Watu watatu wamefariki wawili kati yao wanasadikiwa kuwa ni wafuasi wa Al Shabaab katika mapigano baina yao na jeshi la Polisi.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro amesema tukio hilo limetokea eneo la mpakani mwa mkoa wa Morogoro wilaya ya Mvomero na mkoa wa Tanga ambapo watu hao walikuwa wamejificha msituni.
Amesema jeshi hilo linawashikilia watu sita kwa kuhusika na tukio hilo, na kwamba uchunguzi zaidi unafanyika ikiwa ni pamoja na msako mkali katika eneo hilo.
Taarifa kutoka katika hospitali ya mission ya Turian mkoani Morogoro zinasema kuwa maiti tatu zimehifadhiwa hapo ambapo kati ya hizo,maiti mbili zinaonekana kuwa ni za watu wasio raia wa Tanzania huku moja ikiwa ni ya mtu ambaye alijeruhiwa vibaya na badaye kufariki akiwa hospitalini hapo.
MYTAKE: Hivi hawa ni alshabab kweli au kutishana tu au jeshi letu linataka sifa?
Morogoro: Watu watatu wafariki katika mapambano na Polisi, wawili wanasadikiwa kuwa Al Shabaab..Wengine 50 wanasakwa
3
June 27, 2015
Tags
Uchaguzi huo
ReplyDeletebado hawajakutana nao, acha wajifanyie tu hayo maigizo
ReplyDeleteMASIKINI TANZANIA TUMERUDI ENZI YA NYERERE, HABARI ZOTE ILIKUWA LAZIMA ZIKACHJWE, ZIPIGWE POLISH NDIYO ZIRUSHWE HEWANI... SASA LEO NA NYIE MNAOGOPA HATA KUPUBLISH COMMENTS ZA WASOMAJI WENU.. mweee
ReplyDelete