Nasumbuliwa Sana na Mademu Japo Nimemtangaza Mpenzi Wangu Hadharani -Aslay

Mwanamuziki Aslay Isihaka kutoka katika kundi la Yamoto Band amefunguka na kuweka wazi kuwa anasumbuliwa sana na watoto wa kike ndiyo maana ameamua kuweka mahusiano yake wazi, Aslay alifunguka hayo alipokuwa

akichat Live katika kipengele cha Kikaangoni Live kinachofanyika kila siku ya Jumatano, kuanzia saa nane mchana mpaka kumi Alasiri kupitia ukurasa wa facebook wa EATV.
Aslay alisema kuwa moja ya sababu iliyomfanya kumuweka wazi mpenzi wake huyo ni kutaka kutoa ujumbe kwa wale ambao wanamsumbua kuwa waache kufanya hivyo kwani tayari ana mtu ambae yeye anampenda.
"Nimeamua kuweka mahusiano yangu ya mapenzi wazi sababu nasumbuliwa sana, nahisi kufanya hivyo wataelewa na kuacha, yaani kama nimewapunguzia speed ya usumbufu"
Mbali na hilo Aslay aliweza kuzungumzia juu ya elimu yake na kusema hakuacha shule kwa sababu ya muziki ila ataendelea na shule pale alipoishia, ilaa anaamini atafanya hivyo siku za usoni.
YAMOTO BAND
Mkali huyo ambaye amejipa jina la dingi mtoto amesema kuwa hafikiri kuondoka Yamoto band wala hawazi suala hilo, ila amesema kuwa kwa sasa yeye na wenzake wanajipanga kufanya kazi za kimataifa hivyo wanasubiri majibu kutoka kwa Yemi Alade, kwa kazi ambayo wamemtumia hivyo pia ameeleza kuwa kuna kazi ambayo wamefanya na Sauti Soul wa nchini Kenya ambao waliwaomba kufanya nao kazi.
MAHUSIANO YAKE NA WEMA
Tetesi zilizopo mtaani ni kwamba Aslay Isihaka alikuwa akifukuziwa na Wema Sepetu kimapenzi na watu wengi walipouliza swali walitaka kufahamu ukweli juu ya suala hilo na ndipo hapo Aslay alipofunguka na kuweka wazi juu ya suala hilo na kusema kuwa hakuna ukweli wowote na wimbo wa Nitakupwelepweta hajaimbiwa Wema Sepetu.
"Watu wanakuwa wanaongea mambo mengi juu ya maisha yangu hususani katika mahusiano na kusambaza taarifa zisizo na ukweli, mfano watu wanasema natoka kimapenzi na Wema huo siyo ukweli kabisaa bali Wema ni kama dada yangu, ila kutokana na mambo haya ndipo niliamua kuweka mahusiano yangu wazi ili kila mtu ajue kuwa nipo kwenye mahusiano na mtu fulani na waache kusambaza taarifa zisizo na ukweli."
Kwa kifupi hizo taarifa wanazosema mashabiki hazina ukweli wowote,kwa sasa nimemtangaza mpenzi wangu na ndiye niko nae, sitaki usumbufu tena kwa sasa.

Tanzania Hottest Celebrity Gossip News

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Dogo hiyo ndiyo price ya kuwa maarufu kuna siku usipo take care utatumbukia tu na hao madada wanaokusumbua kwani kuweka hadharani kuwa tayari una mpenzi wako hiyo siyo tiba kabisa kwa hao madada wanaokufuzia sasa hapo ndiyo jus'the otherway aroun'umewaongezea speed double ili siku waje wampiku huyo mpenzi wako uliyenaye sasa hivi duh pole sana dogo no way out na hao madada wa kibongo walivyoumbika ah kwishnei utakwama tu one day goodluck dogo

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad