Tuzo za Muziki za Kili 2015, Jumamosi ya wiki iliyopita zilitimua vumbi kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Mwenge jijini Dar es Salaam ambapo maelfu ya Watanzania wanaopenda burudani walikuwa wakifuatilia mwenendo mzima wa tuzo hizo, ambapo msanii Ali Kiba aling’ara baada ya kunyakua tuzo tano na kumuacha mbali hasimu wake mkubwa, Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’ aliyeambulia tuzo mbili tu.
Mpango mzima ulianza, mishale ya saa tatu za usiku ambapo wasanii pamoja na wadau mbalimbali walijumuika kwenye zulia jekundu na kupiga ‘mapichapicha’ ya ukumbusho kabla ya mchakato wa kutoa tuzo haujaanza.
Baada ya hapo, pazia la burudani lilifunguliwa na msanii chipukizi, Ruby anayetamba na ngoma yake ya Na Yule, akafuatiwa na Ommy Dimpoz, baadaye akapanda jukwaani Barnaba Elias sambamba na Vanessa Mdee, akapanda Christian Bella kisha Weusi wakiongozwa na Joh Makini na Nikki II wakafunga pazia la burudani kwa kukamua ile mbaya.
ALI KIBA ANG’ARA
Ali Kiba.
Baadaye ulifuatia mchakato wa kutoa tuzo ambapo msanii Ali Kiba, alizoa tuzo tano; Mtumbuizaji Bora wa Mwaka, Wimbo Bora wa Mwaka (Mwana), Mtunzi Bora wa Mwaka (Bongo Fleva), Wimbo Bora wa Afro (Mwana) na Mwimbaji Bora wa Kiume (Bongo Fleva) huku hasimu wake Diamond Platinumz akiambulia tuzo mbili tu; Wimbo Bora wa Zouk/ Rhumba (Nitampata Wapi) na Video Bora ya Muziki ya Mwaka (MdogoMdogo).
KILICHOMPONZA DIAMOND NI HIKI
Kutokana na matokeo hayo, inaelezwa kuwa kilichomponza msanii Diamond Platinumz ni ujumbe wake aliowahi kuutuma kwenye mitandao ya kijamii, akiziponda Tuzo za Kili kwamba hazizingatii vigezo, kwa kuwaacha wasanii wanaofanya vyema kwenye tasnia ya muziki na badala yake, ‘kuwapendelea’ baadhi ya wasanii kutokana na sababu binafsi za waandaaji.
“Unajua Diamond alikosea sana kuziponda Tuzo za Kili kwa sababu ndizo zilizompaisha mwaka jana, matokeo yake amempa nafasi mpinzani wake, Ali Kiba kung’ara kwa kunyakua tuzo kibao, nafikiri atakuwa amejifunza jambo,” alisema Bruno Sanga, mmoja kati ya wadau waliohudhuria utoaji wa tuzo hizo.
WASHINDI WENGINE
Ukiachilia mbali Ali Kiba na Diamond, wengine walioziteka tuzo hizo ni mwanadada Vanesssa Mdee aliyenyakua tuzo mbili; Mtumbuizaji Bora wa Mwaka (Kike) na Mwimbaji Bora wa Kike (Bongo Fleva), Mzee Yusuph; Mwimbaji Bora wa Kiume Taarab, Mtunzi Bora wa Mwaka (Taarab) na Kundi Bora la Taarab (Jahazi).
Wengine ni Jose Mara aliyenyakua tuzo mbili, Isha Mashauzi, Joh Makini, Baraka Da Prince (Msanii Bora Chipukizi), Nahreel (Mtayarishaji Bora wa Mwaka) na Mrisho Mpoto aliyeondoka na Tuzo ya Wimbo Bora Wenye Vionjo vya Asili (Waite).
Sauti Sol walinyakua Tuzo ya Wimbo Bora wa Afrika Mashariki (Sura Yako), Profesa Jay (Wimbo Bora wa Hip Hop - Kipi Sijasikia), Jux (Wimbo Bora wa R&B- Sisikii) na Wimbo Bora wa Bendi wa Kiswahili iliyokwenda kwa FM Academia (Vijana wa Ngwasuma) na Bendi Bora ya Mwaka (FM Academia) huku Yamoto Band wakinyakua tuzo ya Kikundi Bora cha Mwaka (Bongo Fleva).
GPL
Kilicho Mponza DIAMOND PLATNUMZ Tuzo za Kill Music Hichi Hapa, Wema na Jokate Watambiana Mabwana, Vanessa na Jux Wapakatana
10
June 15, 2015
Tags
MWANDISHI KUWA MUELEWA ALICHOKISEMA DANGOTE NI UKWELI MTU .TUZO HIZI NI UBABAISHAJI ILA KWA KUWA WEWE SIO MUELEWA UNAMKOSOA DANGOTE KWA SABABU ZAKO BINAFSI.KUNA WANAMUZIKI WENGI WALIOFANYA VIZULI MWAKA HUU LAKINI WAMEWEKWA KANDO SIJUI KWA VIGEZO GANI.MIMI NAZANI WAANDAAJI HAWANA ELIMU YA KUTOSHA YA KUANDAA TUZO,WANAKULUPUKA TU.CHA MUHIMU NI KWENDA KUJIFUNZA NCHI ZINGINE WANAFANYAJE.WATU WENYE AKILI ZAO HAWAKUPIGA KURA NAAMINI ILA WASIOELEWA MTU MMJA ANAPIGA KURA MARA MIA MOJA NI UPUUZI MTUPU.NIMESOMA KAMPENI YA KUMPIGIA KURA DAVIDO AMWANGUSHE DANGOTE HII INA LETA PICHA GANI KWA WATANZANIA?NIMEAMINI SIKU ZOTE UKIWA NA MAFANIKIO MAADUI WANAKUWA WENGI.
ReplyDeletedomo anapenda misifa, kwanza nimeshangaa mwimbo wake wa ntampata wapi alishindaje mbele ya wimbo wa christian bela "nani kama mamaaa"?
ReplyDeleteKili Award ni tuzo kwa wasanii wasiofanya vizuri kama Ali Kiba. Yeye ni kama amepozwa kwani hakuna alichokifanya mwaka huu zaidi ya kuimba utumbo
ReplyDeletekama KILI AWARD NI kwa wasanii wasiofanya vizuri ina maana hata Diamond alivyochukua mwaka jana naye alipozwa hafanyi vizuri maana wale pia walikuwa ni KILI AWARDS na wala sio SERENGETI AWARDS
DeleteSasa domo nae anamafanikio gan kina mengi wasemeje achen kumpaishaa mbona ye mwaka jana kachukua hta hiyo ya mtunzi bora hmkusema au ndo vile mnaona ya wengne yenu mmeyakalia ......apite hivi dharau zitammaliza huyo domo anajiona sana
ReplyDeleteDangote kilichomponza asishinde ni dharau na maneno ya kashfa kwa wenzie. Kwa mfano kuwa kuwaita joket na wema ni makombo, wakati yeye ndio kachukua makombo
ReplyDeleteHa ha ha udaku bwana.
ReplyDeleteSasa hapo hiyo habari ya jokate na wema kutambiana mabwana iko wapi?
Jux na vanessa kupakatana ikwapi?
Acheni uboya.
Mimi naona kuwa siyo haki tuwe na muimbaji mmoja Tanzania yaani Diamond ni jambo la busara tuwe nao wengi kwa mfano safari hii amepewa Ali kiba thst is fine next time apewe Barnaba au Bella that is how should be.
ReplyDeleteMimi naona kuwa siyo haki tuwe na muimbaji mmoja Tanzania yaani Diamond ni jambo la busara tuwe nao wengi kwa mfano safari hii amepewa Ali kiba thst is fine next time apewe Barnaba au Bella that is how should be.
ReplyDeletePeople acheni ushabiki.......semeni yote but mwisho wa siku u got 2 respect diamond kwa kile alichofanya kwnye bongo fleva hadi sasa
ReplyDelete