Kumbe Gari la WEMA SEPETU Kimeo..Ni Lile Alilozawadiwa Kwenye Siku ya Kuzaliwa..Sasa ni Spana Mkononi

Musa mateja
NInoma! Kumbe lile gari la kifahari aina ya BMW ambalo muigizaji nyota wa filamu Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ alizawadiwa wakati wa bethidei yake na kuwa miongoni mwa sababu za kumwagana na mpenzi wake wa awali, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ mwaka jana, linadaiwa kuwa kimeo kwa vile limekuwa likiharibika mara kwa mara, Amani lina stori kamili.

Mapema wiki hii, paparazi wetu alikuta gari hilo likiwa limebuma mitaa ya Victoria, Kijitonyama jijini Dar es Salaam huku mshindi huyo wa Shindano la Miss Tanzania mwaka 2006 akiwa ndani, lakini ili kukwepa aibu, aligoma kutoka nje kuomba msaada, badala yake akabakia ndani huku akijaribu kuwasiliana na watu wake wa karibu.

Mmoja wa wasaidizi wake wa karibu, Petit Man baadaye akitumia gari jingine alifika eneo hilo akiwa ameambatana na fundi, ambao walilisukuma hadi eneo salama na kuliegesha. Wema alibakia ndani ya gari hilo wakati fundi akijaribu kurekebisha dosari ambayo haikuweza kufahamika mara moja.


Hadi gazeti hili linaondoka eneo hilo baada ya juhudi za kumpata ili azungumze kugonga mwamba, hakukuwa na dalili za kupatikana kwa ufumbuzi.Mtu wa karibu na Madam aliliambia gazeti hili kuwa gari hilo limekuwa likimsumbua kwa muda mrefu kiasi kwamba wakati mwingine hulikumbuka gari aina ya Nissan Murano, ambalo alipewa na Diamond siku hiyohiyo ya bethidei yake, lakini akaliuza baada ya wawili hao kutofautiana.

Baadaye Wema alitafutwa kupitia simu yake ya mkononi, lakini haikuweza kupatikana ili azungumzie juu ya gari hilo, ingawa siku za nyuma wakati gari hilo lilipokutwa likiwa limetolewa matairi eneo la Komakoma, alimwambia mwandishi wa habari hizi kuwa anahisi BMW hilo lilikuwa limetumika sana kabla ya kupewa kwa vile limekuwa likimsumbua mara kwa mara.
GPL

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mwee ushamba mzigo jamani, hivi na mvua na mafuriko ya Dar, barabara zote zilijaa maji, magari yalikuwa yanapita kwenye maji, magari mengi yanahitaji kufanyiwa service sasa hivi. Mie lishanizimikia zaidi ya mara 3 kwa siku moja, kumbe ni mimaji iliyokuwa inaleta shida.

    Haya semeni jingine, maana kuhusu magari kuzimika barabarani na kuhitaji kufanyiwa service au hata kubadilisha matairi, na spare nyingine kama break ni vitu vya kawaida sana unless uwe unaendesha TZ 11 kwa sababu hata baiskeli, Pikipiki na Bajaj zote hufanyiwa service pia.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad