Mchezaji Yaya Toure Afanya Maamuzi Magumu

Uongozi wa klabu ya Man city umefanikiwa katika suala la kumshawishi kiungo kutoka nchini Ivory Coast, Yaya Toure aliyekua mbioni kutimka klabuni hapo mara baada ya msimu wa 2014-15 kufikia kikomo.

Juma lililopita uongozi wa Man City ulitangaza kupingana na hatua za kiungo huyo kuwa katika mipango ya kutaka kuondoka klabuni hapo na kwenda kusaka mahala pengine pa kucheza soka lake.

Toure amethibitisha kuendelea kubaki Etihad Stadium, baada ya kuandika katika mitandao ya kijamii, na kupokelea vyema na mashabiki wake waliouona ujumbe huo.

Naye wakala wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 32, Dimitry Seluk amethibitisha taarifa hizo, baada ya kuulizwa na vyombo vya habari ambavyo vilihitaji kujua ukweli wa taarifa zilizotolewa na Toure.

Seluk alitangaza kuanza mchakato wa kumtafutia klabu nyingine mchezaji wake majuma matatu yaliyopita, huku akitoa sababu za hali ya kutoelewana baina ya Toure na baadhi ya viongozi wa Man City ambao walimuonyesha dharau mwaishoni mwa msimu uliopita kwa kushindwa kumtakia kheri kwenye siku yake ya kuzaliwa.

Tayari klabu ya Inter Milan ya nchini Italia pamoja na Chelsea ya England zilikua zinahusishwa na mipango ya kutaka kumsajili kiungo huyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad