Meseji ya Mapenzi Kutoka Wrong Number Imenivurugia Ndoa Yangu


Meseji ya Mapenzi Kutoka Wrong Number Imenivurugia Ndoa Yangu

Jamani, mwenzenu nimevurugwa mpaka nimevurugika, Jana nilirudi kutoka job nimechoka sana. Na ninapolala huwa sipendi kukaa na simu kitandani kwa kujua ina madhara kiafya. Ila niliweka mlio wa vibration kwa sababu sipendi makelele ya simu ninapokuwa nimelala. Ilipofika mida ya saa nne na nusu au tano kasoro, simu ikavibrate. Mke wangu akanishtua kuwa simu yangu inaita. Basi kwa sababu ya uchovu sikutaka kuamka, nikamwambia aniletee. Aliponiletea akawa amefungua na kuona kuna sms imeingia. Akaisoma. Sikuona tabu maana siku zote huwa anachukuaga tuu simu yangu na anaweza kukaa nayo kadiri aonavyo yeye, na akipenda anapitia whattsapp au sms inbox au kucheza games kwa uhuru bila tatizo lolote.

Sasa jana Message iliyoingia ni ya kimapenzi kutoka kwa new number sms yenyewe inasema,

"Nimelala mpenzi wangu, naamini na wewe pia umelala, uniote umenikumbatia, si unaona baridi hii? I wish ungekuwa hapa jamani leo nina hamu ile mbaya..." Ghafla mke wangu anabadilika sura na maongezi. Nikarushiwa maswali yaliyojaa ghadhabu kama mvua ya mawe. Nikaiomba nione kucheki namba mpya, daaah nikapigwa butwaa. Nikasema isiwe tabu, ngoja tuende tigopesa tujaribu kama tunatuma pesa ili tujue jina. Kweli tulipata jina, wala hata silijui la wapi, nikaona isiwe tabu, ngoja nimpigie nimwulize. Mara wife akanyang'anya simu apige yeye mwenyewe. Ilivyopokelewa tuu yaani hata mtu upande wa pili hajajitambulisha vizuri kashushiwa mvua ya matusi, vijembe na vitisho kibao. Honestly nilipanic sana. Heri ingekuwa ni mtu ninayemfahamu au ni mchepuko wangu ningejisikia guilty. Lakini ukweli simfahamu huyi mtu.

Baada ya kukata simu, nikageuziwa mashitaka, kuwa namfahamu ila nimefanya makusudi kutokusev namba, na huyo mwanamke anajifanya kakosea ili kuepuka zali. Daah nikajieleza nijitetee lakini wapi, hapakukalika wala kulalika. Tumeamka asubuhi vurugu mechi, sasa nikipiga ile namba hapokei tena sijui ni woga wa kutukanwa. Jamani hebu vaeni kiatu changu alafu mnishauri nifanyeje mwenzangu anielewe? Mpaka sasa sijajua huyo aliyetuma sms yuko wapi? ila nimechukua tuu namba na jina lililosajiliwa nalo kwenye tigo pesa.

Sijawahi kupata zali kama hili

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mwanaume halisi hafundishwi namna ya kumhandle mkewe. Usiwe bwege ongeza sauti iwe ya kiume zaidi ataelewa tu Acha kulia lia mambo madogo hayo.

    ReplyDelete
  2. Nipe hiyo namba mimi nimpigie huyo demu..

    ReplyDelete
  3. ina maana umezidiwa sauti na mkeo?hayo c mambo ya kuomba ushauri ni madogo sana,kama hataki kukuelewa timua.na kwa nini unamruhusu mkeo atawale simu yako?huo ni uzumbukuku...!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad