Tuzo za muziki Kilimanjaro, KTMA 2015, zimefanyika Jumamosi hii katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam ambapo Alikiba ameongoza kwa kuchukua tuzo tano.
Joh Makini akiwa mwenye furaha baada ya kukwaa tuzo
Joh Makini ni mmoja wa washindi usiku wa Jumamosi
Tuzo alizoshinda Alikiba ni pamoja na mtumbuizaji bora wa muziki wa kiume, Wimbo bora wa mwaka, mtunzi bora wa mwaka muziki wa bongo fleva, msanii bora wa mwaka pamoja na mwimbaji bora wa kiume wa Bongo Flava.
“Nawashukuru media zote na wote kwa kweli pongezi nyingi zinaenda kwa my strongest #Teamkiba yourthe best #kingkiba_for_life,” ameandika Kiba kwenye Instagram. Msanii huyo kwa sasa yupo Dallas nchini Marekani.
Diamond, Vanessa Mdee, Mzee Yusufu,Isha Mashauzi pamoja na Joh Makini wote wameibuka na tuzo mbili kila mmoja.
“#GODENGINEERING #TEAMWEUSI WE DID IT AGAIN !!! WE WON TWO!! KILIMANJARO TANZANIA MUSIC AWARDS!! THANK Y’ALL FOR VOTE,” ameandika Joh Makini.
Hii ni orodha nzima ya washindi wa KTMA 2015:
Mtumbuizaji bora wa muziki wa kiume wa mwaka – Alikiba
Mwimbaji bora wa kike Bongo Flava ameshinda – Vanessa Mdee
Msanii bora wa kiume Taarab – Mzee Yusuph
Mwimbaji bora wa kike Taarab – Isha Mashauz
Mwimbaji bora wa kiume bendi – Jose Mara
Wimbo bora wa mwaka wa muziki wa Taarab – Mapenzi Hayana Dhamana – Isha Mashauzi
Wimbo bora wa mwaka – Mwana (Alikiba))
Wimbo bora wa Kiswahili bendi – Walewale (FM Academia)
Wimbo bora wa muziki wa R&B – Sisikii (Jux)
Wimbo bora wa Hip Hop – Kipi Sijasikia (Professor Jay)
Wimbo bora wa Reggae & Dance Hall – Let Them Know (Maua Sama)
Rapper bora wa mwaka, bendi – Ferguson
Msanii bora wa Hip Hop – Joh Makini
Wimbo bora wa Afrika Mashariki – Sura Yako (Sauti Sol)
Mtunzi bora wa mwaka, Taarab – Mzee Yusuph
Mtunzi bora wa mwaka, Bongo Flava – Alikiba
Mtunzi bora wa mwaka, bendi – Jose Mara
Msanii bora chipukizi – Baraka Da Prince
Mtunzi bora wa mwaka Hip Hop – Joh Makini
Bendi bora ya mwaka – FM Academia
Mtayarishaji bora wa nyimbo, Bongo Flava – Nahreel
Mtayarishaji bora wa nyimbo wa mwaka, Taarab – Enrico
Mtayarishaji bora wa nyimbo wa mwaka, bendi – Amoroso
Wwimbo bora wenye vionjo vya asili ya Kitanzania – Mrisho Mpoto
Kikundi bora cha mwaka muziki wa Taarab – Jahazi Modern Taarab
Kikundi bora cha mwaka muziki wa Bongo Flava – Yamoto Band
ALI KIBA Azoa Tuzo Tano Kwa Mpigo Tuzo za Kilimanjaro Music 2015
6
June 14, 2015
Ha ha ha yaani nimeamani nasiasa zimeanza kiingia kwa wimbo upi?hata mfanyeje dai ni levo nyingine
ReplyDeletehongera kiba watakuelewa tuu, domo wapiiiiiiiii
ReplyDeleteKtm ni mbululazzz wote etmtumbuizaji hata haibu hamna kwelii sijawai ona wapuuzi kama hawa hata mfanyeje diamond ni moto mwingine
ReplyDeleteAlikiba na yeye anajua rohoni kwamba hamna kitu bado sanaaaa
ReplyDeleteKiba BADO Sana kwa dai na yeye anajua hilo
ReplyDeleteHata mukimpa tuzo 20 poa tu hatujali sisi tunaangali mitaa ya juu huko international dai still another class mupo?
ReplyDelete