January Makamba Kaharibu Utamu wa Hotuba kwa Kusema Uongo

Nimemsikiliza Januari Makamba wakati akitangaza nia, amezungumza mambo mengi lakini ameharibu utamu wa hotuba hiyo kwa kusema uongo.

Makamba katika hotuba yake amesema itachukua miaka mingi hata kumi kwa Tanzania kuanza kuvuna gesi na rais ajaye anaweza akaondoka madarakani bado gesi haijaanza kutumika.

Huu ni uongo wa wazi ana pengine inaweza kuwa ni kutojua kwamba tayari gesi imeanza kutumika kwenye maeneo mengi ikiwemo kweye viwanda mbalimbali hususani kwenye jiji la Dar es Salaam na kuna maeneo mengine kwenye majumba inatumika.

Namshangaa Januari anaposema gesi haitotumika kwa miaka ya karibu, anataka kutuambia hata mioundo mbinu ya gesi iliyojengwa itaanza kufanya kazi baada ya miaka kumi?

Namshauri aache kuzungumzia mambo ambayo hayajui na kama anatamani kuyazungumzia basi angeuliza kwa wataalamu wa masuala ya gesi kabla ya kufungua mdomo kuongea asiyoyajua.

Kwa mujibu wa wizara ya nishati na madini gesi itaanza kutumika miezi michache ijayo na tayari mabomba ya gesi yamekamilika kwa asilimia 90 na hata kiwanda cha DANGOTE kinachojengwa kitatumia gesi hiyo ambapo kiwanda hicho kitaanza uzalishaji mwezi wa nane kwa maana hiyo gesi itaanza kutumika kabla ya kiwanda hicho kuanza uzalishaji,

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. HUYU, SI NDIO WALE WALE VILAZA, WASIOPENDA MAENDELEO YA HII NCHI FISADI TU, KWANZA HUYU NDIO MMJA WAPO WA SHUT UP LAW. NDIO MAANA WALIKUWA VIMBELEMBELE, KUWEKA SHUT UP LOW ILI WAFANYE YAO BILA KUJULIKANA, SI UNAONA ANAKUJA NA UONGO MAHUSUSI, ANATAKA KUWAFANAYA TANZANIA WOTE IGNORANT,

    ReplyDelete
  2. Inaonekana wewe ni mpinzani wa January, hakusema kutumika Gas alisema kupata pesa .
    Kutumika gesi na kupata faida ikatumika kwenye nchi nivitu viwili tofauti.

    Sasa alicho sema yeye ni kuwa yale mapesa ya gesi kupatikana yakatumika ndani ya nchi itachukuwa muda mrefu.

    ReplyDelete
  3. Wewe uliyeweka hii post ndo mwongo.January hakusema hivyo.Alisema kuwa serikali haitafaidika na mapato ya gesi hadi mkataba uliopo sasa na wawekezaji wa hiyo gesi utakapoisha .Hapo ndipo serikali itaanza kupata mapato ya moja kwa moja ya gesi hiyo.Acha kukurupuka

    ReplyDelete
  4. YAAAANI CCM IMEKWISHA JANUARI NDIO MJUMBE WA KAMPENI KWELI MWISHO WA CCM UMEFIKA

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad