Mzee Majuto Amuunga Mkono Wema Sepetu, Diamond Amtaka Wema Abadilike Kama Kweli Anautaka Ubunge

Mzee Majuto  kwa mara ya kwanza ameamua kufunguka kumuunga mkono Wema Sepetu kwa nia yake ya kutaka kuwa mbunge.Kupitia ukurasa wake mtandaoni, Mzee Majuto ameandika;

Nisingependa kuyaongea haya kwenye mfungu mtukufu ila kiundani ningependa kuonyesha umoja na kumuunga mkono wazo na lengo la Mwanangu kwa kuwa anaweza na amethubutu sasa isitokee wale wasiopenda maendeleo ya watu na taifa hili kuvuruga misingi na mipango madhubuti ya kuwapa nafasi vijana na hasa wanawake kushika hatamu na kuleta mabadiliko.Kapeleke mabadiliko Singida na Tanzania nzima.

Muhimu ni kuwa na juhudi uwezo imani pamoja na uzalendo. Ujumbe huu pia ni kwa kila kijana na mwanamke mwenye lengo na nia ya udhubutu. Inshallah. Ramadhan Maqbul Waislam wote. Mzee Majuto alimaliza na kumtag Wema.

Moja kati ya waliochangia kwenye andiko hili la Mzee Majuto, ni Diamond Platnumz ambaye alimtaka Wema abadilike kama kweli anautaka ubunge.


  • “Swala siyo watu kumvunja moyo ,..ila yeye abadilishe akili ya mambo ya kushabiki migogoro ya watu wengine mitandaoni aache..katia aibu sana jana ,katangaza ubunge na bado ana shadadia ugomvi wa Diamond na Davido ,...mbunge ndo wakuwa na akili hii kweli,...watu wanahasira na upuuzi unaofanya na team yake na bado yeye mwenyewe anachochea ...watu watamuachaje....abadilike kama kweli anataka kugombea ubunge”


Wewe mdau unakipi cha kusema hapa.

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hana mpya huyo Diamond yeye kamuona Wema tu ndio au tatizo nyotaaa? Mbona mashabiki wa Ali Kiba, wa Jokate na watu wengine ambao sio mashabiki wa mtu yeyote yule ila hawapendi tabia yake ya kudhalilisha wanawake hawampigii kura hawasemi anamuona Wema tu? Asitafute kumfanya Wema kuwa ni kisingizio cha kuanguka kwake, ni yeye mwenyewe na kuropokwa ropokwa kwake hovyo, mtu mzima anakuwa kama Taifa Stars visingizio kila siku.

    Kiufupi na kiutathmini Diamond huwezi kumshinda Davido labda wakupe tu na wewe za upendeleo kama ulivyodai wenzio hawakustahili walipendelewa, na huko MTV labda wakupendelee tu lakini huwezi kumshinda huyo hata bila kupigiwa kura na Wabongo wenzio.

    ReplyDelete
  2. Tena aende akatafute kura za Kinternational wao si matawi ya juu kura za makapuku wanazitaka za nini? Hvi hawa watu wamesahau walivyoiba 3000, 3000 za watu wakati wa White Party? Dogo anajisahau sana siku hizi unajiona umefika ngoja ufike ndio ufanye mashauzi safari bado ndefu watakufanya kama Kikulacho, kuku kapanda baiskeli bata kavaa raizon.

    ReplyDelete
    Replies
    1. huna lolote potelea kule chiziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii wewe

      Delete
  3. acheni ujinga kumshauri mtu siyo kosa. pumbavu zenu

    ReplyDelete
  4. KWA HUYU POVU ZITAWATOKA SANA MIAKA MIA NIMSANII MWENYEMAENDELEO KULIKO WOOOTE ALMAS MWACHENI JAMANI. HUYO WEMA HATA NYUMBA HANA ANAPANGA ANATAKA UBUNGE PESA ZOTE KWENYE STAREHE DAH KWELI KAMA ANATAKA ABADILIKE

    ReplyDelete
  5. Mliotoa comments hamjanikeraa

    ReplyDelete
  6. wema heshimu sana mawazo yako uko sahihi sana dada ila nnakusihi kua makini nawatu wanao kushauri wasije kukupoteza

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad