Sugu Amfikisha Mkewe Kortini..Kisa Kuvaa Nusu Utupu na Kupiga Picha za AIBU

KINDUMBWENDUMBWE! Mbunge wa Mbeya Mjini kwa ‘leseni’ ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Osmund Mbilinyi ‘Sugu’ amemfikisha kortini aliyekuwa mkewe,  Faiza Ally akitaka apewe mtoto wao, Shaa (2) ili amlee kwa vile mama yake huyo si mwadilifu.

Aliyekuwa mkewe na mbunge wa mbeya mjini Joseph Osmund Mbilinyi ‘Sugu’,  Faiza Ally akiwa katika pozi.

Ijumaa iliyopita, saa 2:00 asubuhi, Faiza alipanda kwenye kizimba cha Mahakama ya Mwanzo, Manzese/ Sinza iliyopo Sinza-Makaburini jijini Dar kwa ajili ya kukabiliana na madai hayo.

 Alieyekuwa mke wa mbunge wa mbeya mjini Joseph Mbilinyi "Sugu" akiingia mahakamani.

ZILIPO HASIRA ZA SUGU

Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichomwaga ‘ubuyu’ huo, Mheshimiwa Sugu alifikia hatua hiyo baada ya kuchukizwa na tabia mbaya za mwanamke huyo hasa ya kuvaa nguo zinazomuacha nusu utupu na kupiga picha za aibu, akiamini kuwa, tabia hizo zinaweza kuathiri makuzi ya mtoto huyo.

Mnyetishaji huyo aliendelea kusema kuwa, kwa kipindi kirefu, Sugu amekuwa akimvumilia Faiza, lakini hivi karibuni uzalendo ulimshinda baada ya picha zake akiwa amevaa kigauni kifupi na makalio nje kusambaa mitandaoni.

PALIPOKOLEZEA HASIRA

Faiza alivaa kivazi hicho hivi karibuni kwenye hafla ya ugawaji wa Tuzo za Kili Music iliyofanyika Ukumbi wa Mlimani City, Dar.

 SUGU MBELE YA HAKIMU

Akizungumza mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo, Patrick Vaginga, Mheshimiwa Sugu alidai kuwa mbali na mzazi mwenzake huyo kuwa na tabia ya kuvaa nusu utupu pia ana mtindo wa kupiga picha zisizo na maadili na kuziweka mtandaoni yeye mwenyewe.

 Joseph Mbilinyi akionekana kwa mbali katika maeneo ya mahakama.

KUHUSU MTOTO

Sugu alikwenda mbele zaidi kwa kudai kwamba, pia mwanamke huyo amekuwa na tabia ya kumpiga picha mbaya mtoto wao na kuzimimina humohumo mitandaoni jambo ambalo alisema linamharibu mtoto huyo.

 FAIZA HANA PESA

Mbali na sababu hizo, pia Sugu aliongeza kuwa, Faiza hana kipato kizuri cha kuweza kumlea mtoto na mara kwa mara amekuwa akisafiri jambo ambalo husababisha mtoto huyo kutopata malezi ya mama kwa muda mrefu hivyo kuiomba mahakama impe haki yeye ya kuishi na mwanaye.

 FAIZA AJIBU MAPIGO

Naye Faiza akijibu mapigo katika utetezi wake alisema kuwa, Sugu hafai kumlea mtoto huyo kwa sababu naye ana tabia ya kusafiri kwa muda mrefu hivyo kuishi mbali na mtoto ambapo aliiomba mahakama hiyo isimruhusu baba mzazi huyo kuishi na mtoto kwa kuwa atamharibu.

KESI YAPIGWA KALENDA

Mheshimiwa Hakimu Vaginga akasema kwa vile kesi hiyo ndiyo imeanza kusikilizwa kwa mara ya kwanza aliiahirisha hadi baadaye mwezi huu ambapo hukumu itatolewa.

 SUGU NJIA YAKE, FAIZA NJIA YAKE

Ijumaa Wikienda lililokuwa mahakamani hapo, liliwashuhudia wazazi hao, kila mmoja akiondoka na njia yake.

KWA NINI FAIZA NI MKE WA SUGU?

Kwa sheria za Kitanzania, mwanamke na mwanaume wakiishi pamoja kwa zaidi ya miezi sita, hao tayari ni mke na mume kama ilivyokuwa kwa Faiza na Sugu ambao waliishi pamoja kwa zaidi ya miaka miwili.
GPL

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hakuna sheria Tanzania inayosema watu wakiishi pamoja kwa miezi sita basi wanatambulika kama mke na Mume. Bali kuna sheria inatambua kitu kinaitwa dhana ya ndoa (Presumption of marriage) pale mtu na mpenzi wake wanapoishi pamoja miaka 5 au zaidi kama mke na mume n sio miezi 6. Hata hivyo kuna vigezo vya kutimizwa ili dhana iyo iweze kufanya kazi. So wewe kama mwanahabari hakikisha unaandika kitu ambacho una uhakika nacho. Msipende vitu vya kukopi na kupaste vitakuja kuwaletea matatizo huko mbeleni kwa kuwapotosha watu.

    ReplyDelete
  2. Hao ni PIPA na MFUNIKO!!

    ReplyDelete
  3. Sasa na hapo aweke kiburi chake, mtoto kesha chukuliwa sasa yuko friiiii kujiuza atakavyo. Machozi ya mamba kwa Soud Brown hayatamsaidia kaharibu mwenyewe.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad