Mrembo FAIZA ALLY Awaomba Radhi Watanzania......

Imelda Mtema
MZAZI mwenzake na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ Faiza Ally, hivi karibuni katika tuzo za KTMA aliwaacha watu midomo wazi baada ya kutinga na kivazi kilichoacha sehemu kubwa ya makalio yake nje na kuzua minong’ono katika mitandao ya kijamii.

Akizungumza na Amani kwa kuonekana kujutia kitendo kilichotokea, Faiza alisema kuwa ile nguo aliishona ikiwa imeziba sehemu yote ya nyuma japokuwa ilikuwa imechanwachanwa lakini hakuwa na nia ya kuacha sehemu ya makalio yake nje.

Akiendelea kuzungumza alisema kuwa, siku alipokuwa akienda kwenye tuzo alikuwa peke yake kwenye gari hivyo alivyoinuka ndiyo ile nguo ikapanda bila kufahamu.“Jamani siwezi hata siku moja kujiachia hivyo naomba Watanzania wanisamehe,” alisema.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwa mwonekano tu wa hyo nguo yaonekana ni style yake kwani sio kama imepanda juu wala nn hapo ilipo kaa ndio mahala pake na kuvaa nguo hizo sio mara ya kwanza hyo misama tushachoka ss kikubwa ww mwenyewe jitambue na ubadilike!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad