Kauli ya Mwigizaji Steve Nyerere Baada ya Wadau Kudai Amekurupuka Kufuata Mkumbo Kutangaza Kugombea UBUNGE Kinondoni

Staa wa Bongo Movies na aliyekuwa mwenyekiti wa Bongo Movie Unit, Steve Mengere ‘Steve Nyerere’ ambaye wiki iliyopita alitangaza niua yake ya kugombe ubunge mwaka huu wa uchaguzi amedai kua hajakurupuka kuutaka ubunge kupitia jimbo la Kinondoni na kuwa ataendeleza sanaa hata akiwa mbunge.

Steve Nyerere Amesema Haya.’Kwanza ninataka kuwahakikishia watanzania sijakurupuka, nimekuwa  mwanachama wa chama cha Mapinduzi  umoja wa vijana almost miaka 25 na sasa hivi nina miaka 29 naelekea 30 lakini vilevile nimekuwa kamanda wa vijana miaka 10 tawi la bwani kinondoni, nimekuwa mwamasishaji  wa chama cha mapinduzi kitaifa kwa muda wa miaka 10

Kwa hiyo nataka kusema sijakurupuka na wala sijatamkia sifa kwasababu labda nimeona mtu Fulani amegombea na mimi basi tu  nigombee hapana  nimeona  katika wilaya yangu ya  kinondoni kuna matatizo kadhaa  nani anaweza kuyatetea hayo matatiizo  basi mimi ndio nitakuwa mtetezi wa wilaya wa Kinondoni pamoja na matatizo ya wasanii wetu, kuhusu kazi zangu za filamu nitakuwa nafanya kama kawaida huku nikiwa natumikia kazi za Bungeni’alisema

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad