WAZIRI Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye amekionya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutopitisha mgombea urais kwa njia ya rushwa kwa vile kufanya hiyo kutawaingiza wapinzani Ikulu.
Sumaye ambaye ni miongoni wa makada wanaowania kuteuliwa na CCM kugombea nafasi hiyo, aliyasema hayo juzi mjini Bariadi alipowashukuru wana CCM 45 waliomdhamini mkoani hapa .
Akizungumza na baadhi ya viongozi wa chama hicho na wadhamini hao, aliwashukuru waliomdhamini na kueleza kuwa ikiwa CCM itapitisha wagombea kwa njia za rushwa utakuwa mwanzo wa vyama vya upinzani kuchukua nchi.
“Nyinyi kama wajumbe wa NEC mtambue kuwa Tanzania kwa sasa tunahitaji kiongozi atakayetuvusha, tukichagua kwa rushwa tunawapatia wapinzani nafasi kuingia Ikulu hivyo chama changu kinapaswa kisipitishe mtu kwa rushwa,”alisema.
Alisema sababu kubwa itakayofanya wapinzani kuongoza nchi ni rushwa ndani ya CCM aliyoeleza kuwa imekithiri kwa kiwango kikubwa hasa kwa sasa kuelekea kipindi cha Uchaguzi Mkuu.
“Sijatoa rushwa tangu nianze kutafuta wadhamini , watu wanajitolea tu kwa mapenzi yao kunidhamini sina haja ya kuwanunua watu ninaowapata nawashukuru kwa maana mapenzi yametoka kwao kunidhamini siyo kwa sababu fulani, ”alisema.
Sumaye: Upinzani wataingia Ikulu CCM Wakipitisha mtoa Rushwa
0
June 19, 2015
Tags