Dina Marious wa Clouds FM Aamua Kufunguka..Kumbe Amewekwa Benchi Kutangaza..Adai Anaonewa Sana Katika Kipindi Kibaya Kwake

Kupitia Ukurasa wake wa Instagram Mtangazaji Dina Marious Amefunga Mengi kuhusa hali yake na nini kinaendelea kwenye Ajira yake baada ya muda mrefu kuwa kimya:

Ameandika Haya:

'Katika haya maisha hamna kitu kibaya kama kumuonea na kumnyanyasa mtu ambaye hana hatia.Kwa kutumia cheo,madaraka,nguvu na nafasi uliyonayo ukiamini huyo mtu hana uwezo wa kukufanya lolote

Tunaishi katika dunia ambayo binadamu wamekosa utu na imani.Binadamu wamekuwa wanyama na makatili kuliko wanyama wenyewe.Unaweza ukakutana na simba na chui porini mkakaa mkatia story lakini sio binadamu.

Unafanyiwa unyama eti kisa wanataka revenge kwa mtu wako wa karibu.Ambae revenge hiyo wala haimuathiri lolote zaidi ni kukutesa wewe kisaikolojia siku hadi siku.
Mbaya zaidi sikustahili miaka yote nimejituma,nimejitoa,sijawahi kumvunjia heshima alokuwa juu yangu kwa ngazi zoote.

Ndugu zangu nimeishi kwa muda mrefu katika huzuni,msongo wa mawazo.Na hapa niliponimedevelop na vidonda vya tumbo.Nimekuwa na kitu kifuani kimenikaaa kila siku nahisi nisiposema nitakufa.Ningekuwa nimetendewa haki isingeniuma wala kunisumbua ni kwa sababu nimeonewa sanaa tena katika kipindi kibaya sana.

All this time nimekuwa mnyenyekevu na najichekesha nakujitabasamisha machoni pa watesi wangu.Na wao wakiendelea kunikanyagia chini bila huruma huku wakinichekea.

Leo nimeamka nina huzuni sana sana na ninahuzunika hasa ninapokutana na msg za kuniuliza niko wapi?mbona sisikiki??
Mimi bado ni muajiriwa na ninalipwa mshahara ila nimewekwa benchi tu.

Kuna kitu naomba nikiweke clear kumekuwa na maneno mengiiiiii yanazunguka kuwa nina ugomvi na Zamaradi.Mimi sina ugomvi na Zamaradi sijui ndio amechangia mimi kutolewa kwenye leo tena.Thats not true wala nguvu hiyo hana.Sijajua why watu husema hivyo ila sina ugomvi nae.Hata yeye anajua hatuna ugomvi wowote.Nilipotoka pale niliamua kubadili mfumo wangu wa maisha hivyo hatuna ukaribu kama zamani.Ila haimaainishi tuna ugomvi.

Na malizia kwa kusema sipo radio wala sipo tv kwa sasa.Maswali mnaniuliza kila siku na nina wajibu kila mara na leo nimewajibu tena.
ila nitakuwa kwa radio na tv hapo baadae acha niuze mafuta ya nazi.Maelezo ya mwanzo yamejitosheleza sanaa na sitaenda mbalii sanaa labda nikiandike kitabu ndio yatatimia.

Nimeandika haya kwa ufupi mjue hata sisi pamoja na majina tuliyonayo changamoto zipo na tunakabiliana nazo.Na ipo siku tutashinda maana mtetezi wetu yu hai ' Dina Marious





Tanzania Hottest Celebrity Gossip New

Post a Comment

13 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nenda Radio Station Nyingine, Sauti Unayo Uwezo Wa Kufanyakazi Unao, Usijipe Jakamoyo, Sononi Inaua Na Vidonda Vya Tumbo Ni Balaa. Japo Umechelewa Kidogo Ila Sio Issue Resign Kamata Radio Station Nyingine Uzuri Ni Kwamba Zipo Kibao Kwa Sasa Has a Kwa Mtangazaji Kama Wewe.

    ReplyDelete
  2. Sister wewe una afya yako na ujuzi unao, usikubali kunyayaswa lazima uweke heshima yako mbele. kabla ya kitu chochote hata ikibidi kubadilisha kazi kwa muda mpaka pale utapopata kazi ya utangazaji, Anaetoa riziki ni MwenyeziMungu. Nakutakia kila la kheri.

    ReplyDelete
  3. Rugeee!!unafikiri riziki za watu ziko mikononi mwako?Dada yangu una kipaji kokote utakako kwenda utatusua, move on usiangalie nyuma najua ni ngumu lakini ndio binadamu,usiwaze sana ukapata stress and u got potential move on,remember when one door closed three Will be open for you keep god first.

    ReplyDelete
    Replies
    1. bora jide aliamua kukaa mbali wewe waogopa nini??

      Delete
  4. Mungu ana sababu na wewe kumbuka binadamu akikuambia no kwa Mungu ni Big Yes sababu riziki ya mtu iko miguuni mwake..Usifadhaike moyoni mwako samehe na kusahau yaliyopita maana Imeandikwa Nimeanda meza mbele ya watesi wako hakika wema na fadhili zitakufuata siku zote za maisha yako..

    ReplyDelete
  5. Ukimpiga chura teke unamuongezea hatua..si bure soon tutakuona CNN au BBC salimia Zion

    ReplyDelete
  6. Dah pole sana,,,maisha popote kama mkataba haukufungi anza kutafuta radio station nyingine ukipata 24 hours notice then quit from them,,,ushatupiwa virago its just a matter of tym

    ReplyDelete
  7. Riziki popote dada, songa mbele-pambanaa!!! hujachelewa achana nao hao jamaaa...hawajui kukaa na wafanyakazi.


    ReplyDelete
  8. Na wewe uliona kama clouds ndiyo wazazi wako, ulikuwa unawabania wenzio, kama Hando na Babla wanavyombania Fred, ndiyo mjifunze cha mweznio siyo chako, nenda EFM utapata kazi,

    ReplyDelete
  9. Nashangaa mnavyomuhurumia,jamani kipindi kizima alikuwa anataka aongee yeye Tu,wenzie anawakatisha wasiongee msyuuuuuu malipo Ni hapahapa,sasa hivi bila yy kipindi kimekuwa kizuri zaidi nenda mwanamke msyuuuu

    ReplyDelete
  10. Duuu pole sana dada ila kumbuka nyuma kama ulikuwa unawafanyia wenzio ubaya,Mungu huwa analipa hapahapa,jirekebishe songa mbele

    ReplyDelete
  11. pole sana dada yangu achana nao songa mbele

    ReplyDelete
  12. Kama mnaelewana vizuri na Kaka Millard Ayo,
    Zungumza naye Uendelee na Kazi dada yangu
    Katika Studio yake Mpya,una uwezo Mzuri wa kufungua ukurasa mpya,kipindi kipya kitachowafanya wadau na wasikilizaji wako kukufuata,
    Una haki ya kufanya kazi sehemu nyingine,sio lazima kujishikilia pasipoeleweka na penye watu na mambo yao,
    Binadamu hatuishi kunena na kulalama,
    Focus na Kazi yako D,
    By the Way i use to admire what you did in there, coz you get everthn that a Presenter needs.
    So get out of that emotional thing and wake up ,Please.
    Malik +255 712 499 886

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad