Jamani Housegirl wangu Huyu, Ananitafuta ubaya! (STRICTLY KWA WANAUME TU)

Jamani naomba ushauri kuhusu hili.

Mimi ni mume wa mke mmoja na watoto wanne. Hivi karibuni tumepata housegirl mpya kutoka Singida, amemaliza form four hakubahatika kuendelea na masomo kwa sababu ya kukosa sifa za shule za serikali. Ni mzuri wa kawaida, yaani hana muonekano ule wa mahousegirl-naamaanisha muonekano choka mbaya kweli anafaa hata kuwa mke wa mtu. Katika historia yangu sijawahi hata siku moja kutembea na housegirl na mpaka sasa nishaajiri hao h/girl si chini ya 6, huwa niko very serious na sitaki mazoea nao hata kidogo.

Huyu amekuja naona anataka kuniangusha katika msimamo wangu huu. siku ya kwanza kutambulishwa kwake alionekana kushituka sana ingawa na mimi kwa ndani nilimkubali kuwa mzuri. Maisha yakaendelea na siku zikafunguka. Sasa toka siku hiyo amekuwa anakosa sana sana tu confidence ninapokuwa nyumbani, mara atajikwaa, mara ataogopa kuja mbele yangu n.k mbaya zaidi ninapokuwa peke yangu lets say wengine wapo mbali ananichangamkia sana na kutabasamu muda wote kila nitakalooongee yeye anatabasamu hata kama si la kufurahisha, nikimtuma kitu ataniletea wakati napokea anainua kichwa kuniangalia kiuchokozi halafu anatabasamu, basi na mimi nikawa natabasamu. Ikitokea labda nimerudi nyumbani na nahitaji chakula mapema atanipikia vizuri sana wakati mwingine anongeza kitu ambacho hakikupangwa kwenye ratiba ya chakula cha siku hiyo, anaweza kunkaangia mayai au akachemsha chai ya maziwa akaweka na viuongo haraka haraka na kunipatia chakula.

Tatizo, wife keshamshitukia hizo nyendo zake, amekuwa kila mara ananiuliza kuhusu mtu huyu, anasema mbona fulani ukiwepo anakuwa hana confidence nikamwambia mi sijui embu muulize alipomuuliza akamjibu wife kuwa eti ananiogopa kwa sababu aliambiwa na mlinzi mi ni mkali sana achunge asinikorofishe. Lakini ukiangalia mapozi yake kwangu si ya mtu anayemuogopa. Si hizi ameongeza zaidi, kunisalimia/kuniamkia kwake imekuwa ngumu sana ni mara mojax2 sana. Mi kwa ujumla ni mtu nisiyejali vitu vidogo vidogo na nilichojaribu kufanya ni kuwa mbali nae, nimeongeza kuwa serious, na wakatui mwingine nakuwa mkali ninapoongea nae ili awe mbali nami au afute hicho anachofikiri au kukitafuta, Lakini nahisi ananitafuta ubayaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!

Nimfanyeje? au nifenye lakini nahisi kujidhalilisha kwa mah/girl!
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kama wewe kweli unampenda mkeo kiukweli deep down from the bottom of your heart na unaijali na kuiheshimu ndoa yako kama unavyosema ni mtu "Serious"then just quit it off coz this 5/10 minutes of making love 2 your housegirl mighty cost your marriage so if you want it to happen then siku moja mdandie tu housegirl wenu halafu uone matokeo yake or just think this what you're telling us if it's true or n't but it's happening to your wife i mean she and a houseboy what would be your reaction after knowing it?Usilete mambo ya mkuki kwangu nguruwe mtamu na kwa binadamu mchungu stupid greedy selfish mentality

    ReplyDelete
  2. Tatizo moja la dhambi ukithubutu kuitenda siku ya kwanza kamwe hautaiacha kirahisi utakuwa mtumwa wake kifuatacho ni vurugu na kuvunjika kwa ndoa yako takatifu. kama leo ukithubutu kwa housegirl wako kesho tambua utathubutu zaidi kwa secretary wako ofisini au kwa wanawake wa nje ya nyumba yako. Acha hizo fikra chafu na za kiibilisi za mpango wa kando au kuchepuka. Ndoa yako ni ya thamani sana ndugu ebu fikiria mlipotoka na mkeo miaka yote hiyo mpaka sasa Mungu kawajaalia watoto wanne, kwa shukrani za kishenzi hizo za kutaka mapenzi na housegirl wako ndo unazotaka kumrudishia Muumba wako? Acha mara moja huo mpango wa kishetani. Usiruhusu starehe za tamaa za dakika chache ziharibu ndoa yako na maisha ya familia yako. Ebu fikiria mkiachana na mkeo kutokana na huo ushenzi unaoutamani kuufanya watoto wenu watalelewa na nani? Malezi ya baba na mama ni muhimu katika makuzi ya watoto. Tena ondoa fikra hizo za kijinga akilini mwako. labda nikuulize na mimi swali, hivi ni kipi haswa ulichokikosa kwa mkeo mpaka kuanza kuwa na fikra za kishenzi kama hizo? Sababu umetuambia umekuwa na mahousegirls takribani sita hapo kwako sasa kwani huyo aliyepo kwa sasa ana nini cha ajabu mpaka uanze kuweweseka kiasi hicho mwanaume mzima mwenye kujitambua? Usipokuwa makini utamaliza mabucha yote lakini nyama ni ileile kwa kudanganyika na msemo wenye hila ya kishetani kwamba mchuzi mmoja lakini mapishi tofauti. Angalizo hata kama mapishi ni tofauti lakini ni bora mchuzi uliouzoea maana michuzi ya siku hizi matatizo matupu utakuja upaliwe bure alafu tena urudi humu ho jamani naombeni ushauri. Kuna maradhi yametapakaa kila kona siku hizi acheni tabia zenu za kisheni za kupalamiapalamia watu hovyo bila ya kuwa na staha. Naimani utakuwa umenipata baki njia kuu linda mkeo na familia yako. Usitulete mawazo ya kishenzi humu ndani kuna mambo mengi ya msingi ya kufanya.

    ReplyDelete
  3. Simama na msimamo wako kama kwel hujaanzisha mahusiano nae na kam mnatilia mashaka ongea na mkeo ili aondoke huyo msichana, nawapenda sana wanaume wenye msimamo kwenye ndoa zao

    ReplyDelete
  4. NA MWAMBIE MKEO SINGIDA HAKUNA MAHOUSE GIRL ILA KAMA ANATAKA KUFUNGUA BAA NDO AKATAFUTE HUKO. WATAMLETEA PESA NYINGI. NA BAA YAKE ITAJAZA SANA

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad