Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu) ameshinda kesi aliyomfungulia aliyewahi kuwa mchumba wake Faiza Ally ambaye pia ni mama wa mtoto wake wa kike aitwaye Sasha.
Kwa mujibu wa maelezo ya Faiza kupitia akaunti yake ya Instagram, mahakama imetoa hukumu ambayo ni mtoto achukuliwe na kulelewa na baba yake mzazi.
Sugu alimshitaki Faiza kwa madai kuwa hana maadili na ana hofia kuwa atamharibu mtoto wao, hivyo alitaka kumchukua mtoto kutoka kwa mama yake aishi naye.
Hiki ndicho amekiandika Faiza baada ya hukumu kutolewa:
“Sielewi Joseph ameshindaje kesi- ushahidi wa picha peke yake sioni kama unatosha mimi kupokonywa mtoto wangu,mtoto wangu ni mdogo sana ananihitaji sana, na sita rudi hata ikibidi kuuza kila nilicho nacho kwa ajili ya kusimamia hili.
"Sijapewa nafasi nimepelekwa mahakamani ijumaa na leo jumanne nimepewa hukumu/ mwanangu achukuliwe….. hapana ! sitarudi nyuma na haitakua rahisi ninakata rufaa na kutafuta wakili wa kunisimamia hili.
"Mwanangu anasoma vizuri anaishi vizuri na naamini kwenye mikono yangu yuko salama zaidi ya kokote/ yaani kuhusu kukosa kukaa na mwanangu ni bora kufa kuliko kuishi nikimuona sasha ana lelewa na mama mwingine ikiwa mimi mama yake niko hai na makini katika malezi ya mtoto wangu.
"Nina ndoto na mwanangu nyingi sana , nahitaji kuishi nae yeye ndio kila kitu kwenye maisha yangu/ nampenda sana mwanangu na sijashindwa kumlea.
"Naona uchungu sana kupelekwa mahakamani na kupokonywa mtoto wangu bila sababu za msingi .
"Sitaogopa cheo chake cha ubunge kamwe ntasimama kama mama mwenye haki kwa mtoto wake …mungu naomba nielekeze.nisimamie na unihukumie huu ukatili ninao fanyiwa na baba sasha …..”
Sugu ashinda kesi dhidi ya mama mtoto wake Faiza, mahakama yaamua apewe mtoto
11
June 24, 2015
Tags
MMM!!!!
ReplyDeletepole sana lakini mm km baba pia nisingependa mwanangu alelewe na mama ambae haoni aibu kutembea nusu uchi mbele zawatu mtoto umleavyo ndio akuavyo.kaachini badilitabia kisha nendakadai mwanao
ReplyDeleteUmenena ndugu yangu huyu dada atasababisha mtoto kuwa chokoraaaa
DeleteBORA KACHUKUWA MWANAE BWANA, MAAANA MAMA HAJITAMBUI KBISA NA MTOTO ANAKUWA ANAONA VITIMBWI VYA CHIZ MAMA YAKE
ReplyDeleteMtoto bado mdogo anamuitaji mama yake sio mama wa kambo, kwa hili hmmm hapana angeonywa tuu!!! kwa mara ya kwanza, akirudia labda, sio jukumu la kumtenganisha mtoto na mama yake, bado mdogo, sasha anamuitaji mama yake kwa sasa sio baba yake au mama wa kambo
ReplyDelete
DeleteTumeshamuonya sana Faiza kwa tabia alizokuwa anaonyesha,sanasana tumeishia kutukanwa,na kama wewe ni wa mitandao basi nadhani umeona jinsi alivyokuwa anajibu utumbo.Kweli mtoto mdogo bado kuishi mbali na mamake lakini si kwa huyu mwanamke.
Big up SUGU, umefanya jambo la maana sana, huyo mwanamke hajitambui. Eti anaomba Mungu amsimamie! yani Mungu akusimamie ukamharibu mtoto? Mungu amekupa mtoto badala ya kumlea kwa heshima unamvalia nusu uchi alafu unasema eti namlea vizuri. Aibuuuuuuuuuuuuuuuuuuu. Hongera tena Sugu.
ReplyDeletefaiza huwezi kulea chochote acha mtoto akapate maadili akiona picha zako ukubwani atajiua
ReplyDeleteaibu gani mama wa mtu kujiacha hivo bora achukulliwe inshallah ushindwe kesi
kwanza kabisa Hongera Sugu kwa ujasiri ulioonyesha wa kukomboa maisha ya mtoto wenu toka kwa mama yake aliyekwisha poteza dira na mwelekeo wa kimalezi na kimaadili kwa ujumla. Bila shaka yoyote hakuna kitu chochote kizuri ambacho Sasha angerithi toka kwa mama yake zaidi ya tabia zake za kishenzi na kihuni za kukaa uchi na kujinadi kama bidhaa zilizomwagwa mnadani. lawama za mama Sasha ni sawa na maneno ya mkosaji huwa haishi kutapatapa. Tena sikio la kuwa huwa halisiki dawa kama ni kuonywa kaonywa mara ngapi dhidi ya hizo tabia zake? Naimani kubwa sana Sasha atapata malezi stahiki toka kwako Sugu wapo wengi waliokumbwa na mikasa kama huo wako ila usife moyo endelea kuthubutu zaidi kama ulivyoweza kumnusuru Sasha toka kwa mama yake aliyechanganyikiwa. Faiza muogope Mungu wako tena kumbuka Mungu hamna ushirika na watu wadhambi wasiojiheshimu na wapumbavu. Tulikuonya sana lakini shukrani yako iligeuka kuwa matusi na kutuita sisi wapumbavu. Sasa ndo naamini kweli mpumbavu huwa haelewi anachofanya hata akielekezwa, neno mpumbavu unapenda kulitumia pasipo kujua maana yake kweli wewe ni mpumbavu uliyetukuka. Haiwezekani Sasha ategemee malezi bora toka kwa mama ambaye ni mpumbavu ngoja mzazi mwezako akusaidie malezi ni dhahili yamekushinda hata yeye pia ni mzazi ana haki zote za kumlea mtoto wenu hasa pale inapothibitika kuwa malezi yanayostahiki kwa mtoto hayapatikani kwa mmoja wa mzazi anayeishi naye. Siku zote mti hujulikana kwa matunda yake vilevile mtu hutambulika kwa matendo yake. Haiwezekani kutegemea mema toka kwa mtu mwovu ni sawa na kutegemea kuvuna zabibu toka katika mmea wa bangi. Faiza kama unataka urudishiwe Sasha umlee kwanza badilika kimatendo na kitabia na hili linahitaji muda si suala la leo au kesho kutwa sasa una kazi ya kuonyesha jamii kuwa umebadilika hayo malumbano yako hayatakusaidia chochote muda ndio hu kuonyesha kuwa wewe ni mtu mwema na si yule waliomzoea mwanzoni. Uchaguzi na uamuzi upo mikononi mwako kutengeneza au kuharibu zaidi. ulichokipanda kwa kipindi chote ndo ulichokivuna kama hujaridhika na mavuno uliyopata rufaa haitosaidia dawa ni moja tu anza kupanda mazao yaliyo mema.
ReplyDeleteAlikuwa anataka umaarufu sasa yamemkuta, umaarufu hautafutwi kwa kukaa uchi, ungebuni kitu cha maendeleo mbona ungepata umaarufu tu, Wewe ukaona kukaa uchi kwenye jamii ndio utapata umaarufu, pole we.
ReplyDeletebig up Suguuuuu
ReplyDelete