Ali Kiba Kataja Sababu za Kwanini Hamfollow mtu Hata Mmoja Instagram

Ali Kiba 
Ali Kiba ni staa kwenye muziki wa Bongo Fleva.. kama wewe ni mtumiaji wa Instagram utakuwa umeona kwamba Ali Kiba haja-follow mtu yoyote ukitembelea mitandao ya kijamii ya Ali Kiba utaona ya kuwa ana mashabiki wengi wanaomfuatilia kupitia mitandao hiyo.

Katika post ya Instagram kwenye page ya Mseto East Africa ambao walikaa na kuongea na Ali Kiba na kumuuliza swali hilo, majibu yake ni haya hapa


  • “Yea si follow mtu kwasababu, kwanza kabisa nafanya kazi na watu wengi kuna akina TUVA kuna watu kibao lakini watu wa Media ndio tuko nao karibu,sasa wengine walikua waki complain nikawa naogopa zile lawama nilichoshauriwa na hao wenyewe kwamba ni heri ni si follow mtu na vile vile nilipenda ivyo kutokana na promotion ya ujio wangu ambao ulikuwa unakuja ili niweze ku concetrate na account yangu nijue mafans wangu wanataka kitu gani wanani advice kitu gani na pia imesaidia naona jinsi gani wako serious namimi kwasababu naongea nao,kuna wengine wananipa challenge kuna matusi uhmm ni vitu vya kawaida na vile vile wanapokuwa wananisema wananijenga wananitengeneza kiasi fulani,wananibadilisha ni wapi nimekosea naweza kubadilisha”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad