bifu la kiba na Dimond kama kweli lipo na ni kubwa kiasi hicho halina maana na tukalikemea na kulipuuza kwa pamoja litakwisha, ni rahisi kiasi hicho, lakini tukiachia media ikatulisha upuuzi tukauamini na kuwaaminisha Ali Kiba na Dimond kama jamii tutakuwa tumefeli sana.

    Hizi team Kiba na team Dimond ziache ushabiki usiokuwa na tija bali zifanye jitihada za kuwashauri, kuwasaidia ktk utunzi, kuwasapoti katika kununua album na biashara watakazoanzisha/walizonazo na mengine mengi ya kuwainua wanamuziki na kuwafanya wakue kimuziki, kibusara na kiuchumi.

    Kila mmoja anauwezo wa kushine bila kumzuia mwingine, jiulize Marekani au Nigeria kuna wanamuziki wangapi wenye mafanikio kimaisha na kiuchumi na hawana mabifu ya kijinga?

    Viongozi wa vyama vya burudani ( ikiwepo BASATA) na wizara inajua juu ya bifu hili la kijinga lakini hakuna kinachofanyika, mwishowe kwa sababu ya ulimbukeni wetu watu wanampigia kura DAVIDO kwa sababu tu ya chuki ya kuambukizwa ambayo wengi hata hawajua imeanzia wapi. AIBU.

    Hivi kweli leo hii Dimond akikosa tuzo za MTV ikaenda kwa Davido wewe Mtanzania inakusaidia nini? unafikiri Wanigeria watakuona shujaa? watakusifia kwa kitendo cha kishujaa?

    Hivi kweli hawa waliopo kwenye uongozi kwenye sekta ya burudani hawaoni sababu ya kukaa na hawa vijana wadogo wawili na kujaribu kujua tatizo ni nn na kulimaliza?

    hebu jaribu ku-imagine siku hakuna bifu kati ya Dimond na Ali Kiba halafu kizuri zaidi wamefanya Colabo hawa waliojiajiri kwenye hizi team KIBA na Team DIMOND wataaibika kiasi gani? mauzo ya hiyo colobo yatakuwa makubwa kiasi gani? sifa za busara zao zitavuma kwa umbali gani? pesa watakazopata ni nyingi kiasi gani? nchi itapata sifa kiasi gani kuwa na wanamuziki wazuri wanaoshirikiana? TUJIULIZE.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad