Mtume Mohammad (SAW) katika moja ya hadithi zake aliainisha tabia kuu tatu za mtu mnafiki.
Kwanza, mtu mnafiki akizungumza husema uongo.
Pili, mtu mnafiki akiahidi hatekelezi
Tatu, mtu mnafiki akiaminiwa hufanya hiyana.
Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kimetuonesha sifa hizi za mnafiki dhahiri kwenye sakata hili la kuwapokea kwa mbwembwe madiwani waliotoka CCM Monduli.
Madiwani hawa wametoka CCM kufuatia kukatwa jina kwa Waziri mkuu 'mstaafu' Edward Ngoyai Lowassa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania kuteuliwa kugombea nafasi ya urais kwa kupitia CCM.
Kitendo cha kuwapokea madiwani hawa kwa mbwembwe tena huku pakitumika maneno kama "safari ya matumaini bado inaendelea" ni kitendo cha fedheha sana kwa chama.
Wakati Zitto Kabwe akiondoka/ akiondolewa CHADEMA tuliona wale walioamua kuondoka nae walivyoitwa kila jina baya mitandaoni na hata baadhi ya viongozi walijitokeza kuwakandia waziwazi.
Tumeona namna gani Edward Ngoyai Lowassa alivyotukanwa kila tusi na viongozi wa CHADEMA. Ameitwa mwizi, fisadi, , mnyang'anyi na majina mengine mengi. Na hata wafuasi wake 4u movement tuliona walivyopewa maneno mabaya humu.
Tumeona viongozi wa CHADEMA wakiponda tabia ya kupokea wanachama waliokimbia vyama kwa sababu ya migogoro ya kimaslahi mara kwa mara.
Kwa hayo machache najiuliza hivi yale maneno ya kuponda watu yalijitokeza sababu walihama CHADEMA? Kumbe kuhama ni kosa lakini kuhamia ni sahihi? Kumbe hawa wafuasi wa Lowassa walikuwa wachafu walipokuwa CCM lakini wakiwa CHADEMA ni wasafi? Hivi mtu akija CHADEMA anasamehewa dhambi??
Tabia ya kuyarudi maneno yenu imekuwa ya kawaida sana lakini kwa hili sasa mmejifedhehesha sana. Miaka michache iliyopita mliwaita CUF kila jina baya mara CCM B, mara vibaraka, mara mas**ga nk lakini baada ya muda mkaungana nao na kuunda UKAWA. Mlimfukuza Kafulila kwa mbwembwe lakini leo mpo nae UKAWA huku mkimsifu.
Sitashangaa kesho mkiungana na ACT ili tu mtimize malengo yenu.
CHADEMA tambueni mlichokifanya ni kitendo cha hovyo mno, mmewaonesha watanzania mlivyo walaghai na opportunist wakubwa. Mmeonesha kila tabia za kinafiki na kizandiki na msivyo na msimamo.
Tabia kama hizi zitawafanya ikulu muisikie redioni tu na kuishia kulalamika kwamba mnaibiwa kura kumbe mnajihujumu wenyewe.
chadema hayo ni maneno yasiwaogopeshe kabisa. Lowasa akija mchukueni tu.peoples power kwa saana.
ReplyDeleteHuyu hayo maneno anawaandikia watoto wadogo ama watu wazima tunaojua kwamba ndani ya ccm hakuna anayeweza kusimama akatuambia nani msafi? Ccm walipokuja na msemo wa kuvua gamba is there anyone who did vua gamba??? Je Kikwete alipoingia ikulu aliingia na pesa za nani? Je anatoka ikulu akiwa amevuma kwa haki?
ReplyDeleteTafadhali msituone watoto, Lowasa na ccm wote ni wachafu. Wafuasi huwa wanafuata tu pesa au mapenzi ya kweli juu ya ideology...that's human nature
Wewe haujui kuwa chadema ni wanafiki hawawezi kupata nchi hata wadhikili uchi tuna jua hao wote ni waharusha waende tu hata Ruasa awafate ccm haitishiwi nyau
ReplyDeleteMimi sio mtanzania ila Chadema niliipenda sana hapo nyuma ila nilipo fuatilia vizuri sera zao na matamshi ya viongozi wao na nithamu yao duuh kweli niliona kwamba hamna chochote ila ni wale wanao jitafutia umaarufu na mali na uongozi.
ReplyDeleteKwahiyo kila mwana Mwonduli ni Lowassa? acha umbege wewe, wale ni wanachama sio Lowassa, harafu akili zenu zimeganda? yaani tofauti hapo hamioni
ReplyDeletemwandishi nakupongeza kwa jinsi ulivyoandika, hakuna ubishi kwamba chadema ni walaghai, wanafiki na wazandiki, mimi binafsi hilo nalijua siku nyingi ni watu wanaotafuta sifa kwa wananchi wakati uwezo wao wa kufiri ni mdogo, nami niungane na mwansdishi wa 10.17pm kwamba hawatakaa wapate nchi
ReplyDeleteNdugu zangu mliotangulia nimesoma msomi yenu wote nikagundua Kua ninyi hamjui siasa ni mchezo mchafu? Hua namshangaa mtu
ReplyDeleteMishipa ya Shingo ikimtoka kubishana kuhusu siasa, siasa ni game Kama football mtu yeyote akijiunga na upinzani toka Chama tawala wewe kinakuuma kitu gani kwa wanasiasa wao wanaingiza cku huku nyuma Sisi tunachukiana , aje edo au yeyote anapokelewa ataongoza nchi kwa sera za chadema sio za .......
Ndugu uliochangia juu yangu, una mawazo yanayo fanana na mimi. Siku zote siasa ni kama mchezo wowote uwe wa mpira/vinginevyo. Unaweza ukawa na ndugu yako yuko team B na wewe team A mkaingia kushindana na mkacheza gem ikapelekea hata kuumizana lakn mwisho wa siku mshindi anapatikana hivyo ndivyo ilivyo katika siasa. Na ndo maana waswahili wanasema, wagombanao ndyo wapatanao so, si ajabu hao wanachama A kuhamia B.
ReplyDelete