CCM Wamjibu LOWASSA........Wasema Kuhama kwake Hakuna madhara na kwamba Watapata ushindi wa kishindo

Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Dar, Juma Simba Gaddafi  jana  aliongoza  mkutano  wa  CCM  na  waandishi  wa  habari  uliofanyika  Peacock Hotel Dar, na  haya  ndo  mambo  aliyoyasema;


"CCM inatoa shukrani kwa ushirikiano mlioutoa katika Mkutano wetu Mkuu wa Kumtambulisha Mgombea Urais Dk. Magufuli pale Mbagala, CCM ni Chama chenye busara tumeona tuwashukuru

"Tume ya Uchaguzi tunawaomba wawe makini kuongeza Mashine na Watendaji ili watu wapate nafasi kujiandikisha na watumie fursa yao Kupiga Kura… CCM tuna uhakika tutashinda.

"Kingine tunawashukuru waliojitokeza Kugombea nafasi mbalimbali za Ubunge na wajitokeze kwa wingi pia kupiga kura…

"Tumemaliza Uchaguzi Dodoma na kumpata Mgombea wetu Dk. Magufuli, tunajivunia kwa sababu ana rekodi nzuri…

 "Tuna imani CCM itaendelea kuongoza 2015 mpaka 2020, tumefanya mengi yanayokubalika."

Akiongelea  sakata  la  Lowassa  kuhamia  CHADEMA, Gaddaf  alisema;

"Yeye aliingia CCM kwa ridhaa yake hakuna mtu alimlazimisha, ametoka kwa ridhaa yake na CCM itabaki kuwa CCM… Wafuasi walikuwa ndani ya CCM, kuondoka kwake ameondoka yeye na sio wa kwanza kuondoka.

"Mtu akitoka huwezi kujibu kwa nini ametoka, nawathibitishia mtu yoyote akitoka CCM itabaki imara… Tutashinda asubuhi kweupe…

"Kama Lowassa angekuwa anaondoka na watu wengi ungewaona jana, lakini alikwenda yeye akarudisha kadi… watu wengi wanatoka kwenye Chama na CCM bado iko imara."

Akiongelea  kuhusu Uteuzi wa Mgombea wa Urais CCM Dodoma, Gaddaf  alisema;

"Mkutano Dodoma tuliumaliza, lakini tumekwenda kwenye NEC Wajumbe wako 360, walipiga kura majina matano na Wagombea wote wa Halmashauri Kuu akiwepo Rais, Waziri Mkuu na Lowassa walikuwepo… kama asingekuwepo hayo yangesemwa, lakini alishiriki na alipiga Kura"

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Si mpaka muibe kura,nyie subirini tu naona hamsomi alama Za nyakati.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad